Ommy Dimpoz: Hata nikiacha muziki nitaishi bila shida yoyote, siyo chawa wa GSM Wala Joho, baba yangu alinitelekeza

Msanii Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu mambo mbalimbali, kama vile wapi anapata pesa, ukaribu wake na GSM na aliyekuwa Governor wa Mombasa Hassan Joho na kuhusu kutelekezwa na baba yake mzazi.

Akiongea katika kipindi cha Salama Na Ommy Dimpoz amesema yeye Kwa Sasa yupo vizuri kifedha hivyo hata akiacha muziki ataishi bila shida yoyote Ile. Ommy Dimpoz amesema Kwa Sasa yeye ndiye mwenye tenda ya kushughulika na matangazo yote ya GSM kupitia kampuni yake ya marketing aliyoianzisha ambayo imeajiri wataalamu wa kutosha. Kampuni hiyo inajihusisha na online branding zote za GSM, posters nk.

Ommy Dimpoz amewashauri wasanii wengine kuwa na plan B katika maisha Kwa kutumia influence waliyonayo kufanya biashara zingine badala ya kutegemea muziki peke yake. Pia Ommy Dimpoz amesema yeye siyo chawa wa GSM Wala Joho.

Kuhusu ukaribu wake na Joho Ommy Dimpoz amesema Joho amemsaidia sana kipindi alichokuwa akiumwa Kwa kuwa alibeba gharama karibia zote za matibabu ya south Africa na hospital ya Nairobi. Hivyo ukaribu wao umekuwa ni kama ndugu kwani mtu anayekusaidia katika matatizo hasa ya ugonjwa bond inayokuwepo ni kubwa.

Kuhusu GSM, Ommy Dimpoz amesema ukaribu wao ni wa kibiashara zaidi, Ommy Dimpoz amesema alianza kutangaza bidhaa za GSM kama Balozi kuanzia mwaka 2015, na kwamba Kwa Sasa amefungua kampuni yake ya marketing ambayo ndiyo inayohusika na matangazo yote ya GSM.

Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu Mahusiano hafifu kati yake na baba yake na kusema hali hiyo imesababishwa na ukweli kwamba baba yake alimtelekeza akiwa mdogo hivyo Ommy Dimpoz kulelewa na mama yake mdogo pamoja na bibi yake baada ya mama yake kufariki.

Amenukuliwa akisema "Sina kinyongo naye", Ommy Dimpoz anasema kutekeleza huko kumefanya kukosekana bond kati Yao na si kwamba yeye ana mchukia baba yake. Baba yake Ommy Dimpoz na Mama yake hawakuwahi kuoana, hivyo baba yake alikuwa anaishi na mwanamke mwingine na familia yake.

Kuhusu album

Ommy Dimpoz amesema yupo mbioni kuachia album yake ambayo anaiandaa huku executive producer akiwa pfunk majani.

Joho... GSM.. 1+1= 11[emoji818][emoji817][emoji322]
 
Mimi nafikiri mzazi anatakiwa ajijenge asihitaji kulelewa na mtoto huko uzeeni etc...
Jukumu la mzazi ni kumlea mtoto, na wala siyo mtoto kumlea mzazi. Acheni kutaka mambo yaende kinyumenyume!
Hili la watoto kutokuwa na bond nzuri na wazazi Tanzania ni kubwa mno ,ila watu hawajui tu.

Wanaume mnavozaa hakikisheni mnaleaa msifikili kuwa baba ni kuzaa tu, bila malezi na kutengeneza ukaribu zaidi na mtoto basi unajiandalia bomu lako mwenyewe na badae hakuna mtoto atakaye kujali, niamini Mimi ......

Kama mtoto amekuwa Hana ukaribu na wewe usifikili akija kukua atakuja kuwa na feelings zozote na wewe et baba yake ,hata kwa uchawi au Nini yaani hapa mtoto anakuwa Hana chembechembe za huruma na wewe kwani toka utotoni ulishindwa kutengeneza hisia zako juu yake hili swala Mimi naliona hata kwenye familia kabisa. Wazazi wanajisahau watoto wanakua hovyo hovyo tu bila kuwa na malezi ya wazazi, wakishakuwa wakubwa automatic wanajikuta hawana hisia zozote na baba, kwani muda mwingi katika ukuaji wametengwa hawajapata ule upendo,ukaribu na umoja ,unafikili akikua atakujali?

Kuhusu ommy kumtelekeza baba yake Mimi hata sishangai kabisa ,na mtaani wapo wengi sana nawaona .
 
Akumbuke kuwa alikua mahututi hospital, kwa uwezo wake Mungu akapona , so amshukuru sana Mola wake, so anapaswa kutubia na sio kurudia miziki kwa mara nyingine.
 
Wapo pia ambao wanapata malez mazur tu lkn wakishakuwa wanakuwa hawana bond na baba zao..mm nina mifano hai
hawajakuona aende zake huko km hamtaki hakumjali basia asitumie jina lake kujitanabaisha hapa eti baba km mama alikuwa mapepe je??unajua nini weye?? nina shaka labda siyo baba ake wa ukweli!! damu inauma sana!
 
Hili la watoto kutokuwa na bond nzuri na wazazi Tanzania ni kubwa mno ,ila watu hawajui tu.

Wanaume mnavozaa hakikisheni mnaleaa msifikili kuwa baba ni kuzaa tu, bila malezi na kutengeneza ukaribu zaidi na mtoto basi unajiandalia bomu lako mwenyewe na badae hakuna mtoto atakaye kujali, niamini Mimi ......

Kama mtoto amekuwa Hana ukaribu na wewe usifikili akija kukua atakuja kuwa na feelings zozote na wewe et baba yake ,hata kwa uchawi au Nini yaani hapa mtoto anakuwa Hana chembechembe za huruma na wewe kwani toka utotoni ulishindwa kutengeneza hisia zako juu yake hili swala Mimi naliona hata kwenye familia kabisa. Wazazi wanajisahau watoto wanakua hovyo hovyo tu bila kuwa na malezi ya wazazi, wakishakuwa wakubwa automatic wanajikuta hawana hisia zozote na baba, kwani muda mwingi katika ukuaji wametengwa hawajapata ule upendo,ukaribu na umoja ,unafikili akikua atakujali?

Kuhusu ommy kumtelekeza baba yake Mimi hata sishangai kabisa ,na mtaani wapo wengi sana nawaona .
Ommy Apache visingizio! Inakuwaje awe na bond na Joho akose kuwa bond na babake? Joho anampa malezi gani?🤣
 
hawajakuona aende zake huko km hamtaki hakumjali basia asitumie jina lake kujitanabaisha hapa eti baba km mama alikuwa mapepe je??unajua nini weye?? nina shaka labda siyo baba ake wa ukweli!! damu inauma sana!
Huu ujinga wa eti asitumie jina kwani aliliomba, mtu yoyote ana haki ya kujinga na mtu asiyemkubali bila kujali ni nani kwake. Atang'ang'ania vipi sehemu ambapo roho yake haipakupakubali kabisa, nina watoto wanne lakini kama atatokea mmoja au zaidi ya mmoja wakanitenga kwa sababu zao siwezi kuhangaika kudai waache kutumia jina langu as the matter of fact sina mamlaka ya kumzuia mtu yoyote duniani kutumia jina lolote hata hili nililowapa watoto kuwa ndiyo ubini wao.
 
Uongo ,uongo .uongoo

Kuna mengine nnje ya pasia

Yaani unalipwa mamilionn na kwa kuweka kurasa za biashra tu hpn Kuna kitu ipo siku itajulikana

Nina mashaka na wasiwas sna na wewe
Ombi langu tunza tu rinda lako mkuu kunbuka uliuguwa sna Kia's Cha kukaribia kukata kuondoka

Sasa unayo yafanya itakucost
 
Na man u wanaukame wa win win win win draw draw win win labda katumika kuhamasisha ushindi.

Nakumbuka Arsenal walishikwa na matukio ya rangi ya upinde na tangia hapo wakaanza kufanya vizuri sana
Hii yote ni akili ya wivu kmmk yaaani mwanaume mwenzako akifanikiwa ANALIWA akipotea kwenye game HAKUJIONGEZA kweli sisi kiumbe kinachoitwa BINADAMU ni hatari sanaaa
 
sina mamlaka ya kumzuia mtu yoyote duniani kutumia jina lolote hata hili nililowapa watoto kuwa ndiyo ubini wao.
Umejibu na mihemuko mkuu ona !! neno ''kujitanabaisha'' na mipicha kabisa, ajili ya viji centi vya mawazo! haya ndo matatizo i!!

well!! kwa mfano wenye jina ''Juma, jonh, somoye. Marwa, chacha, Hamisi! wako wengi! tatizo linakuja unatumia jina langu/picha!! ........ siyo uniunganishe mimi km Baba yako na picha juu ''sawa!

Mtoto wangu hawezi nikataa kwa namna yeyote ile iwayo ''Nakuapia'' km ikitokea wa hivo?? siyo wangu huyo! hata ufanyeje! hata achanganyikiwe!

Wooote! tuliolelewa na wazazi wote wawili kamwe hatukuishi Nao km Malaika, tulikwazana, lkn haikutufanya tuwakatae baada ya kutoboa, mpaka tunaishi nao! kwa upendo wa juu ,.... tena sana sijkosea!

Mzazi akiumwa! mtoto unajisikia nawe unaumwa ! ndo Mungu alivyo tuweka ivo!! mfano! Mfalme Daudi Rafiki wa Mungu aliwindwa na kutaka kuuawa na Mwanae kabisaaa mpendwa wa kumzaa!!

Lkn hakuacha kuomboleza! kifo chake! wewe nani umshinde Mtu aliye ongea na Mungu tit for tat!......na km ni mwanao wa Mauno yako, Damu yako, halafu akukatae!! siyo rahisi! eebanaee!! Hatoboi ''

Utake usitake atasimangwa na sisimizi wasio ongea! atakufa kachoka mno na Mateso ya Dunia, inafanya kazi mpaka sasa!!! lkn akienda salama siyo wako huyo!!km Musa alivondoka kwa Faraoh! tena kwa jeuri!

Km unabisha una wazazi jaribu tu uone moto!!!......utakunya juu! halafu unangoja chini! wazazi ni miungu wa dunia! aliye sema ''uwaheshimu'' siyo mjinga! mtu atakaye kuwekea kigingi usiwaheshimu analo!!

Na waziri aliye Mdanganya Abusalom ampindue Baba yake, jamaa alijinyonga, Mwanao hawezi kukuacha hivi hivi!! km mzazi mmoja wapo hana laana hiyo!!

eti ukasema nenda! utaweza lkn! utakuwa na laana usiyoijua, ulizia kwa wakubwa zako huko nyuma nani alifanya mambo km hayo! na km huyo mwanao ni ke haolewi ng'oo!! watu wakija wakisikilizia!

Historia yakeee! wanakula kona, na hata km akiolewa/kuoa, hapo hilo ndo litakuwa simango kuuu ndoani!! ukimuacha mkeo, huyo huyoo atakuimbia wimbo huo huo!! ivi..... ''Ndivyo Mlivyo''...... halafu utaumiaaaaa kiasi cha kujitoa roho!!

Wako wazazi wapende tu! piga nao story, mwanangu akiamua kutoka sikubali kirahisi!...sababu hatuna laana hiyo!
 
Msanii Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu mambo mbalimbali, kama vile wapi anapata pesa, ukaribu wake na GSM na aliyekuwa Governor wa Mombasa Hassan Joho na kuhusu kutelekezwa na baba yake mzazi.

Akiongea katika kipindi cha Salama Na Ommy Dimpoz amesema yeye Kwa Sasa yupo vizuri kifedha hivyo hata akiacha muziki ataishi bila shida yoyote Ile. Ommy Dimpoz amesema Kwa Sasa yeye ndiye mwenye tenda ya kushughulika na matangazo yote ya GSM kupitia kampuni yake ya marketing aliyoianzisha ambayo imeajiri wataalamu wa kutosha. Kampuni hiyo inajihusisha na online branding zote za GSM, posters nk.

Ommy Dimpoz amewashauri wasanii wengine kuwa na plan B katika maisha Kwa kutumia influence waliyonayo kufanya biashara zingine badala ya kutegemea muziki peke yake. Pia Ommy Dimpoz amesema yeye siyo chawa wa GSM Wala Joho.

Kuhusu ukaribu wake na Joho Ommy Dimpoz amesema Joho amemsaidia sana kipindi alichokuwa akiumwa Kwa kuwa alibeba gharama karibia zote za matibabu ya south Africa na hospital ya Nairobi. Hivyo ukaribu wao umekuwa ni kama ndugu kwani mtu anayekusaidia katika matatizo hasa ya ugonjwa bond inayokuwepo ni kubwa.

Kuhusu GSM, Ommy Dimpoz amesema ukaribu wao ni wa kibiashara zaidi, Ommy Dimpoz amesema alianza kutangaza bidhaa za GSM kama Balozi kuanzia mwaka 2015, na kwamba Kwa Sasa amefungua kampuni yake ya marketing ambayo ndiyo inayohusika na matangazo yote ya GSM.

Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu Mahusiano hafifu kati yake na baba yake na kusema hali hiyo imesababishwa na ukweli kwamba baba yake alimtelekeza akiwa mdogo hivyo Ommy Dimpoz kulelewa na mama yake mdogo pamoja na bibi yake baada ya mama yake kufariki.

Amenukuliwa akisema "Sina kinyongo naye", Ommy Dimpoz anasema kutekeleza huko kumefanya kukosekana bond kati Yao na si kwamba yeye ana mchukia baba yake. Baba yake Ommy Dimpoz na Mama yake hawakuwahi kuoana, hivyo baba yake alikuwa anaishi na mwanamke mwingine na familia yake.

Kuhusu album

Ommy Dimpoz amesema yupo mbioni kuachia album yake ambayo anaiandaa huku executive producer akiwa pfunk majani.

Naam
 
Back
Top Bottom