Ommy Dimpoz: Ugonjwa wangu ulisababishwa kunywa kitu chenye sumu, inabidi niende kutibiwa nje

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mwanamuziki na mkali wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ambaye yuko Afrika Kusini kwa matibabu, amewataarifu watanzania kwamba anaendelea vyema na sasa ana nafuu ijapokuwa bado anaumwa.

"Ugonjwa huu wa matatizo kwenye mfumo wangu wa chakula umenianza siku nyingi kidogo, nimekuwa nikihangaika kwenye hospitali tofauti nchini Tanzania na kwa wakati tofauti nilikuwa napewa majibu tofauti.

Wengine waliniambia koo langu limepata uvimbe na kusababisha kutoweza kupitisha chakula vizuri, wengine waliniambia nina kansa ya koo.

Lakini nakumbuka wakati wa kipindi cha harusi ya AliKiba nilikutana na Gavana, Joho wa Mombasa akanisaidia kunikutanisha na madaktari wengine nchini Kenya.

Vipimo vya nchini Kenya vilionyesha kwamba ugonjwa wangu ulisababishwa na kunywa kitu chenye sumu, na wakasema ukubwa wa tatizo nililokuwa nalo inabidi niende kutibiwa nje".

Amplifaya
Millard Ayo




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuu sibora wangemtoa shipa, kuliko kumuua sauti yake yakuimba kwakulitia vyupa koo lake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa maada bila shaka ni mzalamo wazalomo akili zenu mnazijua wenyewe.kupigwa juju nini fafanua najua utasema kuroga kuroga nini?maradhi yapo na yapo kwa ajili yetu moja ya vitu vya kijinga ambavyo hutakiwi kuchochea kamwe ni mambo ya ushirikina.omi dimpoz hajarogwa ni maradhi tu yamemukuta kama ambavyo yangenikuta mimi na wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…