JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,957
Ilikuwa ni mwaka jana, Bw Ntembanda aliyekuwa akisoma chuo kimoja hapa dsm, bwana huyu akiwa mwajiliwa wa kampuni moja hapa mjini, bwana wa familia ya mke na watoto watano, alienda pale kujiendeleza akilipiwa na kampuni kwa shariti kuwa alitakiwa arudi ofisini na cheti kusudiwa na nje ya hapo kazi hana. Kama mnavyojua watu wenye familia wanaoenda kujiendeleza wengi wao uwezo wao ni mdogo sana.
Bwana Ntembanda kama ilivyo kwa watu wa aina yake alikuwa akifaulu kwa njia mbadala pale chuoni, akiwa mwaka wa 3 na wa mwisho tena mtihani wa mwisho akadakwa na kibomu ambacho matokeo yake ni DISCO,
haya ndo maneno aliyomwambia msimamizi wake, "DISCO yangu ina maana hii kwangu, nitafukuzwa kazi na matokeo yake maisha yangu yatakuwa rehani, familia yangu itasambaratika na kibaya zaidi huenda hata ndoa yangu ikafa, SITAKUBALI haya yatokee wewe ukiwa hai, hivyo basi ni ama uendelee na msimamo wako nidisco lakini na wewe uhai wako utakuwa halali yangu, nipo tayari kushinda kwa waganga mradi tu na wewe uharibikiwe, mwisho wa kunukuu".
Inasemekana mkwara huo ulimrudisha nyuma mwalimu yule na bwana Ntembanda akavaa gauni lake swaaaaafi mwaka jana.