Ongeza AURA Yako: Jinsi ya Kuheshimika Bila Maneno

Dr Arshavin

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
26
Reaction score
80
Jinsi ya kuongeza AURA yako

(Define Aura As Ule Utulivu Wenye Nguvu Unaomfanya Kila Mtu Akuheshimu Na Kuhisi Uwepo Wako Bila Hata Wewe Kuongea Sana).

1. Ficha michongo yako, weka matokeo mezani.

Kuropoka sana kuhusu mipango yako kunavuja nishati (energy) yako bure. Matokeo huwa yana sauti kubwa na yenye mamlaka kuliko ahadi za mdomoni. Ukitembea kimya kimya na kuacha mafanikio yako yashuhudie, watu watakuchukulia siriaz kiwango cha juu sana.

2. Tabasamu la kiutu uzima (Mdomo ukiwa umefungwa).

Tabasamu la namna hii linaonyesha una self-control ya kutosha na unajiamini. Huhitaji kuoverreact au kucheka hovyo ili tu uonekane unavutia au unakubalika. Kujizuia huku kunamfanya mtu aonekane ana misingi na amekomaa kifikra.

3. Tikisa kichwa tu, sio kila saa kujieleza.

Kutikisa kichwa kunaonyesha umekubali au umeelewa jambo bila kuanza kuleta maneno mengi yasiyo na ulazima. Inakufanya uonekane mtu makini, mtulivu, mchunguzi mzuri wa mambo na unayetawala hisia zako vizuri mbele ya wengine.

4. Punguza stori za "Mimi hivi, mimi vile".

Wape nafasi wenzako wajifunue wenyewe kwanza. Uliza maswali ya akili, sikiliza zaidi, na uongee kidogo sana kuhusu mambo yako binafsi. Unapokuwa fumbo, heshima yako inaongezeka maradufu kwa sababu watu huwa wanathamini sana watu wasiotafuta kiki au attention.

5. Usiwe mtu wa kupatikana kila saa.

Ukiwa mtu wa kuitika kila unapoitwa au kutokea kila unapofatwa, unashusha thamani yako. Linda muda wako kwa wivu mkubwa. Watu wakijua upo busy unajenga utafutaji wako au unajifua, kile kipindi kidogo unachotokea kinakuwa na uzito na thamani kubwa sana kwao.

6. Piga mshiko thabiti (Firm Handshake).

Kushikana mikono kiungwana na kwa nguvu ya kiasi kunatuma ujumbe wa haraka sana ndani ya sekunde ya kwanza kuwa wewe ni mtu unayejiamini. Sio mshiko legelege wa kinyonge, na sio mshiko wa fujo au ubabe. Ni thabiti, wa kiume, na wenye msimamo.

7. Ongea kwa utulivu na kwa malengo.

Kuongea kwa haraka haraka na kukurupuka kunatuma picha kuwa una wasiwasi au uoga. Maneno ya taratibu, yenye sauti ya kueleweka na thabiti, yanabeba mamlaka makubwa. Chukua muda wako; watu watasikiliza kwa makini zaidi ukionyesha huna haraka ya kusikilizwa.

8. Vaa pamba safi, simple na nadhifu.

Huhitaji nguo za mamilioni ya pesa ili uonekane wa maana. Nguo safi, iliyokukaa vizuri mwilini na muonekano simple huwa unashinda siku zote. Jinsi unavyojiweka kwa nje inaonyesha ni kiasi gani unajiheshimu ndani yako na una nidhamu binafsi. Sio lazima uvae nguo zenye malogo makubwa.

9. Kuwa vizuri na ukimya (Comfortable with silence).

Ukimya ni nguvu kubwa sana. Huhitaji kulazimisha kujaza kila nafasi kwa maneno yasiyo na kichwa wala miguu pale mnapokuwa mmekaa na watu. Kuwa mtulivu hata kukiwa na ukimya kunaonyesha una nguvu kubwa ya ndani na una amani kamili na nafsi yako.
 
Najieleza ,sifichi mambo yangu , na bado natamba , sio bar sio kazini sio kwenye biashara , tafuta lingine motivation spika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…