Ommy Dimpoz taabani akimbizwa Ujerumani

Ommy Dimpoz taabani akimbizwa Ujerumani

Sema uzuri wa Hospital Za Bongo mtu Unaambiwa Ukweliii ila ukienda Nje lazima Wakudanganye danganye ili wakupige Hele Foreigner hadi zikiwa zinataka kuisha wanakwambia Una Ca ila Cancer ya Koo TZ rate yake imekuwa Kubwa sana Hasa kwa Vijana Umri wa Ommy ngoja tusubiri na Tuone
Ni kwann rate imekuwa kubwa sana?
 
Watu wazima hawa wakuogopwa sindio alisema mam yake nanii kampakata? Sasa naye anapakatwa? Jaman midomo.
 
Ugua pole Ommary...Mungu akuponye.

Lakini humu jf ulishawekwa uzi unaitwa "mapenzi ya njia ya mdomo ni chanzo kikuu cha saratani ya koo"
Haya ndio yalizunumzwa mule...nime nukuuu


Saratani imeendelea kuwa tishio hapa nchini huku hofu ikiendelea kuikumba jamii kutokana na wataalamu wa afya kushindwa kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari. Takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha ongezeko la saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012.

Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Ocean road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. "Saratani ya mdomo ipo, na nyingine zinasababishwa na zinaa " anasema Dk Mwaiselage.

Tafiti za saratani

Tafiti mbalimbali zimewahi kufanyika nchini na kubaini kuwepo kwa ongezeko la saratani ya mdomo.Utafiti uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini aina za saratani 1,594, kati ya hizo 509 zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003 pekee.

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa kati ya saratani 509 za mdomo, saratani 242 zilisababishwa na Virusi vya Human Papiloma ambavyo hutokana na zinaa. "Ninachojua mimi ni kuwa Virusi vya HPV husababishwa na magonjwa ya zinaa, hivyo mtu anayeugua saratani ya aina hiyo, imetokana na zinaa," anasema Dk Mosha.

Wanaume waathirika zaidi wa Saratani

Takwimu hizo ni zile zilizopatikana kwa watu waliokwenda kufanyiwa uchunguzi katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Dk Mosha anasema kuwa wanaume ndiyo huathiriwa zaidi na saratani ya mdomo ambapo kwa hapa nchini, asilimia 53 ya wanaume waliofika MNH kwa ajili ya vipimo, walibainika kuugua saratani hiyo, huku wanawake wakiwa ni asilimia 47. Utafiti kama huo ulifanywa pia na Dk Amos Mwakigonja, mkuu wa Idara ya Patholojia katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MUHAS).

Dk Mwakigonja alifanya utafiti wa saratani ya mdomo aina ya Kaposi's Sarcoma ambapo wagonjwa 78 walibainika na saratani hiyo kuanzia mwaka 1990 hadi 2003. "Saratani za mdomo zipo za aina nyingi na zimetofautiana kulingana na visababishi vyake," anasema Dk Mwakigonja. Katika utafiti wake Dk Mwakigonja alibaini kuwa wanawake wengi walikuwa na saratani ya mdomo aina ya Kaposi's Sarcoma kuliko wanaume.

Hata hivyo, utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 50 ya wanaume walikuwa na saratani ya mdomo hatari zaidi (systemic) kuliko wanawake ambao ni asilimia 37.

Mapenzi kwa mdomo husababisha maradhi

Dk Mwakigonja anasema kuwa mapenzi yoyote kwa njia ya mdomo lazima yasababishe maradhi ya zinaa iwapo mmoja ameambukizwa. Pia anasema kwamba sampuli nyingi za wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao (mashoga) zilibainika na saratani ya mdomo. Utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa Shahada ya Uzamivu ambao ulionyesha kuwa wagonjwa wengi wa saratani ya mdomo walikuwa ni wanaume wenye umri wa miaka kati ya 38 na kuendelea na wanawake ni 31.

Ufatiti wa WHO Tanzania

Shirika la Afya Duniani (WHO) pia lilifanya utafiti mwaka 2010 nchini kwa kushirikiana na Kituo cha Taarifa za HPV, ambapo ilibainika kuwa asilimia 20 ya saratani za koo na mdomo nchini zinasababishwa na ufanyaji wa mapenzi kwa njia ya mdomo.

Taarifa hizo za WHO zinaeleza kuwa wanaume 747 hugundulika na saratani ya mdomo kila mwaka wakati wanawake 472 hubainika na saratani hiyo pia. Wakati huohuo, wanaume wanaopoteza maisha kutokana na saratani hiyo ni 444, kwa mwaka na wanawake ni 270, kwa mwaka. Utafiti wa WHO umebaini kuwa saratani ya mdomo inashika nafasi ya sita katika aina 24 za saratani 24 zinazoisumbua zaidi Tanzania.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa wanaume wanaoathirika zaidi ni wenye umri wa kati ya miaka 15 na 55, ambao tayari wameshaanza kujihusisha na ngono. Kama maradhi mengine ya kuambukiza, Virusi vya HPV huambukizwa kwa urahisi zaidi kutoka kwa wanawake kwenda kwa wanaume kuliko kutoka kwa wanaume kwenda kwa wanawake. Utafiti huo uliodhaminiwa na mfuko wa Bill na Melinda Gates na Kituo cha Saratani na Mpango wa Utafiti wa Taasisi ya ICO unaeleza kuwa mitandao ya kijamii na picha za ngono ndiyo chanzo cha watu wengi kuiga ufanyaji wa mapenzi ya aina hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la The New York Times, tafiti zimefanyika na kubaini kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wanaobainika na saratani ya koo na mdomo duniani, husababishwa na Virusi vya Human Pappiloma vinavyotokana na magonjwa ya zinaa.Tafiti hizo zinaonyesha kuwa wagonjwa wengi wanaogundulika na saratani hiyo ni wanaume wenye umri wa kati, wenye uwezo wa kifedha, wasiovuta sigara wala siyo walevi waliokubuhu.

Utafiti huo ulibaini kuwa wanaume wapo hatarini zaidi kupata saratani ya koo inayosababishwa na Virusi vya HPV. Miaka ya 80, idadi ndogo ya watu waliougua saratani ya koo walihusishwa na maambukizi ya Virusi vya HPV. Kihistoria, watu waliobainika na ugonjwa huo, ni wenye umri wa miaka 70 kwenda juu ambao walikuwa ni wale walevi waliokubuhu na wavuta sigara.

Ilielezwa kuwa Virusi vya HPV vipo kwa wingi kiasi ambacho watu wazima wanaojihusisha na ngono ya aina yeyote ile, huweza kupata maambukizi ya zinaa hata kama siyo saratani. Hata hivyo ilibainishwa kuwa saratani isababishwayo na virusi vya HPV ni rahisi kuitibu kuliko saratani ya koo isababishwayo na tumbaku au pombe kali.

Virusi vya HPV ni nini?

Kwa jina la jumla, saratani ya koo au mdomo huitwa saratani ya kichwa na shingo. (Neck and Head Cancer) HPV ni miongoni mwa virusi hatari zaidi duniani visababishwavyo na magonjwa ya zinaa na vinaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili. Zipo aina zaidi ya 120 za HPV, baadhi huweza kuzalisha usugu (warts) ambazo si saratani katika sehemu za siri, mikononi na miguuni. Maambukizi ya HPV hufanyika kwa urahisi, hata kwa kugusana ngozi au majimaji, huku maambukizi mengine yakisababishwa na ngono.

Virusi hatari na vinavyosababisha saratani ni HPV-16, HPV-18, HPV-31 na HPV 45. Aina hii ya Virusi vya HPV husababisha saratani ambapo uvimbe waweza kujitokeza kwa ndani na unaweza usionekane ukilinganisha na vivimbe vingine vya saratani. Wataalamu wanasema HPV-16 na HPV-18 inahusishwa zaidi na saratani ya shingo ya kizazi na endapo mapenzi kwa njia ya mdomo yatafanywa na mtu mwenye uambukizo huu ni rahisi kuambukizwa.


Kutoka mitandao mingine kuhusu kansa ya koo

Vihatarishi vya kansa ya koo
Ingawa chanzo halisi cha kansa ya koo hakijulikani, mambo yafuatayo yanaweza kusababisha mtu kupata saratani ya koo. Hata hivyo, pamoja na kuwepo vihatarishi hivi, ni vigumu kueleza kwa ufasaha kwa nini mtu au watu fulani wanaweza kupatwa na kansa ya koo na mtu mwingine asipate. Vihatarishi hivi ni
  • Umri: Hatari ya kupata saratani ya koo huongezeka zaidi kwa watu walio na umri wa miaka 65 na kuendelea. Hata hivyo saratani ya koo aina ya adenocarcinoma inaweza kutokea hata kwa wanawake walio na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea.
  • Jinsia: Tafiti nyingi zimeonesha kuwa wanaume wana uwezekano wa kupata saratani ya koo mara tatu zaidi ya wanawake.
  • Uvutaji sigara: Wavutaji sigara wapo katika hatari ya kupata saratani ya koo ukilinganisha na wasio wavutaji.
  • Unywaji pombe wa kupindukia: Unywaji wa pombe kwa kiasi cha chupa tatu na zaidi kwa siku unamuweka mnywaji katika hatari ya kupata saratani ya koo ikilinganishwa na mtu asiyekunywa kabisa pombe. Aidha wanywaji wa kupindukia ambao pia ni wavutaji sigara wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya koo ikilinganishwa na wanywaji wa pombe wasio wavutaji sigara. Kwa maneno mengine, unywaji pombe pamoja na uvutaji sigara hufanya kazi kwa pamoja kuongeza uwezekano wa mtu kupata saratani ya koo.
  • Lishe: Kuna mjadala kuhusu mchango wa aina fulani za vyakula katika kusababisha saratani ya koo. Wakati watafiti wengine wanasema ulaji wa matunda na mboga mboga husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya koo, watafiti wengine wanapinga kuhusu suala hilo.
  • Unene kupindukia : Unene wa kupitiliza huongeza uwezekano wa kupata saratani ya koo aina ya adenocarcinoma.
  • Matatizo ya tumbo: Matatizo sugu katika tumbo yanayosababisha tindikali kurudi kwenye koo (acid reflux) kutoka tumboni husababisha madhara katika seli za koo na hatimaye kupelekea saratani ya koo kwa baadhi ya watu.
  • Tatizo sugu la kucheua kwa tindikali: Iwapo tatizo la tindikali kucheuliwa kwenye koo litaendelea kwa muda mrefu mpaka kuwa sugu, sehemu ya chini ya koo yaweza kuathiriwa na kusababisha hali ijulikanayo kitaalamu kama Barrett esophagus. Hali hii huongeza uwezekano wa kutokea kwa saratani ya koo.
Dalili za saratani ya koo
Mgonjwa mwenye saratani ya koo katika hatua za awali anaweza asioneshe dalili zozote zile. Hata hivyo, kadiri saratani inavyozidi kukua na kuenea, mgonjwa anaweza kuwa na dalili zifuatazo:
  • Chakula kukwama kwenye koo
  • Siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate
  • Maumivu wakati wa kumeza chakula hasa chakula kigumu
  • Maumivu kwenye kifua au mgongoni
  • Kupungua uzito
  • Kiungulia
  • Sauti ya mkwaruzo au kikohozi kikavu cha zaidi ya wiki mbili
Hata hivyo ifahamike kuwa dalili hizi zinaweza kutokea pia kwa baadhi ya magonjwa mengine tofauti na saratani ya koo. Hivyo ni vizuri kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
 
Eti mungu amfanyie hiki au mungu ampe kile!

BS.

Kwa nini huyo mungu asingeizuia hiyo hali.

Anazuiaje kama mtu alikuwa nafanya kitu cha kusababisha ugonjwa na akashauriwa aache lakini akawa mbishi je?
 
Dimpoz anasumbuliwa na koo ambapo katikati ya mwaka huu 2018 alifanyiwa operation katika moja ya hospitali kubwa nchini Afrika ya Kusini,licha ya kuonekana kuimarika kwa afya yake miezi kadhaa iliyopita lakini tatizo hilo limemrudia tena siku chache za hivi karibuni.awali kabla ya kwenda kupatiwa tiba South Afrika, madaktari wa muhimbili walimueleza kuwa ana dalili za kansa ya koo,jambo ambalo hakukubaliana nalo.
Dua za Watanzania zinahitajika kwa kijana wetu OmmyView attachment 970154
Naona chini ya hilo gazeti wamemalizia "Baba aomba tumuombee", je yy mgonjwa alikuwa anakumbuka muda wa kufanya maombi maana nakumbuka alipotoka Hosp. alituahidi tusubiri mambo matamu yanakuja ss kama anakumbuka ya duniani sijui kama ya akhera yake kama anakumbuka M/Mungu muziki kakataza amrudie mola wake na toba basi ndio jambo la msingi,huo ni mtihani Muumba kampa na ni ukumbusho kwake na kwetu ili tumkumbuke aliyetuumba tuishi ktk misingi aitakayo.
 
Ugua pole Ommary...Mungu akuponye.

Lakini humu jf ulishawekwa uzi unaitwa "mapenzi ya njia ya mdomo ni chanzo kikuu cha saratani ya koo"
Tushaambiwa na Nei na Mond kuwa mchizi hadind.i sasa hayo mapenzi kwa njia ya mdomo anayafanyaje? au tuamini jamaa anamombasiwa?
 
Source ya habari haiaminiki ila ommy hajapost kwa mda mrefu zaidi ya siku 16,hajapost kitu chochote Insta ambapo si kawaida yake,mara nyingi anapost kila baada ya siku mbili ila hii ya kukaa siku 16 bila kupost chochote possible anaumwa kweli.
 
Back
Top Bottom