Elections 2010 On TBC1: Augustine Mrema vs John Mrema vs Meira (jimbo la Vunjo)

Elections 2010 On TBC1: Augustine Mrema vs John Mrema vs Meira (jimbo la Vunjo)

Swali la Kwanza:

John:
Elimu - Wathibitishe ni vipi Elimu itaboreshwa
Kivipi kutakuwa na ongezeko la walimu na ubora
Umasikini - watatuhakikishiaje kuwa watatunyanyua?
 
CCM:
Shule za Msingi - Waalimu, Vifaa na Madawati na kukosa ada.
Walimu ni tatizo. hakuna nyumba za kupanga. Tutaanzisha mfuko wa Elimu, utatatua matatizo. Tutahamasisha wadau ili waalimu wakae bure.
Kuwe na ushindani katika Elimu kwa kuweka motisha
mashindano ya shule na shule
Vifaa - Kila shule kuwa na maktaba. Wafadhili wapo
Umasikini - VIKOBA, SACCOS - Kina mwanamama na vijana kila kikundi kiwe na miradi na wapate wafadhili na mafunzo
 
Mrema TLP:
Budget: Kuhakikisha pesa hailiwi . Bunge litenge 20%
Kuelekeza pesa ziende kwenye Elimu
Shule zifanyiwe ukarabati na Madawati yapatikane. Yeye aliwahi kukopesha waalimu baiskeli
Safari hii atawakopesha pikipiki
Kila kata iwe na sekondari
Waalimu wa sayansi - atashughulikia anafahamiana na watu nchi nzima
Maabara ya sayansi zitapatikana
Umasikini - atasimamia zao la kahawa na kupata zao mbadala
Kuanzisha vikundi vya uzalishaji kwa ajili ya mikopo
 
Mrema CHADEMA:

Mshahara 20% - nitagharamia wanafunzi wanaaofaulu. Kuwashindanisha katika mfuko huu wa Mbunge
Waalimu - Tutakaa na waalimu tupate ufumbuzi
Nyumba za Waalimu - Kukaa na Wadau ili kuapta ufumbuzi
Motisha kwa waaliimu watakaofaulisha wanafunzi
Umasikini - Kilimo. Asimia 70% ni wakulima. Pembejeo hazifiki. hakuna usimamizi. Atasimamia hilo.
Utalii - Upatikanaji wa ajira na ujira unaostahili
Maji - Fedha zipo. Billion 15.2 zimetolewa na wajerumani. Pia WB wametoa ila haijulikani pesa zinaenda wapi.
 
Swali la Elimu bado sijaona jibu la kueleweka, wote naona wanazunguka tu. Kwamba unafahamiana na watu nchi ndio utapata walimu? Walimu siyo mikopo ya pikipiki au baiskeli.

Serikali ipi ambayo itakubali kutenga 20% ya bajeti ielekezwe kwenye elimu?

Kuanzisha mfuko wa elimu pekee hauwezi kuwa utatuzi, bali eleza na jinsi mfuko huo utakavyotumika ili watu wajue and who will be financing huo mfuko wa elimu.
 
Du! Wakuu nina dharura kidogo . . .

naomba mdau yeyote aliye kwenye TV anisaidie. Please . . .
 
Superman,

Siko kwenye TV ndugu yangu, mimi nilikuwa ninafuatilia maelezo yako. Nashukuru kwamba dharura imetokea zikiwa zimebaki dakika chache, natumaini hiki ni kipindi cha lisaa limoja.
 
Conclusion:

Wagombea ni wazuri... wananchi wa Vunjo wamejaliwa kwa hili.
 
Mrema: "Nipeni mimi vijana wanakwenda kufanya majaribio" haha a ahahaha, jamaa hana point kabisa
 
wote ni wazuri lakina mrema wa chadema anajua kujieleza na ana points nzuri.

Mgombea wa CCM ni mzuri zaidi... kwa sababu pia anatakiwa awe kwenye defensive mode... wakati wengine sio lazima... and yet anashamiri.... Hata hivyo nadhani yeyote atakayepiat... jamaa watakuwa wamelamba dume.
 
Hakuna kitu kwa mgombea wa CCM, kelele tu hana kitu kipya sera zao ndiyo hizo hizo kila mwaka utekelezaji sufuri kabisa, MGOMBEA ANAYEFAA VUNJO NI WA CHADEMA.
 
Hakuna kitu kwa mgombea wa CCM, kelele tu hana kitu kipya sera zao ndiyo hizo hizo kila mwaka utekelezaji sufuri kabisa, MGOMBEA ANAYEFAA VUNJO NI WA CHADEMA.

KWELI BWANA :mad2: MGOMBEA WA CHADEMA ATAFUFUA KNCU.... VERY INTERESTING.
 
John Mrema ni member wa JF nadhani akipata muda atatupa kwa undani wake yanayoendelea, nasikia Augustino Mrema alisimama bila kuruhusiwa akakalishwa?
 
Mzee wetu mrema kwa kweli mmmhhhhhhhhhhhh, HATA MKE WAKE ANAJUA YUPO FIT, AHAHA AHAHAH
 
John Mrema ni member wa JF nadhani akipata muda atatupa kwa undani wake yanayoendelea

Akija naomba ani-PM kuna vitu ninataka kumshauri ili kuboresha vipaumbele vyake. Lakini afanye hivyo kama ana nia ya kupata ushauri na mawazo ya watu wengine.
 
Akija naomba ani-PM kuna vitu ninataka kumshauri ili kuboresha vipaumbele vyake. Lakini afanye hivyo kama ana nia ya kupata ushauri na mawazo ya watu wengine.
Nimemtumia PM mkuu, naamini akiingia atawasiliana nawe haraka tu
 
Back
Top Bottom