One on one Interview: Mch. Godfrey Malisa (anayesemekana kufukuzwa CCM) akifungukuka. Asema wamevunja katiba, hawafai kuwa viongozi tena..!!

One on one Interview: Mch. Godfrey Malisa (anayesemekana kufukuzwa CCM) akifungukuka. Asema wamevunja katiba, hawafai kuwa viongozi tena..!!

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
1,967
Reaction score
4,267

View: https://youtu.be/-NdDsArLVlU?si=eH35yrxDVCmdL3QM
➡️Huyu mzee anayesemekana kuwa amefukuzwa uanachama CCM, ni wazi kuwa yuko so determined kuhakikisha kuwa mchakato wa kumpitisha Bi Samia Suluhu Hassan na Dr Emmanuel Nchimbi kuwa wagombea urais huko CCM unarudiwa kwa kufuata taratibu na katiba ya CCM..

➡️ Kuna kila dalili kuwa yeye katangulizwa tu mbele Ili ashitue mitambo na kuona mwitikio wa wavunja kanuni na katiba. Lakini nyuma yake, wapi vigogo wa CCM na serikali yao wengi na wakubwa wakisubiri the right time to strike...

YAJAYO CCM YATAWAUMIZA WENGI NA KUWA NJIA YA KUKIONDOA CHAMA HIKI KWENYE RAMANI YA TAIFA LA TANGANYIKA...
 
Naona Mzee ameamua kuwa siriaz na jambo la uvunjifu wa Katiba
 
Nabii Sanga: CCM itapata mtikisiko na mpasuko mkubwa ambao Kila mtu atajua, tuiombee!
 
Hajui katiba ya CCM huyo

Mkutano mkuu ndio mkuubwa kimaamuzi kuliko kamati kuu na halmashauri kuu.Mkutano mkuu una uwezo hata wa kuvunja kamati kuu na halmashauri kuu yote na waweza hata kataa agenda zote za kamati kuu na halmashauri kuu wakaja na ya kwao mpya

Huyo Malisa hajui nguvu ya mkutano mkuu huyo

Mkutano uliamua kuja na agenda hiyo haikuwemo keenye agenda lakini kwa nguvu waliyonayo kikatiba ikaibuliwa na kupitishwa na wajumbe wote wa mkutano mkuu

Yeye Malisa kufukuzwa uanachama ni sahihi sababu anapinga kitu kilichopitishwa na kikso cha juu kabisa cha chama ambacho ni mkutano mkuu.Kile kilichofanywa na mkutano mkuu hakuna cha kamati kuu wala halmashauri kuu wenye ubavu wa kupinga sembuse yeye Malisa
 
Back
Top Bottom