Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Mwanamuziki na mkali wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ambaye yuko Afrika Kusini kwa matibabu, amewataarifu watanzania kwamba anaendelea vyema na sasa ana nafuu ijapokuwa bado anaumwa.
"Ugonjwa huu wa matatizo kwenye mfumo wangu wa chakula umenianza siku nyingi kidogo, nimekuwa nikihangaika kwenye hospitali tofauti nchini Tanzania na kwa wakati tofauti nilikuwa napewa majibu tofauti.
Wengine waliniambia koo langu limepata uvimbe na kusababisha kutoweza kupitisha chakula vizuri, wengine waliniambia nina kansa ya koo.
Lakini nakumbuka wakati wa kipindi cha harusi ya AliKiba nilikutana na Gavana, Joho wa Mombasa akanisaidia kunikutanisha na madaktari wengine nchini Kenya.
Vipimo vya nchini Kenya vilionyesha kwamba ugonjwa wangu ulisababishwa na kunywa kitu chenye sumu, na wakasema ukubwa wa tatizo nililokuwa nalo inabidi niende kutibiwa nje".
Amplifaya
Millard Ayo
Sent using Jamii Forums mobile app