One stop business center ya Ubungo ikijengwa itaua Kariakoo na kubadilisha mfumo mzima wa biashara Kwa Tanzania na nchi jirani

Yale majini yanayofugwa au kufanya mishe mishe kkoo hayatakubali. Na wachina wanslijua hilo watakuja na bizness model ambayo hsitaathiri kkoo.
 
View attachment 3086463Itachuana na Mlimani City kwa karibu
Kwani eneo hili la Urafiki hapo Ubungo litakuwa na tofauti gani na maeneo mengine kama hayo ambayo yanamilikiwa na Raia wa China yaliyopo kwenye nchi zingine mbalimbali hapa duniani?? Kwenye nchi kadhaa ambazo nilizowahi kuzuru hapa duniani nimewahi kuyaona maeneo ya biashara ya namna hiyo ambayo wenyewe wa-China wameyabatiza na kuyaita kwa Jina la 'China Town' au 'China City,' maeneo ya namna hiyo yapo katikà nchi mbali mbali.
 
Si kwel hata kidogo. Ile itakua kama mliman city tu kwa ajil ya aina flan ya watu na kkoo itabak kkoo kwaajil yetu watanganyika na raia wa visiwani pamoja na nchi jirani
 
Si kwel hata kidogo. Ile itakua kama mliman city tu kwa ajil ya aina flan ya watu na kkoo itabak kkoo kwaajil yetu watanganyika na raia wa visiwani pamoja na nchi jirani
Tusipuuze saana sababu inategemeana na ni nini serikali imekusudia. Iwapo bidhaa muhimu za China zitapatikana hapo kwa bei nafuu basi Kariakoo inaweza kuathirika sababu wateja wote wa mikoani na nchi jirani watakuwa na options.
 
Labda wawe na bandari yao wenyewe na TRA yao wenyewe ndo wataweza kuiua Kariakoo.
Kariakoo inaenda kufa kwa sababu ya ujanja sana , wachina wanaagiza moja kwa moja na mizigo yao ndani ya bongo ni nafuu kwa wauza wa mikoani .

Kariakoo haikuzwi na machinga unasikia ni soko kubwa Africa mashariki ni ile hali ya kuuza vitu kwa jumla . Na hapo kariakoo wabongo wanaoingia chimbo ni wachache sana wengi ni vibaraka wa wachina ndio wanaingiza mizigo moja kwa moja .

Ujio wa wachina baadhi ya mapapa watapoteza wateja wa jumla .
 
Wan
Meona wafanya biashara wa kariakoo mnawasikiliza sana Chadema.
Sasa wanashusha Mchina jikoni nyumbani mtakoma.
Kariakoo sasa hivi hao unaowasifia hapa hawaagizi tena mizigo kwa container zao wenyewe kama zamani,wanaagiza kupitia kwa makuli wao kama wafanyabiashara ndogo ndogo (hapa sijui kama nitaeleweka)

Yaani wanapeleka hela silent ocean (watu wanasema ni ya GSM) then mzigo unaandikwa ni wa Mtanzania mfanyabiashara mdogo mdogo kwa title lets say ya Ally (huyu ni mfanyakazi wa mchina mwenye viambatanisho vyote vya biashara but hana frame ni kuli tu) mzigo ukija unapelekwa godown kwa mchina maisha yanaenda.
 
Kariakoo lazima itayumba kidogo, Kwa sababu wanategemea kununua bidhaa za China na kutupandishia bei. Sasa kama bidhaa nitazipata hapo Ubungo kwa bei ya Kariakoo wakaazi wa Mbezi, Mwenge, Bagamoyo, Kibaha n.k watakwenda kufanya nini Kariakoo? Kwanza wengi hatupendi zile vurugu za wamachinga na kukoseakana kwa parking. Karikaoo kutabaki kwa watu wa Mbagala na Kigamboni tu
 
Mzee mchina akileta nyembe , akauza kwa Bei nafuuu , mimi nimenunua napeleka dukani narudi kko kufanya nini
Nina marafiki wenye maduka kariakoo, ninajua namna wanavyofanya biashara zao na tumeshajadili sana huu mradi kwa kina.

Hivyo naelewa ninachomaanisha hapa.

Wenye huo mradi wenyewe wanawategmea wafanyabiashara wa kariakoo wahamie hapo, na walikua wanawafuata kuwashawishi hivyo sio jambo rahisi kama unavyodhania wewe.
 
Kuruhusu ule ujenzi maana yake tumeruhusu Tanzania kuwa dampo la bidhaa za China.

Wachinà walipaswa anzisha viwanda ili kukabiriana na upungufu wa ajira.
Hata maduka yake yatajiri watanzania, flow ya wazambia , wacongo, Malawi, Burundi itakuwa kubwa sana so ajira zimo humo, mfano mimi nikichukua order za kubeba mzigo wa duka naupeleka nje huko au mikoani , huoni kama gari zangu zitakuwa zimepata kazi
 
Wakati mnajadili, mlihitimisha ni nini kitachosababisha wateja wa Kariakoo wasiende Ubungo kwa bidhaa ambazo zinapatikana Ubungo na Kariakoo?
 
Wakati mnajadili, mlihitimisha ni nini kitachosababisha wateja wa Kariakoo wasiende Ubungo kwa bidhaa ambazo zinapatikana Ubungo na Kariakoo?
Ni kweli italeta changamoto ila sio kwa haraka hivyo na kwa kiasi cha kuimaliza kabisa Kariakoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…