py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,476
- 4,448
Wana simba nawatahadharisha na fitna anayotaka kuileta mwalimu Omog kutaka kuigawa dressing room tufahamu dressing room kuigawa ni kuiharibu timu na kujitafutia matatizo.Tujikumbushe Mourinho alivyokuwa Madrid aliigawa dressing room na kila mmoja ni shahidi kile kilichomtokea pia Benitez alivyopoteza ushawishi kwenye dressing room aliangukia pua.
Omog ni mwalimu wa zamani wa Azam fc na msimu huu kawasajili wachezaji takriban 4 aliowafundisha Azam ambao ni Bocco,Nyoni,Manula na shomari hilo halina tatizo kama aliwapendekeza na wapo kwenye mipango yake ila tatizo linakuja pale anapoleta upendeleo na kutaka kugawa wachezaji.Tunafahamu Omog unampenda sana Bocco sababu ulimfundisha Azam lakini kumpa unahodha hilo hatuliafiki.
Mchezaji kasajiliwa tena mgeni kisha anapewa unahodha hivi wachezaji waliotumikia muda mrefu watajisikiaje tatizo sio mkude kuvuliwa unahodha bali kumkabidhi mgeni unahodha hapa Omog analeta ubesti tu
Yaani leo hii morata apewe ukapteni mbele ya akina Cahill ,willian ? Au salah apewe ukapteni mbele ya akina Henderson ,coutinho .
Na lau ingekuwa amri yake basi Nyoni pia angepewa unahodha mkuu ila moyo unamsuta
Mchezaji mgeni haijui camp vizuri ,yeye ndiye anayehitaji msaada ila ndiye anapewa jukumu la kuongoza ni wazi hii ni hatari kwa wana msimbazi huenda ikaleta mpasuko ndani ya klabu na mgogoro na kupelekea timu kupata matokeo mabovu.