Ommy Dimpoz akiri kununua views Youtube kwenye wimbo wa Wanjera

Ommy Dimpoz akiri kununua views Youtube kwenye wimbo wa Wanjera

Kwahiyo na kina Chris Brown,Adelle na wao wananunua viewers? Wale wana views zaidi ya milioni 200 kwenye video zao YouTube
Adele hello ina views billion 1 na kitu ka million mia 7 nyingne wiz khalifa see you again ina billion 2
 
Naomba nikurekebishe,sio kwamba kanunua views bali mtu kajitokeza na kumshawishi atoe hela hili apate views wengi kwenye video yake mpya na kutaka kuhakikishiwa ndio akatoa link na kufanyiwa kazi kama mfano bila yeye kutoa pesa yeyote,na kwa stly hiyo amegundua kuwa na views wengi mda mwingine ni michezo tu na sio kweli watu wameangalia.
 
Tatizo hawaamini kuwa Mondi keahawapiga lapa wakikumbuka wameanza wote juzi keshakuwa hatari mashabiki wake wanatoka pande zote za Africa, hicho ndio kinachowasumbua hawaamini kama mchizi keshatoboa. Bora wakae kimya wabaki na heshima zao kuliko kujigawa kwa kihoro walichonacho sana sana watapoteza mashabiki.
 
Ukiweza kununua nunua otherwise aache majungu ya uvunguni
 
Wanawake wengi huwa na tabia ya kujump into conclusion.....Nashangazwa sana tabia hii kuwa nayo wanaume pia...ndo kizazi chetu hiki...


Facts
1. Hakuna mahali ommy kamtaja Diamond...Kasema kaambiwa wasanii wanaofanya hivyo wapo so it can be anyone...Na hakuna alipoashiria kuwa ni Diamond...Huku ni kujishtukia na kujump kwenye conclusion...

2. Jambo la kununua views youtube sio ishu mpya wala kusema ni ya waafrica, hii hufanyika popote pale na wengi tu wanafanya...Na ni katika mijadala ya muda mrefu tu mitandaoni..Na ni kitu ambacho KINAWEZEKANA

3. Wapo wasanii wakubwa tu wameshawahi kutuhumiwa kununua views akiwemo justib beiber.. Tuhuma ambazo baadhi ya kampuni za statistics zilisema ni zina ukweli...

Musicians accused of 'buying virtual fans' on YouTube


4. Watanzania wengi ni wajinga. Wakishapenda kitu akili zao sijui huziweka wapi. Yani mtu ni mjinga halafu anajifanya mjuuuuuzi...JAMANI SIMU ZETU SI ZA KUPIGIA PICHA TU NA KUINGIA SOCIAL NETWORKS...Kuna kitu kinaitwa google mnaweza kuwa mnakitumia kabla ya kuja kupost utumbo humu...

5. Kuna mataahira watakuja kujibu na we si ununue? Hapa tunaongelea facts..Kwamba inawezekana au laa...Na ukweli ni kuwa inawezekana na wapo wanaofanya...Na si ujinga kufanya kama hutoshtukiwa, ni njia mojawapo ya kujitangaza..Sema wabongo wengi akili zao fupi wanadhani viewers wa youtube ni kwa ajili ya sifa tu...Ile ni njia ya kujulikana zaidi ulimwenguni....
 


Hivi kweli umeisoma hii article au unataka Kupotezea watu muda? Haionyeshi Ni jinsi gani ya kununua viewers kitu wanachojaribu kuelezea Ni how to earn more views on your YouTube video. Na njia wanazoeleza humu Ni za kawaida Tu labda Nina wasiwasi hujasoma kitu ulichopost hapa. Wanaseme use the social medias, kama Facebook, blogs na nyinginezo. Pale kwenye Youtube channel yako mtu akifungua Tu video inaanza kucheza and counting. Labda ulitaka kutufahamisha nini kwenye hii post yako.
 
Hivi kweli umeisoma hii article au unataka Kupotezea watu muda? Haionyeshi Ni jinsi gani ya kununua viewers kitu wanachojaribu kuelezea Ni how to earn more views on your YouTube video. Na njia wanazoeleza humu Ni za kawaida Tu labda Nina wasiwasi hujasoma kitu ulichopost hapa. Wanaseme use the social medias, kama Facebook, blogs na nyinginezo. Pale kwenye Youtube channel yako mtu akifungua Tu video inaanza kucheza and counting. Labda ulitaka kutufahamisha nini kwenye hii post yako.
umesoma hadi mwisho?au lugha inakupiga chenga?
 
Hizi tuhuma zimekuwa kama za kawaida zinapozungumzwa hasa kama Zinagusa pande pendwa zinakanuswa vikali na kejeli juu
 
Leo katika pita pita zangu kwenye YouTube nikakutana na interview ya Ommy Dimpozi.
Nilitamani sana kusikia maana mda mrefu sijamsikia.

Nilishangaa sana jinsi alivyokuwa anaongea.
 
Back
Top Bottom