NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
1.Ukifanya harusi bila kuchangisha mtu kosa rafiki zako watakasirika na wengine hawatakuja hata kama umeamua kugharamia mwenyewe kila kitu.
2.Watu wanachanga harusi budget kubwa inakuwa kwenye pombe kuliko chakula wengine wanasema kama ni chakula atanipikia mke wangu mimi nataka pombe ambapo mke wangu hawezi kutengeneza bia.Halafu mafanikio ya harusi ni kama watu walikunywa sana.
3.Harusi ikiisha baada ya kutumia hela nyingi mamilioni baada ya siku chache kuna kitu wanaita kuvunja kamati au uchakavu.Wanatumia tena nusu ya gharama za harusi iliyopita kwa kunywa na chakula huku bwana na bibi harusi wakwenda kuishi maisha ya ukiwa ambapo hizo gharama za uchakavu ingekuwa ni zawadi za kuwasaidia maharusi kuanza maisha mapya.
4.Unakuta mtu ana eneo kubwa sana anaweza fanyia harusi kwake lakini anakwenda kukodisha ukumbi kwa mamilioni ya wachangiaji
5.Bwana harusi mwenyewe anataka harusi ya kifahari ambapo iko chini ya uwezo wake.Hivyo anakopa mamilioni na hata gari kumkonga bibi harusi.Baada ya harusi anakuwa na madeni ya kutisha matokeo yake maisha yanakuwa magumu mahusiano yake na bi harusi wake yanakuwa mabaya ndoa baada ya miezi mitatu inavunjika.
6.Binti akitaka kuolewa baadhi ya mila wanamgeuza fursa kutajirika wanadai mahari kubwa sana au mifugo na wakati wa kupanga mahari watu wanaweza bishana kuanzia saa mbili asubuhi hadi 12 jioni.Matokeo yake binti aliyeolewa anaishi kwa manyanyaso makubwa mno kwenye ndoa yake maana mume amemlipia gharama kubwa.
7.Kuchangisha harusi.Kwani ni lazima uchangishe? Ukiona huwezi fanya harusi wewe na familia yako basi ujue huna uwezo wa kutunza mke.Harusi ni muhimu kwanini usumbue wengine.Fanya kwa uwezo wako tafuta wageni waalikwa labda ndugu zako wakaribu tu waandalie chakula tafuta sheikh au mchungaji au padre fungisheni ndoa yenu.Kwa maoni yangu ndoa simple huwa zinadumu kuliko ndoa za magharama makubwa.Nimeshawahi shuhudia harusi miaka ya 1990 iligharimu milioni60 ya watoto wa vigogo hadi barabara mbili zilifungwa.Bia zilikuja kwa Meli enzi hizo bia zilikuwa zinaitwa Steller Artois.Ile ndoa ilidumu kwa miezi mitatu ikavunjika.Kigogo huyo wa baba wa bibi Harusi matajiri wenzake na watu wenye cheo kikubwa walimchangia mamilioni.Nchi ya Ghana hakuna kitu kinaitwa kuchangia harusi unawaalika watu kwa uwezo wako ila siku ya harusi wanakuja na zawadi ambapo ni kubwa kuliko kama ungechangiwa watu wakala na kunywa pombe.Nishaona harusi moja Ghana mtu alitoa zawadi ya harusi gari.hata nchi jirani Kenya wametuzidi kwa hili.
8.Vijijini hakuna wapishi au tuite buffe hivyo wanapikia nyumbani.Unakuta umekaa mtu amekujazia sahani nakukuletea kwanini msiache iwe self service unampimia mwenyewe.Hii inapunguza matukio ya watu kuwekeana sumu na madawa ya kulevya.
9.Mtu akikuchangia baadhi sio wote akili yake yote haoni ni ili akusaidie au akupige tough huo mchango anaupigia hesabu atavyo kula na kunywa.Akiona idadi ya chupa hakupata inavyostahili analalamika hakutendewa haki.
Huyo jamaa hapo pichani ni mtu na heshima zake.Kamchangia harusi rafiki yake binti yake anaolewa kwa jinsi hiyo basi.Angetakiwa awe ni moja ya msaada kuhakikisha harusi ya mwenzake inaenda vizuri matokeo yake anakunywa kufidia mchango wake akawa mzigo kwa harusi nzima na mkewe.Wenye harusi wakaingia gharama ingine kumtafutia usafiri
Naomba kutoa hoja najua sitakosa mapovu ila nimetoa yangu ya moyoni
Ila tunahitaji kubadilika kwa kweli.