Ongeza nyama kwenye hoja!Ninachoweza kukwambia,one night stands huwa zinategemea na mazingira kadhaa...
Moja,mara nyingi inakuwa ni watu waliokwenda kikazi/kibiashara sehemu mbali mbali na wakakutana na watu waliowazimia lakini hakuna uwezekano wa uhusiano,hivyo wanaishia hapo.
Pili,mara nyingine unakuta kuna mtu amechukizwa na mpenzi wake na anapokwenda out na mihasira akishalewa,unakuta anafanya hayo mambo,na kesho yake anatambua kuwa bado yuko kwenye uhusiano na hivyo yanaishia hapo.Wengine,especially wanawake,hufanya kwa hasira baada ya kugundua mpenzi wake ame cheat on her.
Mwishowe,bila kujali kama muhusika ana uhusiano ama la,one night stands hutokea katika mazingira ya ulevi ambapo wahusika wanaangushiana nyota katika mazingira hayo(ya ulevi),wahusika hao mara nyingi huwa tayari wana mahusiano yao!Na hivyo wanachukulia matendo yao kama tamaa tu za kimapenzi.Pia inaweza kutokea kwa watu wanaofahamiana lakini hawako kwenye uhusiano.
Kimsingi one night stand huwa inatokea hivyo,yani muhusika hakuwa na mpango wa kuingia kwenye uhusiano pale anapo/alipo kutana na mwenzake waliyefanya naye mapenzi.