Ommy Dimpoz azuiliwa kuingia Marekani!

Ommy Dimpoz azuiliwa kuingia Marekani!

Alitaka kuleta mambo ya town kisomo kwa wale wajomba wa immigration pale airport, thubutu yake!.
 
Akuuu mie nashangaa mbona yamekuwa haya wakati kila muda twasikia wakienda vizuri na kurudi vizuri
Evelyn Salt
 
Attachments

  • 1424111551949.jpg
    1424111551949.jpg
    25 KB · Views: 494
Akuuu mie nashangaa mbona yamekuwa haya wakati kila muda twasikia wakienda vizuri na kurudi vizuri
Evelyn Salt

Soma post zilizo pita utagundua kilicho sababishwa kurudishwa!
 
Aisee
Nasikia viza aliyokuwa amekata haikuwa ina mruhusu kufanya show nchini marekani! Inasemekana alitakiwa kukata viza ambayo inaonesha ana kwenda kufanya show nchini marekani na bila shaka gharama zake ni tofauti na ile ya kwenda kutembea!Viza aliyo kuwa amekata ilikuwa ya kwenda kutembea tuu na kusalimu ndugu na jamaa si kufanya show!

Sasa kilicho tokea alipo fika uwanja wa ndege akazuiwa kuingia nchini marekani kwani viza aliyo kuwa amekata ilikuwa haimruhusu kufanya show ni baada ya kuhojiwa!

Ninacho jiuliza kwanini watanzania tunafikiri kila sehemu tunaweza kufanya ujanja ujanja? Kwanini hatupendi kufata utaratibu?Bahati mbaya zaidi show ilikuwa imesha andaliwa na jana kama si juzi ilibidi afanye!

Yani mtu anataka pesa halafu anaogopa kuingia gharama kukata viza itakayo mruhusu kufanya show nchi ya watu!

Huu sio ujanja ni ujinga tu.
 
Unaomba visa online na unatoa sababu inayokupeleka huko kwenye form. Ukiitwa kwenye usaili lazima uulizwe unaenda kufanya nini. Sasa kama kwenye form na kwenye usaili kajaza vingine na alipofika huko akasema vingine basi huo ndio ujinga wenyewe unaosemwa kila siku
 
Kuna mwingine aliulizwa pale ubalozini kwanini anataka akasome chuo Us wakati hata China au India vyuo vipo basi akajibu kua ni anapenda tu Us
Hhhhhhaa akatemwaaa
 
Ommy dimpoz anaingia Tanzania Leo usiku,baada ya kurudishwa na kutakiwa kupanda ndege inayofata,meneja wake ndio amesema hivyo
 
Ukute huwa hata kodi za mapoto hawalipi ndo maana wanaenda kama tourist
 
Back
Top Bottom