Mmanu
JF-Expert Member
- Feb 11, 2015
- 1,775
- 1,011
Habari wanaJf
Katika kufuatilia aina ya uchezaji wa hawa wachezaji wawili Onana wa Simba na Skudu wa Yanga kwa mechi mbili walizocheza kwa maana zile za utambulisho wa wachezaji na ngao ya jamii kule Tanga kuna vitu nimeviona vya utofauti kutoka kwa wachezaji hawa.
Mahalatse Makudubela "Skudu" amekuwa ni mchezaji ambaye amekuwa akifanya mambo mengi uwanjani yasiyo na tija kwa timu yake ikiwa pamoja na kupenda kukaa sana na mpira lakini mwishowe kupoteza lengo la huo mpira kwa kutozalisha faida yeyote. Amekuwa ni mchezaji wa kutaka sana kushangiliwa kwa kufanya vitu ambavyo mpira wa kisasa unavikataa 'ball dancer' japo amekuwa akiimbwa sana na mashabiki wa Yanga ila kwa mechi hizo mbili ikiwa hajafanya kitu chochote kilicholipa jitihada za mashabiki kumshangilia.
Willy Essomba Onana nae ameimbwa na mashabiki wake lakini amevimba kichwa kwa kutaka kuivaa Simba kuliko kutoa alichonacho jambo ambalo hupelekea kucheza kistaa na kupelekea kupoteza mpira kirahisi mno. Lakini faida ya huyu jamaa ni aina ya mpira wake ambao ni direct and objective footbal[emoji460] ambao ni aina ya soka la kisasa linalopendwa na makocha wengi wa kisasa duniani japo kuna wakati amekuwa akifanya mambo yanayoigharimu timu. Ameipa Simba mwanga na faida ya kile alichonacho.
Kwa soka la bongo ambalo leo shujaa kesho hufai kwa aina ya uchezaji wao na matumaini makubwa waliyonayo mashabiki wao wanayotegemea kutoka kwao je ni kweli wataendelea kupewa imani hiyo au watasalitiwa mapema tu?
Kwa wataalam wa masuala ya soka na wenye jicho la uchambuzi ni mchezaji yupi atakuwa wa kwanza kupewa "Thank you" na timu yake kwa hawa wachezaji wawili?