eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Magari mawili kuharibika ni coincidence tu ila tu watu ni wepesi kutafsiri
Yakiwa 20 kama ya Mwakiyeyeu!!??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Magari mawili kuharibika ni coincidence tu ila tu watu ni wepesi kutafsiri
Babaangu ametengeneza Barabara eneo lile gari lao liligoma kuwaka eneo lile... Ndiye aliye nisimulia hadithi za pale... Anafahamu majina ya walio lala pale na miaka yao ya kufa akiwemo Martin kiyeyeu 1935Duh!!!,ilikuwa mwaka gani?,Wewe ulikuwepo au ulisimuliwa?.
Watu wameendelea kuwa na nguvu zao hata wanapokufa.
Kaburi la Morris Kiyeyeu liligoma kuvunjwa kwa zaidi ya miaka arobaini ili kufisha miradi ya umeme na barabara ya Tanzam.
Mifano iko mingi Sana, ila hapa Kuna video inayoonyesha nduguye MK254 akigoma kupelekwa kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.
Yakiwa 20 kama ya Mwakiyeyeu!!??
Mkuu Bujibuji hiyo story ya Kiyeyeu inapotoshwa kwa makusudi na si kweli kwamba kaburi liligoma kuvunjwa kupisha mradi wa umeme. Ukweli ni huu;
Utekelezaji huo wa mradi wa umeme ulienda sambamba na ulipaji fidia kwa wote ambao wangeathirika kwa namna moja au nyingine vikiwemo nyumba, mashamba na kadhalika.
Nguzo za umeme zilipofika hapo (maeneo ya Tanangozi) watekelezaji wa huo mradi wakagundua kuna makaburi ya familia (siyo moja) ya Kiyeyeu ambayo hayakuwekwa kwenye ulipaji wa fidia. Ili kukwepa kuwalipa fidia familia ya Kiyeyeu wakaamua kupitisha nguzo za umeme upande wa pili wa barabara halafu kuzirudisha kwenye njia ya kawaida mara tu baada ya kuyapita makaburi hayo.
Ndiyo maana mara tu kabla ya yale makaburi nguzo ilikuwa inavuka barabara na mara tu baada ya makaburi zinarudi upande ule ule.
Hebu nipe hiyo mkuuBujibuji unamfahamu O.M.K Muhehe wa Tabata? Aliwahi fanya kazi kiwanda Cha cement Cha Rhino?
je wanataka kutuambia kuwa yale matambiko yaliyokuwa yanafanyika ilikuwa ni kiini macho? maana kwa wale wasafili nafikiri walikuwa wakiona wenyewe kiti na ngozi viliwekwa pale juu ya kaburi pamoja na pombe aina ya comoni kama ishala ya kumbembeleza akubali kuhamaMdondoaji said:
Tumain Msowoya, Iringa
HATIMAYE kaburi la kihistoria la Martine Kiyeyeu lililokuwa katika eneo la Isimila, kijiji cha Ugwachanya limeondolewa katika hifadhi ya barabara ya Tanzania-Zambia, Mkoani Iringa kwa ajili ya kupisha upanuzi wa barabara hiyo.
Kaburi hilo ambalo lilikuwa pembezoni mwa barabara hiyo, limeondolewa katika oparesheni iliyoendeshwa na Wakala wa barabara (Tanroads) kwa akiwashirikisha wananchi wa kijiji hicho.
Kaburi la Kiyeyeu linalokadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 40 hadi 50, lina historia ndefu kutokana majaribio ya kuliondoa mara kadhaa kushindikana.
Moja ya maajabu ya kaburi hilo ni kushindwa kupitishwa kwa umeme kupita juu ya yake na pia linadaiwa kushindikana kuondolewa mara mbili na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga alipokuwa akijaribu kuling'oa.
Lakini jana kaburi hilo na mengine 21 yaliyokuwa kwenye eneo hilo yaliondolewa na kuhamishiwa upande wa pili wa barabara, ambako kulikuwa na kaburi moja la mtoto wa kike wa Kiyeyeu, ambaye hakuzikwa katika eneo lililokuwa na makaburi ya ndugu zake.
Wakizungumza na Mwananchi, baadhi ya watu walioshiriki katika zoezi la kuondoa kaburi hilo walisema kazi haikuwa ngumu kama walivyodhani.
"Tumeondoa ‘kiulaini', hakuna mila wala desturi iliyofanywa kabla ya kuliondoa, na ndugu wa Kiyeyeu wanasema watakuja kazi ikimalizika kwa ajili ya kumaliza mila zao," alisema Gaitan Utenga.
Alisema kazi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano walioupata kutoka Tanroads ambao waligharamia shughuli nzima ya kuondoa kaburi hilo ilyowashirikisha vijana zaidi ya 30.
"Tumelipwa pesa yetu vizuri, wamenunua sanda na masanduku kwa ajili ya mazishi na hatimaye kaburi limeondolewa tofauti na imani iliyokuwa imezagaa miongoni mwa wengi kwamba ingeshindikana," alisema.
Mwenyekiti wa kamati ya kuondoa kaburi hilo ambaye ni mmoja wa wanafamilia wa Kiyeyeu, Pulo Kikoti alisema hakuna tatizo lililotokea wakati wa kuondoa kaburi hilo. Kazi hiyo alizanza jana saa nne asubuhi na kumalizika majira ya jioni.
Alisema ugumu ulikuwa katika kulibomoa kutokana na aina ya ujenzi wake, lakini baada ya kubomolewa kazi ya kulihamishia upande wa pili wa barabara haikuwa ngumu.
Hata hivyo walisema tayari makaburi yote 22 yaliyokuwa katika eneo hilo yameondolewa na kwamba kazi ya kuzika mafuvu ya marehemu ambao wote ni familia ya Kiyeyeu inatarajiwa kumalizika leo mchana.
"Ndugu wanasema mwishoni baada ya mazishi kukamilika na makaburi mapya kujengwa, watakuja kufanya mila zao, lakini mpaka sasa tumemaliza shughuli nzima ya kuondoa kwa kaburi hilo ambalo lilikuwa gumzo kwa miaka mingi," alisema.
Mzee huyo alisema wengi waliamini kuwa eneo hilo lilikuwa la maajabu, kutokana na ukweli kwamba lilishawahi kujaribiwa kuondolewa zaidi ya mara mbili na ikashindikana.
"Kulikuwa na imani nyingi hapa, lakini tulijitosa kuhamisha na kweli hakuna kilichotokea hapa, naweza kusema imani hizi hazikuwa za kweli, mbona tumefanikiwa?" alihoji Kikoti.
Kuondolewa kwa kaburi la Kiyeyeu kumekuwa gumzo kwa watu wengi wakiwemo abiria wanaopita katika barabara hiyo ambapo kila mmoja amekuwa akishangaa jinsi kazi hiyo ilivyofanyika.
Awali mkazi wa Mafinga, Sadick Mhomanzi alijitokeza akidai kuwa anaweza kuliondoa kaburi hilo la Kiyeyeu na kwamba hakuna madhara yoyote ambayo yangeweza kumpata.
Hata hivyo mapema jana, Mhandisi aliyeshiriki operesheni ya kupitisha umeme kwenye kaburi hilo mwaka 2006, Eliasante Mwakalinga, alionya kuwa Sadick asithubutu kwani angeweza kupatwa na balaa.
Akizungumza na gazeti hili kutoka mkoani Mtwara jana, Mwakalinga ambaye sasa ni mwalimu wa Chuo Cha Mafunzo Stadi Veta mkoani Mtwara, alisema maajabu yanayofanyika kwenye kaburi hilo, yanatisha na yanaweza kuwa hatari kwake.
"Mimi sijui atatumia mbinu gani lakini lazima iwe ushirikina au nguvu za kiroho. Hata hivyo ni vema akatafakari kwa kina uamuzi huo kwani unaweza kumgharimu na akaongeza historia ya kaburi hilo kwamba sasa, wamekufa watu watatu badala ya wawili," alisema Mwakalinga.
Alisema wakati wanatengeneza laini ya umeme eneo la kaburi hilo mwaka 2006, umeme uligoma kupita juu yake na wakalazimika kuhamisha njia ndipo walipofanikiwa.
Mwakalinga alipendekeza serikali kulifanyia uchunguzi kaburi hilo na ikiwezekana litangazwe kivutio cha watalii kwani kuna mambo mengi ya ajabu mbali na watu wawili kufariki dunia walipokuwa wanajaribu kuliondoa.
"Ukiwa huku Iringa utapata maelezo mengi kuhusu wazee wetu hawa, wengine walikuwa wanazikwa na vitu vyao, wengine walizikwa wakiwa wamekalishwa chini na hata baadhi yao walikuwa wanazikwa kwa kupakatwa na vijana wenye nguvu. Hayo yote ni historia yetu ambayo ni vyema tukaienzi,"alisema
Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti maajabu ya kaburi hilo mkazi wa Mafinga, Sadick lijitokeza na kusema anaweza kuliondoa bila wasiwasi wala madhara yeyote tofauti na maelezo ya watu kwamba watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa kujaribu kufanya hivyo.
Mhomanzi alitoa kauli hiyo wakati ambapo taarifa za uhakika kutoka katika eneo la kijiji hicho zikidai juhudi za kuliondoa kaburi hilo ili kupitisha barabara eneo hilo zimekuwa zikishindikana hata pale ilipotumika familia ya Marehemu Martin Kiyeyeu mwenyewe.
Lakini Mhomanzi kwa kujiamini alisema atakwenda yeye mwenyewe na kutumia jembe lake la mikono kuchimba na kuondoa udongo huo hadi mifupa ya marehemu Kiyeyeu na kuihamisha bila ya kudhurika.
"Amini maneno yangu kuona kaburi linashindikana kuondolewa, hakuna mtu anayeweza kushindwa, kaka mimi niko tayari nitafanya kazi hiyo kwa mkono wangu kabisa,"alisema Mhomanzi.
Mhomanzi alihoji "Kama ndugu wa marehemu wameridhia kuondolewa kwa kaburi hilo na kupatiwa eneo mbadala ni kitu gani kinaweza kuzuia? mimi siamini hivyo,Tanrods waniwezeshe mimi kuifanya kazi hiyo, nitakwenda na jembe langu pamoja na koleo kuifanya kazi hiyo nitakachokosa ni trekta la kubebea udongo na mifupa"alisema .
Source: Mwananchi.
Nadhani ile fitina kwamba watu watakufa sijui watu watapatwa na balaa mara sijui mizimu itakufata kwenye keyboard itakuwa imeisha maana hili kaburi lilikuwa ni tishio Iringa. Mie niliwahi kusema ni fikra na hisia za watu tu. Ukimuweka mungu mbele kanyaga twende basi it is all about having confidence in yourself.
Click to expand...
Tujifunue kwenye blanketi la ujinga tulilojifunika jamani. Kuhusu umeme kupindishwa tulishajadili hapa na sababu iliyotolewa... sio ushirikina. Kama sisi tunaojua kutumia computer tunakuwa na imani mbovu kama hizi ... je huko vijijini si ndio balaa? Nani atamwokoa mwingine?Baba Jose said:
Haya mambo yana ukweli,jiulize tu kwa nini umeme ulipindishwa,kilishofanyika ni wana ndugu wameridhia wamefanya tambiko na kumu omba mzee kiyeyu akubari ili barabara ipite kwa maendeleo ya taifa vinginevyo nakuambia kaburi lisingetoka
Vituko vya mochwariWatu wameendelea kuwa na nguvu zao hata wanapokufa.
Kaburi la Morris Kiyeyeu liligoma kuvunjwa kwa zaidi ya miaka arobaini ili kufisha miradi ya umeme na barabara ya Tanzam.
Mifano iko mingi Sana, ila hapa Kuna video inayoonyesha nduguye MK254 akigoma kupelekwa kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.
Dah!!!,Nimekukubali mkuu.Niliuliza kutaka uhakika kwasababu kuna mwaka nilipita maeneo Fulani ya iringa nikaona nyaya za umeme wamezichengesha nilipouliza wakasema eti umeme uligoma kuflow kisa nyaya kukatiza juu ya kaburi.Sasa naunganisha matukio.Babaangu ametengeneza Barabara eneo lile gari lao liligoma kuwaka eneo lile... Ndiye aliye nisimulia hadithi za pale... Anafahamu majina ya walio lala pale na miaka yao ya kufa akiwemo Martin kiyeyeu 1935
Sasa Bujibuji,huyo jamaa aliyekubali kumpakata,alibaki kaburini na kufia humo au alimpakata kwa muda then kabla ya mazishi alitoka?STORY YA KABURI LA KIYEYEU
FAHAMU ZAIDI KABURI LA MAAJABU
Kanungila Karim Kaburi la Mzee Martin Kiyeyeu aliyefariki mwaka 1974, kama linavyoonekana katika picha kando ya barabara ya Iringa-Mbeya
uliwahi kusikia maajabu ya Kaburi hili la mtu maarufu katika fani ya waganga wa jadi Almaarufu Kiyeyeu?
Kaburi la Kiyeyeu, lipo Njiapanda ya Mlolo pembezoni kabisa mwa barabara iendayo Mkoani Mbeya ukitokea Iringa lipo upande wako wa kulia, katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Hili ni kaburi alilozikwa mtu mmoja aliyekuwa Mganga maarufu wa jadi katika ukanda mzima wa maeneo ya mkoa huo, ambaye alifariki dunia miaka ya nyuma kidogo lakini hadi leo hii kaburi hilo ukiliona ni kama limejengwa jana. Ukiangalia kwa makini picha hii utaweza kuona jinsi nyaya za umeme wa Tanesco zilivyokwepa kaburi la Martin Kiyeyeu
Baada ya kufariki dunia mganga huyu, alizikwa kwa kufuata taratibu na mira za Machifu ambapo alizikwa kwa kusindikizwa na mtu aliye hai, aliyejitolea kwa ajili ya kuzikwa naye akiwa hai ili kumsindikiza, ambapo inadaiwa mtu huyo aliketi na kumpakata mganga huyo aliyezikwa huku akiwa amekaa.
Kaburi hilo limekuwa liwashangaza watu waliowengi na hata ndugu wa marehemu huyo kutokana na kuwa na maajabu na miujiza isiyoisha kana kwamba mtu huyo amezikwa mahala hapo jana.
Moja kati ya maajabu makubwa yaliyowahi kutokea mahala lilipo kaburi hilo ni wakati Shirika la umeme lilipokuwa katika zoezi la kuweka Nguzo za umeme pembezoni mwa barabara hiyo na kutokana na kaburi hilo kuwa karibu kabisa na barabara kubwa. Ndipo ilipoamuliwa kuweka nguzo hizo na kupitisha nyaya za umeme kiubishi.Lakini baada ya kumaliza zoezi hilo walishangazwa kwa kuona kuwa eneo la juu ya kaburi hilo hapakuwa ukipita umeme hali ya kuwa ulipoanzia hadi kabla na baada ya kaburi hilo umeme umejaa tele, ila eneo la juu ya kaburi hilo tu hakuna umeme.
Jambo hilo liliwafanya Tanesco kukubali matokeo na kuamua kuchukua uamuzi wa busara kwa kuhamishia baadhi ya nguzo hizo upande wa pili wa barabara ili kukwepa eneo hilo, hivyo nyaya hizo zikavuka barabara kabla ya kufikia kaburi hilo.
Baada ya kulivuka kaburi hili, na baada ya kufanya hivyo ummeme huo uliwaka na hadi hii leo unaendelea kuwaka, hivyo Serikali japo haiamini uchawi lakini hapa iliamini uchawi upo.
Moja ya maajabu ya kaburi hilo ni kushindwa kupitishwa kwa umeme kupita juu ya yake na pia linadaiwa kushindikana kuondolewa mara mbili na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga alipokuwa akijaribu kuling’oa.
Hata hivyo kaburi hilo na mengine 21 yaliyokuwa kwenye eneo hilo yaliondolewa na kuhamishiwa upande wa pili wa barabara, ambako kulikuwa na kaburi moja la mtoto wa kike wa Kiyeyeu, ambaye hakuzikwa katika eneo lililokuwa na makaburi ya ndugu zake baada ya mila na matambiko kufanyika.
Alizikwa haiSasa Bujibuji,huyo jamaa aliyekubali kumpakata,alibaki kaburini na kufia humo au alimpakata kwa muda then kabla ya mazishi alitoka?
Duh!!!!,kazi kweli kweli.Alizikwa hai
Familia ya Kiyeyeu ndiyo haikulipwa!Kwa maana ya kuwa mradi huo haukulipa fidia kwa mtu yeyote au familia ya kiyeyeu tu nids ilisahaulika katika fidia?