Nilifuatilia kwa umakini mkubwa mdahalo wa wagombea ubunge jimbo la Vunjo, uliorushwa na TBC juzi. Kwanza nilishtuka niliposikia Kijana John Mrema anasema kuwa ana umri wa miaka 30. Alionekana mchanga sana akilinganishwa na wapinzani wake pale; Lyatonga wa TLP na Meela wa CCM.
Hata hivyo baada tu ya kupewa kipaza kila mgombea aanze kwa dk 5 za kujieleza kwa ufupi, nilisisimka jinsi John Mrema alivyojieleza kwa umahiri mkubwa, akitoa takwimu mbalimbali na kuzihusisha na mipango yake. Kwa kweli kwa mtu yeyote aliwasikiliza na kama yuko fair, atakubali kuwa yule kijana aliwaacha kwa mbali sana wapinzani wake kwa uwezo wa kujieleza na mipango makini. Hali iliendelea kuwa hivyo hata pale walioanza kuulizwa maswali kwani John Mrema alijibu kwa ufupi, lakini kwa umahiri mkubwa. Sijui upepo uko vipi huko lakini kama yule kijana akienda bungeni..., Dah CHADEMA watatisha.