Ommy Dimpozi: Sitaki kufa maskini kama Ngwair

Ommy Dimpozi: Sitaki kufa maskini kama Ngwair

wajojo

Senior Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
155
Reaction score
83
Mwanamuzik chipukizi Ommy Dimpozi,ameonyesha kuwa na kiwango cha juu sana cha dharau kwa kumdhihaki na kumtusi mtu aliyetangulia mbele ya haki."SITAKI NIKIFA YATOKEE KAMA YA NGWAIR,AMEKUFA AFRIKA KUSINI,HATA KUUSAFIRISHA MWILI KUULETA TANZANIA IMEBIDI MPAKA WATU WACHANGIE,ILE NI AIBU SANA",alisema Ommy kwa dharau.

Vile vile Ommy baada ya kushinda tuzo ya video bora ya mwaka Ommy alibwabwaja:"jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa",kama vile haitoshi Ommy alizidi kusisitiza kuwa HATAKI KUFA MASKINI KAMA NGWAIR,je hii kauli ni nzuri kwa mtu aliyetangulia mbele ya haki???,

=================
Habari kamili
=================

Akimweleza mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, Juni 10 (Jumatatu) na Juni 11, mwaka huu (Jumanne), Ommy alidhihaki hata ushiriki wa wanamuziki waliosimamisha shughuli zao kwa muda kisha kuungana na kushikamana kuhakikisha Ngwair anazikwa kwa heshima.
"Sitaki nikifa yatokee kama ya Ngwair, amekufa Afrika Kusini, hata kuusafirisha mwili kuuleta Tanzania imebidi mpaka watu wachangie, ile ni aibu sana," alisema Ommy kwa dharau.

JUMANNE (JUNI 11)
Kutokana na uzito wa maneno ambayo Ommy aliyatamka kuhusu Ngwair, siku iliyofuata (Jumanne), mwandishi wetu alimpigia simu kumuuliza kama maelezo hayo ya kashfa aliyatoa akiwa amelewa au la?
Ommy kwa kujiamini, alijibu kwamba alichokisema kuhusu Ngwair ni ukweli kwa asilimia 100.
MWANDISHI: Nakushauri kama mdogo wangu, siku nyingine usirudie kutamka maneno hayo ni mabaya sana kwa mtu aliyekufa.
OMMY: Sijaongea neno baya, nimesema ukweli wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Wewe unaona mtu akichangiwa baada ya kufa ndiyo kipimo cha umaskini?
OMMY: Kuna mambo mengi ambayo yangefanyika kabla ya kuchangiwa lakini Ngwair alishindwa kuyafanya.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angefanya nini wakati yeye ameshakufa?
OMMY: Kuna mambo yangefanyika, mfano kusafirisha mwili kutoka Afrika Kusini.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angejisafirisha mwenyewe?
OMMY: Nachosema mimi ni kwamba wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Sikiliza Ommy, hata mabilionea wakubwa huwa wanachangiwa. Mtu kuchangiwa siyo kashfa wala aibu kama unavyotaka kulionesha tukio la Ngwair. Marehemu Steven Kanumba alikuwa anatembelea Toyota Lexus V8, mbona alipokufa kila kitu alifanyiwa? Ni jambo la kawaida.
OMMY: Ngwair alikuwa na ‘stresi' za maisha ndiyo maana alikuwa anakula unga.
MWANDISHI: Ulishawahi kumwona Ngwair akitumia unga?
OMMY: Kwanza nakusikia unanirekodi, sijui una malengo gani.

MANENO YA KASHFA MLIMANI CITY

Juni 8, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) mwaka 2012-2013, Ommy Dimpoz alizungumza maneno ya kashfa ambayo moja kwa moja yalitafsiriwa ni dongo kwa Ngwair.
Baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha Video Bora ya Mwaka na kukabidhiwa tuzo yake, Ommy alibwabwaja: "Jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa."
Japo hakutaja jina la yule aliyekuwa anamzungumzia, tafsiri ya wengi ni kwamba Ommy alikuwa anamzungumzia Ngwair kwa sababu ndiye staa aliyekuwa amezikwa kishindo cha siku moja tu kabla ya usiku huo wa tuzo. Ngwair alizikwa Alhamisi, tuzo Jumamosi.
"Huyu dogo ana nyodo sana, sasa haya ni maneno gani ya kuzungumza? Hapa anamzungumzia Ngwair, ila anapaswa kujua kwamba yeye bado msanii mdogo sana kumlinganisha na Ngwair," alisema mtangazaji mmoja kwa masikitiko.

MAPOZI NI KAWAIDA YAKE, ATIMULIWA KIGOMA ALL STARS

Ndani ya Kampuni ya Kigoma All Stars, awali Ommy alikuwa mmoja wa wajumbe kwenye bodi ya wakurugenzi lakini hivi karibuni alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Msechu.
Chanzo chetu makini ndani ya Kigoma All Stars, kimetonya kuwa Ommy alionesha tabia mbaya dhidi ya wasanii wenzake wanaounda kampuni hiyo, hivyo hakukuwa na jinsi zaidi ya kumtimua ujumbe wa bodi na kumuweka Msechu.
"Alikuwa ameshakuwa kero. Unajua pale Kigoma All Stars wote ni mastaa lakini yeye anajiona yupo juu ya wote. Tunaitisha vikao hatokei, tunakwenda kufanya shoo hatokei, tunamuona hana umoja na sisi na hatufai.
"Uamuzi wa kwanza ulikuwa ni kumtimua kabisa ili asiwepo kabisa kwenye kampuni yetu, maana siyo lazima kila mtu mwenye asili ya Kigoma awepo Kigoma All Stars. Baadaye kwa busara za mlezi wa kampuni yetu, Zitto Kabwe ndiyo tukamuondoa kwenye bodi.
"Tumembakiza kwenye kampuni kama mwanahisa wa kawaida tukiwa tunampima. Akiendelea kuleta mapozi yake, hatutamvumilia, tutamfukuza moja kwa moja," kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kiliongeza, ndani ya Kigoma All Stars kuna wasanii wakubwa kama Nasibu Abdul ‘Diamond', Ali Kiba, Mwasiti Almasi, Sunday Mangu ‘Linex', Banana Zorro na wengineo lakini hawaringi, isipokuwa Ommy ndiye fungakazi kwa maringo.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), vilevile Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipoulizwa kuhusu Ommy kutimuliwa kwenye bodi, alikiri hilo kufanyika.
"Ni kweli kuna mabadiliko kwenye bodi, wanamuziki wenyewe kwa sababu ndiyo wanahisa, waliamua kumuondoa Ommy Dimpoz na nafasi yake akawekwa Peter Msechu," alisema Zitto.
Kuhusu kutimuliwa kwenye bodi Kigoma All Stars, Ommy hakutaka kuzungumza chochote, badala yake alijikanyagakanyaga.

OMMY NA NYIMBO TATU

Ommy anajiita super handsome, mapozi, kampuni yake anaiitwa Pozi Kwa Pozi, majina hayo yanatosha kueleza sababu kwa nini amemdhihaki Ngwair na haelewani na wasanii wenzake.
Ndiyo kwanza ana nyimbo tatu tu, Nai Nai (alisaidiwa sana na Ali Kiba), Baadaye na Me & You (amesaidiwa sana na Vanessa Mdee) lakini amekuwa wa migogoro na mbwembwe nyingi dhidi ya wasanii wenzake.
Alishawahi kurushiana maneno kwenye vyombo vya habari na mwanamuziki Cyril Kamikaze, baadaye akaingia kwenye gogoro zito na mwana Hip Hop wa Nako 2 Nako Soldier, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez'.
Kuhusu Lord Eyez ambaye ni memba wa Familia ya Weusi, alidai alimuibia taa, power windows, vioo na vifaa vingine vya gari lake lakini kesi ilipofika mahakamani, Ommy hakwenda kutoa ushahidi.
Ommy alishindwa kutoa ushahidi lakini kabla yake alitangaza katika vyombo vya habari kuwa Lord Eyez ni mwizi na kwamba alimwibia vifaa vya gari lake, zaidi ya hapo alikusanya watu wakampa kipigo memba huyo wa Weusi kisha wakampeleka polisi ambako aliwekwa lupango.


Habari kwa HISANI YA Global Publishers Tanzania Limited
 
Who cares acha abwabwaje .. anayesaka maisha mazuri habwabwaji hovyo
 
Mwanamuzik chipukizi ommy dimpozi,ameonyesha kuwa na kiwango cha juu sana cha dharau kwa kumdhihaki na kumtusi mtu aliyetangulia mbele ya haki."SITAKI NIKIFA YATOKEE KAMA YA NGWAIR,AMEKUFA AFRIKA KUSINI,HATA KUUSAFIRISHA MWILI KUULETA TANZANIA IMEBIDI MPAKA WATU WACHANGIE,ILE NI AIBU SANA",alisema ommy kwa dharau.Vile vile ommy baada ya kushinda tuzo ya video bora ya mwaka ommy alibwabwaja:"jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa",kama vile haitoshi ommy alizidi kusisitiza kuwa HATAKI KUFA MASKINI KAMA NGWAIR,je hii kauli ni nzuri kwa mtu aliyetangulia mbele ya haki???,

That is from him..alichokosea ni kumtaja mtu! ajitahidi sana, wasanii wa bongo ni maarifa wamekosa! hata yeye anaweza kufa maskini tu! wenye juhudi hawadhiaki hata siku moja..Ajipime vizuri!!
 
SIRI tunasema BAYANA tunaficha. Ukweli usimame kwenye ukweli na unafiki ukae pembeni. Kufa masikini ilihali wewe no super star mi AIBU
 
Kuna ukweli ila kakosea namna ya kuongea
 
Yeye aendelee tu kukata mauno.
 
ivi kuna mtu apa duniani anapenda kufa maskini au kufa kifo cha aibu ...??? ok tunamtakia kila la kheri katika safari yake ya kufa tajiri na kifo cha kishujaa...Rip ngwea
 
Huyu mtoto anajisikia mnooo...yani majivuno tu amejaaliwa...n wat if angekuwa na deal km Diamond..show kila kukicha...contract na makampuni...si tungetukanwa kabisa.??? Lets say akifa leo..huo utajiri anao..au ana ahadi na Mungu kuwa atakufa akishamiliki gorofa kadhaa posta na kkoo...shule hamna ni ulimbukeni...maskini akipata m...ta...ko hulia mbwata...
 
kwahiyo wanafanyaje kama wanadhulumiwa??? :yell::nod:
SIRI tunasema BAYANA tunaficha. Ukweli usimame kwenye ukweli na unafiki ukae pembeni. Kufa masikini ilihali wewe no super star mi AIBU
 
Same times wasanii wetu wanakufa maskini kutokana na kupenda sana starehe! Sasa kama Ng'wea angekuwa havuti hayo masembe si angekuwa tajiri kidogo...
 
Hivi kimeimba wimbo gani hicho kitoto? atakuwa alizaliwa kwa kutanguliza migu huyo, hana nidhamu hata kwa mama yake, mjinga sana huyo dogo...
 
Tatizo la wabongo hatujazoea kuambiana ukweli......Tumekalia unafki na kuogopana.
Nakuuliza mheshimiwa wajojo Ngwea amekufa TAJIRI au MASIKINI..????
 
Last edited by a moderator:
Mwanamuzik chipukizi ommy dimpozi,ameonyesha kuwa nakiwango cha juu sana cha dharau kwa kumdhihaki na kumtusi mtu aliyetangulia mbele ya haki."SITAKI NIKIFA YATOKEE KAMA YA NGWAIR,AMEKUFA AFRIKA KUSINI,HATA KUUSAFIRISHA MWILI KUULETA TANZANIA IMEBIDI MPAKA WATU WACHANGIE,ILE NI AIBU SANA",alisema ommy kwa dharau.Vile vile ommy baada ya kushinda tuzo ya video bora ya mwaka ommy alibwabwaja:"jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa",kama vile haitoshi ommy alizidi kusisitiza kuwa HATAKI KUFA MASKINI KAMA NGWAIR,je hii kauli ni nzuri kwa mtu aliyetangulia mbele ya haki???, Kiukweli ommy umekosea sana kusema hvo mtoaji wa riziki ni mungu
 
True wamezd kuendekeza mitung mikas bangi,ona mwenzie mr nice alivyokuwa and now alipo, hv wakitkanwa baada ya kuaga dunia mtalalamika? Acheni utoto
 
Hapa mi niona ni kuto kuelewana kwa kauli aliyotoa..ujumbe wake kama mlimsikilza vizur alikuwa na maana nzuri sana ila kilichotokea ameshindwa kuuwakilisha kwa audience na ndio mana umepokelewa tofauti ila sio eti alitoa maneno kwa kejeli.. Na ndio maana alibase kuyahamasisha makampuni yajitahidi kuwatumia wao na sio wasanii wa nje ili nao waweze kujikwamua kimaisha zaid ya walipo na km mnakumbuka alitumia mfano wa mesi kuwekwa picha nyuma ya then dimpoz anatumbuiza.
 
Back
Top Bottom