Ongeza faida kwenye biashara yako kwa kumkwepa middle man

Ongeza faida kwenye biashara yako kwa kumkwepa middle man

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,001
Reaction score
23,449
Maisha ya biashara na ujasiriamali kila unapoamka inapaswa upashe akili moto kuongeza ile 500 uliyoipata jana leo upate 1000 na kesho kutwa upate 1500 Hiyo ndio inatwa biashara na ujasiriamali.

Leo nataka kuandika kitu kidogo chakufungulia mwaka kuamsha waliolala,na jambo lingine leo nataka zaidi kuongea na wale wanaolalamika hawaoni faida katika biashara wanazofanya ijapokua wana wateja na biashara inaenda hata mtu ukienda kazini kwake kweli unaona kbsa huyu mtu anauza anapata pesa lakini yeye kiuhalisia moyoni mwake jioni anajua fika kbsa sipati kitu cha maana.

WATU wa namna hii mpo,najua upo sehemu unajifkiria kuacha hiyo bishara ujaribu biashara nyingine labda utatoboa,ila leo nataka tuongee kitu flani kisha ntaomba mkijaribu kwa vitendo,msipoona matunda yake basi nawaruhusu kufunga au kubadilisha biashara mnayofanya ila kwasasa naomba usifunge biashara au kubadilisha biashara,soma hii thread taratbu uielewe kisha ingia nayo kwenye vitendo.

Middle Man/Mtu wa katikati/Dalali
Huyu n yule mtu anaewasiliana moja kwa moja na mzalisha bidhaa anainunua kisha na yeye ndio anakuja kukuuzia wewe mfanyabiashara,najua n mara nyingi tunaenda masokoni/madukani kununua vitu mbali mbali vya biashara yetu wale wanaotuuzia vile vitu huko masokoni/madukani ndio hawa leo nataka tuwaongelee hawa ndio ma middle man wenyewe.

Yawezekana unauza sana halafu hujui hela inaenda wapi,unafanya biashara sana ila huoni ukpga hatua mbele shida sio biashara yako ila shida na mchawi anaekuvuta shati usiende mbele ni huyu middle man wala hujalogwa.

Unapotaka kuona faida ya ujasiriamali/biashara yako jitahidi kufa na kupona,afe kipa afe beki,kwa jasho na damu fanya kila unaloweza kumkwepa middle man ndipo utakapoona faida ya ujasiriamali na biashara yako. Nitatolea mifano ya biashara kadhaa ili nieleweke nin hasa naongelea leo.

KUUZA MKAA
Kuna mtu yupo mahali anafanya biashara ya kuuza mkaa kwa watu wa mtaani kwake,ukimuuliza mka ananunua wapi yeye atakwambia Pale mbeleeee kuna mama anauza mkaa kwa jumla,unapoenda kununua mkaa kwa yule mtu kumbuka yeye hachomi miti wala hatengenezi mkaa kwa maana hiyo na yeye ananunua kisha anakuja kukuuzia wewe, Gunia analonunua 50,000 yeye anakuja kukupga 150,000,sasa wewe muuza mkaa kwanini usimruke huyu mtu ukaenda tafuta mkaa huko porini kwa watengeneza mkaa wenyewe, unafkiri hautopata?

Ukifanikiwa kwende porini mwenyewe gunia utalichukua kwa 50k na utakuja kupata faida mara mbili ya ile uliyokua ukipata mwanzo,inawezekana amua tu kuacha uvivu na uinuke hapo ulipo ukatafute mwenzako anapata wapi huo mkaa.

KUUZA CHIPSI
Kuna mtu huu mwaka wa 5 anafanya biashara ya chipsi lakini maendeleo n 1+1-2 analalamika kalogwa,muulize unanunua wapi viazi anakwambia ananunua mabibo sokoni au soko kuu,gunia linauzwa sokoni 100,000 tena hapo limeshapunguzwa punguzwa ndipo mnauziwa laki,wakati ujazo wagunia hilo la laki yawe magunia matatu ndio gunia 1 kwa mkulima shambani na shambani gunia mkulima anauza 80,000, lakini kutokana na uvivu wetu wakusubiri mpaka tuletewe sokoni ndio tufate viazi tunaenda nunua mtoto wa gunia kwa 100,000,hivi unategemea faida utaipatia au iona wapi?

Uwezo wa kwenda shambani unao kama unaweza fata gunia sokoni unashndwa nn kufata gunia kwa mkulima wa viazi shambani,ila upo unasubiri Middle man akuletee,sawa kaaa hapo subiri uletewe utalikuta sokoni.

BIASHARA YA GENGE
Mtu ananunua karoti sokoni,hoho sokoni hajiulizi hizi hoho/karoti zinatoka wapi,kwann mimi nisizifate huko zinakotoka? anasubiri karoti auziwe moja 300 wakati akienda shambani mkulima anamuuzia Ndoo ya lita kumi sh.3000,hivi ndoo ya lita kumi mpaka ijae ina karoti ngapi ndani? Lakini yeye anasubri aletewe pale soko kuu akanunue 500 aje atupge mtaani karoti sh 700 atuambie karoti saivi ni BEI kumbe n uzembe wake na uvivu wake. Ukigusa Limao gengeni saivi unaweza ambiwa ni buku ila muulize huyo muuza genge katoa wapi hilo limao atakwambia soko kuu.

BIASHARA YA GESI na VIFAA VYAKE
Upo ofisini unauza gesi zikikuishia unavuta simu unapga unaletewa na kampuni hadi mlangoni,hivi umeshawahi jiliza what if nikifata mwenyewe hizi gesi ntauziwa kiasi gani? niwambie tu wauza gesi fateni gesi wenyewe huko zinapojazwa,Mtanishukuru badae kwa bei mtakayoikuta.

Unauza burner/Stand/Regulator/Pipe hivi vifaa umewahi kujua vinatengenezewa wapi? jiulize kisha vifate kutoka kwa mtengenezaji mkwepe middle man yule unaempgia simu akuletee vifaa kila vikiisha utaona bei utayoikuta.

MAMA NTILIE
Tukiachana na hawa wanaokopa vitu kwa mangi then wanalipa jioni,nawaongelea nyie mnaonunua mchele kwa cash mnauziwa kilo ya mchele 2500 hivi umeshaenda kahama huko au magugu au mbeye mchele unakotoka ukajua bei ya huo mchele unaouziwa kilo 2500,ni kwamba hiyo bei unapigwa mruke huyo middle man uone matunda ya ujasiriamali wako.

Tuache uvivu ndugu zangu tusisubiri kuletewa kisha ndio tukanunue,wanaofata mizigo china sio kwamba wao n maboss sana au wanapenda sifa hao wote wameshaona madhara ya middle man,kama unafanya biashara yoyote usipende mambo ya Free delivery sijui toa oda tunakuletea usipende hizo ofa ndio zinapunguza faida yako na mwisho unaona hupati faida kumbe unapata,Middle man ndio anaekufanya wewe ujione kama hela yako inapotea hujui inakoenda.

Kabla hujafunga au kubadlisha biashara unayofanya hebu mkwepe middle man halafu fata mzigo production center halafu tuone kama ndani ya mwezi huu mawazo ya kufunga hyo biashara kama yataendelea kuwepo.

Faida ya mauzo yako inapotezwa na huyo middle man ndie anaekupa loss wala sio kwamba una matumizi makubwa au nni TUACHE UVIVU vyakuletewa vina gharama.

Heri ya Mwaka Mpya.
 
Leo umeyumba mzee

Sasa hawa wafanya biashara wafuate gesi kiwandani kabisa mbona kama haileti maana hivi, hebu wewe fikiria kila mfanyabiashara afuate gesi kiwandani ni usumbufu kiasi gani utakuwepo kwa kiwanda husika katika kuhudumia wateja hapa ni sawa pia kwa kampuni za kuzalisha soda.

Alafu kwa watu wenye magenge unakuta mtaji wao wengine hauzidi hata 30,000, sasa afuate nyanya shambani kweli wakati yeye Mwenyewe anauza kulingana na uwepo wa wahitaji wa hizo huduma ndio unataka afuate karoti au nyanya shambani kwa kukwepa shilingi 200.
 
Duuuh... mkuu biashara inaenda stage kwa stage sio kama unavyotaka wewe hvyo.

Kwenye biashara kuna makundi makuu kama manner hv.
1" mzalishaji (producer/manufacturer)

2" msambazaji/mnunuaji wa jumla kutoka kwa mzalishaji (wholesaler/supplier)

3" mnunuaji wa jumla kutoka kwa msambazaji anajulikana kama mchuuzi/mmachinga (retailer)

4" mnunuzi wa mwisho/ mtumiaji (final consumer)

Sasa apo wewe retailer kwenda moja kwa moja kwa manufacturer kununua mzigo si kazi rahisi coz kuna vigezo inabidi uwe navyo either uwe na sifa za kuwa wholesaler.

NB:- mtaji wako na maarifa yako ndo yatakuweka katka kundi fulani.
 
Mkuu, umepiga cha Arusha ndio ukaandika huo upupu au

Muuza chipsi huyu mwenye mtaji wa 700k (pungufu) , ili akwepe 'mido mani' inabidi:

1. Afuate viazi shambani moja kwa moja, kesho utasema awe na shamba lake la viazi
2. Afate nyanya za kachumbari shambani moja kwa moja, kesho utasema awe na shamba la nyanya, amkwepe mwenye shamba ambaye pia ni mido mani in disguise
3. Afate mafuta pale Murzah moja kwa moja, wakati pale wanauza kwa jumla,
4. Awe na kiwanda cha kutengeneza tomato cha kwake,
5. Afate nyama ya mishkaki kule Pugu , akwepe madalali wa Vingunguti, kesho utasema afuge ng'ombe wake mwenyewe

Icho kitu hakuna, mfumo wa biashara ni kutegemeana kutoka mzalishaji mkuu mpaka mtumiaji wa mwisho

Ingekuwa mido mani wa vyumba sawa
 
Duuuh... mkuu biashara inaenda stage kwa stage sio kama unavyotaka wewe hvyo.

Kwenye biashara kuna makundi makuu kama manner hv.
1" mzalishaji (producer/manufacturer)

2" msambazaji/mnunuaji wa jumla kutoka kwa mzalishaji (wholesaler/supplier)

3" mnunuaji wa jumla kutoka kwa msambazaji anajulikana kama mchuuzi/mmachinga (retailer)

4" mnunuzi wa mwisho/ mtumiaji (final consumer)

Sasa apo wewe retailer kwenda moja kwa moja kwa manufacturer kununua mzigo si kazi rahisi coz kuna vigezo inabidi uwe navyo either uwe na sifa za kuwa wholesaler.

NB:- mtaji wako na maarifa yako ndo yatakuweka katka kundi fulani.
Kiuhalisia wewe umesoma commerce kama sijakosea unajua channel of distribution, nimependa haya maelezo yako ya mwisho hapo kwenye NB:- sasa mtaji unaenda na vigezo.
 
mkuu, umepiga cha Arusha ndio ukaandika huo upupu au

muuza chipsi huyu mwenye mtaji wa 700k ( pungufu ) , ili akwepe 'mido mani' inabidi:

1. afuate viazi shambani moja kwa moja, kesho utasema awe na shamba lake la viazi
2. afate nyanya za kachumbari shambani moja kwa moja, kesho utasema awe na shamba la nyanya, amkwepe mwenye shamba ambaye pia ni mido mani in disguise
3. afate mafuta pale Murzah moja kwa moja, wakati pale wanauza kwa jumla,
4. awe na kiwanda cha kutengeneza tomato cha kwake,
5. afate nyama ya mishkaki kule Pugu , akwepe madalali wa Vingunguti, kesho utasema afuge ng'ombe wake mwenyewe

icho kitu hakuna, mfumo wa biashara ni kutegemeana kutoka mzalishaji mkuu mpaka mtumiaji wa mwisho

ingekuwa mido mani wa vyumba sawa
Hahaha jamaa umenifurahisha sana unapomalizia kuwa mwisho wa siku muuza chips awe na kila kitu chake kumkwepa middle man, ila jamaa leo kateleza na bandiko lake lipo wazi.
 
Yaani muuza genge itambidi afate nyanya Kilolo Iringa huko, apitie karoti na kabeji, morogoro milimani huko Mgeta, akachukue bamia morogoro dumira pale, au kigamboni mbutu kwa Yericko Nyerere au kimbiji kule, halafu akafate vitunguu Singida kule...wakati vyote hivyo akienda Sokoni anavikuta kwa pamoja na kuchukua na kuondoka zake kutengeneza kafaida kake.

Halafu mkuu unadhani kununua nkaa kwa producer na kuusafirisha ni kazi rahisi? Leseni ya kuwa mnunuzi na muuzaji ni kama laki sita....sasa huyo mama mwenye genge anayenunua gunia moja moja anayeuza rejareja kwa kisado ana huo uwezo wa kufata mkaa porini? Manaa akienda itambidi angalau anunue kuanzia gunia 100
 
Kuna vitu bandiko lako linaleta maana , ila kuna vingine sio kaz rahs kama unavyofikria....vitu vingine vinaathiriwa na ukritimba wa serikali ....kuwekeana vibali pesa ndefu , miundo mbinu mibovu n.k...leo Tu kusafrisha samak toka Mwanza unazongwa zongwa daah....

Angalia nchi za wenzetu wamerahsisha mambo Kias kwamba unaweza agiza kifutio kimoja toka China tena Kwa free shipping..... Hvyo inakuwa rahs kumkwepa middle men, kumkwepa middle men bongo ni ngumu Kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano hii inachangizwa na serikali Kwa 75%
 
Binafsi nimekuelewa Sana mtoa maada, tatizo hapo ni mtaji muuza chipsi wa Dar hawezi kwenda Njombe kununua gunia moja la viazi.
Nauli ya Dar kwenda njombe tu ni zaidi ya laki.....sasa utatoa laki kufuata gunia moja au mawili ya viazi, na bado kuyasafirisha.

Nadhani mleta mada amekurupuka. Middlemen ni principle connection kati ya manufacturers na final users.

Haya ndio matatizo ya kutokusoma vizuri masomo ya commerce.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo ni zuri sana ila nadhani linaleta mkanganyiko katika nitalifanyaje haliyakua mtaji wangu ni mdogo!?

Naam baada ya kusoma nimeamua kua nitafute wenzangu kadhaa wenye magenge ya mkaa halafu tuagize moja kwa moja huko unakotengenezwa! kwakua siwezi kufanya mm peke yangu wacha nishirikishe wajasiriamali wenzangu tuungane tuipige hiyo hela ya middleman, afterall business is about taking risks.

Hili bandiko halikua la kila mtu.


Asanteni sana.
 
Unapotaka kuona faida ya ujasiriamali/biashara yako jitahidi kufa na kupona,afe kipa afe beki,kwa jasho na damu fanya kila unaloweza kumkwepa middle man ndipo utakapoona faida ya ujasiriamali na biashara yako.
 
Back
Top Bottom