Ona hawa mafisadi wa bara la Afrika wanavyojimwambafai

howardlite

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2016
Posts
242
Reaction score
392
Kwenye mada,

Kuna wakati unawaza kuhusu kwanini Afrika?Unaelewa ni agenda ya mezani ya kila siku ya nchi zilizoendelea.
Kama tunavyofikiri namna ya kuendesha familia zetu vizuri kwa ustawi ndivyo mataifa ya magharibi yanavyofikiri ni nini cha kuchukua Afrika kwa kodi zao za meza.

Kuna wakati njia zinazotumika unajiuliza nani yuko tayari kufa kwa haraka kwaajili ya taifa lake la Afrika.
Kuna wakati tunabaki tunalaumu sana viongozi wetu kuhusu ufisadi,rushwa kuweka rehani rasilimali za mataifa yao kwa namna kama hii wangapi wako tayari kuinua kidole juu kuwapinga hawa mafisadi wa bara la Afrika kwa mbinu wanazozitumia ukizingatia wako mbele kiuchumi,kiteknolojia na kihuni tutasalimika?

Tujiulize kuwa wakala wao(puppet) kunaepukika?Wangapi wamekufa kwa vifo ambavyo ni matokeo ya kwenda kinyume na sera na falsafa zao?

Tufanye nini kwa mazingira ya aina hii kwa yanayoingizwa polepole Africka,mahususi nchi yetu?
Kuna dhamira yoyote ya nchi zetu kusini mwa jangwa la Sahara na Afrika kujilinda na uharibifu huu kama wakina Mzee Nyerere,Nkruma na wengine walipata upinzani mkubwa kutoka kwa ndugu zao wa Afrika?

Afrika haiwezi kuendelea kama tutandelea kuwabebesha lawama watu wasiohusika(mabeberu) kwa madhaifu yetu,badala ya kuweka mipango mizuri ya maendeleo na kuisimamia.
 
Ufisadi,Rushwa na wizi wa mali za uma kutoka kona ya Tanzania
 
Afrika haiwezi kuendelea kama tutandelea kuwabebesha lawama watu wasiohusika(mabeberu) kwa madhaifu yetu,badala ya kuweka mipango mizuri ya maendeleo na kuisimamia.
Kutohusika wenyewe wanasema uhusika wao kwa uwazi kabisa na namna ambavyo hawawezi kuacha,kuacha kwao kuifisadi Afrika ndio kuanguka kwa mataifa yao.
Point ni nini cha kufanya na uwezekano wa kukifanya.
 
Kuna dhamira yoyote ya nchi zetu kusini mwa jangwa la Sahara na Afrika kujilinda na uharibifu huu kama wakina Mzee Nyerere,Nkruma na wengine walipata upinzani mkubwa kutoka kwa ndugu zao wa Afrika?
Usitishike mkuu, hatutatawaliwa tena kwa njia yoyote ile.

Hawa 'puppet' wanaojitokeza mara hii hawafiki mbali, watadhibitiwa tu.

Mfumo mzima wa hao mabeberu umekwishastukiwa. Unaona duniani kote wanavyohaha, lakini hawafurukuti tena.

Sana sana wamebaki na vifaa vyao hivi vya Banki ya dunia na IMF kueneza sumu zao, lakini hata hivyo vyombo vitakomeshwa tu.

Hawa 'puppet' waliopo hapa ni kuendelea kuwakabili tu, wasipewe nafasi.
 
Afrika haiwezi kuendelea kama tutandelea kuwabebesha lawama watu wasiohusika(mabeberu) kwa madhaifu yetu,badala ya kuweka mipango mizuri ya maendeleo na kuisimamia.
Huenda nitaonekana kujipinga kwa kukubaliana na wewe katika sehemu moja ya hoja yako ya "kujilaumu wenyewe kwa madhaifu yetu", na wakati huo huo nikipinga kabisa hilo la "lawama wasiohusika."

Kama wewe huoni nguvu nyingi wanazotumia hao unaosema hawahusiki, hapo ndipo kosa lako linapoanzia.

Hawa 'puppets' wanaolazimisha kuwepo madarakani unadhani wapo kwa manufaa ya nani kama siyo hao unaosema wasilaumiwe?
 
Kwenye mada,

Kuna wakati unawaza kuhusu kwanini Afrika?Unaelewa ni agenda ya mezani ya kila siku ya nchi zilizoendelea.
Kama tunavyofikiri namna ya kuendesha familia zetu vizuri kwa ustawi ndivyo mataifa ya magharibi yanavyofikiri ni nini cha kuchukua Afrika kwa kodi zao za meza.

Kuna wakati njia zinazotumika unajiuliza nani yuko tayari kufa kwa haraka kwaajili ya taifa lake la Afrika.
Kuna wakati tunabaki tunalaumu sana viongozi wetu kuhusu ufisadi,rushwa kuweka rehani rasilimali za mataifa yao kwa namna kama hii wangapi wako tayari kuinua kidole juu kuwapinga hawa mafisadi wa bara la Afrika kwa mbinu wanazozitumia ukizingatia wako mbele kiuchumi,kiteknolojia na kihuni tutasalimika?

Tujiulize kuwa wakala wao(puppet) kunaepukika?Wangapi wamekufa kwa vifo ambavyo ni matokeo ya kwenda kinyume na sera na falsafa zao?

Tufanye nini kwa mazingira ya aina hii kwa yanayoingizwa polepole Africka,mahususi nchi yetu?
Kuna dhamira yoyote ya nchi zetu kusini mwa jangwa la Sahara na Afrika kujilinda na uharibifu huu kama wakina Mzee Nyerere,Nkruma na wengine walipata upinzani mkubwa kutoka kwa ndugu zao wa Afrika?

Aisee!!!
 
Back
Top Bottom