Oneni huu mkwara kwa mwalimu.

Oneni huu mkwara kwa mwalimu.

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,957
Ilikuwa ni mwaka jana, Bw Ntembanda aliyekuwa akisoma chuo kimoja hapa dsm, bwana huyu akiwa mwajiliwa wa kampuni moja hapa mjini, bwana wa familia ya mke na watoto watano, alienda pale kujiendeleza akilipiwa na kampuni kwa shariti kuwa alitakiwa arudi ofisini na cheti kusudiwa na nje ya hapo kazi hana. Kama mnavyojua watu wenye familia wanaoenda kujiendeleza wengi wao uwezo wao ni mdogo sana.

Bwana Ntembanda kama ilivyo kwa watu wa aina yake alikuwa akifaulu kwa njia mbadala pale chuoni, akiwa mwaka wa 3 na wa mwisho tena mtihani wa mwisho akadakwa na kibomu ambacho matokeo yake ni DISCO,

haya ndo maneno aliyomwambia msimamizi wake, "DISCO yangu ina maana hii kwangu, nitafukuzwa kazi na matokeo yake maisha yangu yatakuwa rehani, familia yangu itasambaratika na kibaya zaidi huenda hata ndoa yangu ikafa, SITAKUBALI haya yatokee wewe ukiwa hai, hivyo basi ni ama uendelee na msimamo wako nidisco lakini na wewe uhai wako utakuwa halali yangu, nipo tayari kushinda kwa waganga mradi tu na wewe uharibikiwe, mwisho wa kunukuu".

Inasemekana mkwara huo ulimrudisha nyuma mwalimu yule na bwana Ntembanda akavaa gauni lake swaaaaafi mwaka jana.
 
Ningekuwa mimi ndio huyo mwalimu ningemjibu hivi ulipolalia wewe mimi ndipo nilipoamkia
 
Walimu ndio watumishi wanao ongoza kwa kwenda kwa waganga hapa tanzania.
 
Walimu ndio watumishi wanao ongoza kwa kwenda kwa waganga hapa tanzania. Sawa hata ndo nimetoka huko. Ila nilikuwa nawaloga wanaosababisha watoto wafeli. Kawambwa ameonekana kwenye Ramli ya mganga akifanya yake ya hovyo.
 
Ningekuwa mimi ndio huyo mwalimu ningemjibu hivi ulipolalia wewe mimi ndipo nilipoamkia

una roho ngumu basi, yaani uweke rehani maisha yako kisa mtu kufaulu? labda kama na wewe mshirikina, nilidhani utaanza maombi ningekuelewa.
 
Ilikuwa ni mwaka jana, Bw Ntembanda aliyekuwa akisoma chuo kimoja hapa dsm, bwana huyu akiwa mwajiliwa wa kampuni moja hapa mjini, bwana wa familia ya mke na watoto watano, alienda pale kujiendeleza akilipiwa na kampuni kwa shariti kuwa alitakiwa arudi ofisini na cheti kusudiwa na nje ya hapo kazi hana. Kama mnavyojua watu wenye familia wanaoenda kujiendeleza wengi wao uwezo wao ni mdogo sana. Bwana Ntembanda kama ilivyo kwa watu wa aina yake alikuwa akifaulu kwa njia mbadala pale chuoni, akiwa mwaka wa 3 na wa mwisho tena mtihani wa mwisho akadakwa na kibomu ambacho matokeo yake ni DISCO, haya ndo maneno aliyomwambia msimamizi wake, "DISCO yangu ina maana hii kwangu, nitafukuzwa kazi na matokeo yake maisha yangu yatakuwa rehani, familia yangu itasambaratika na kibaya zaidi huenda hata ndoa yangu ikafa, SITAKUBALI haya yatokee wewe ukiwa hai, hivyo basi ni ama uendelee na msimamo wako nidisco lakini na wewe uhai wako utakuwa halali yangu, nipo tayari kushinda kwa waganga mradi tu na wewe uharibikiwe, mwisho wa kunukuu". Inasemekana mkwara huo ulimrudisha nyuma mwalimu yule na bwana Ntembanda akavaa gauni lake swaaaaafi mwaka jana.

Inategemea na chuo chenyewe au msimaizi mwenyewe.Kuna siku alikamatwa mtu na hizo nondo,alipojaribu kuweka mkwara kama huo msimamizi akavua shati.Mwili mzima zilikua chale tupu.Akamwambia "Usinitishe mimi pia nimeaga nyumbani".Tulipofungua chuo jamaa alikua amedisco,mwalim yuko Dortmund anasoma Phd.Jiamini kwenye mtihani la sivo utafukuzwa mwaka wa mwisho uende kudanganya kwenu,utaskia eti "Nilkiua nawazidi akili maprofessor,nauliza sana maswali hadi wakanifukuza".
 
Back
Top Bottom