Ongeza faida kwenye biashara yako kwa kumkwepa middle man

Middle man wapo na wanakuwepo kwa sababu ya mambo mengi,

Lets say unafuga kuku, Ukisema uuze Directly kwa enduser utaweza supply?

Mahoteli huwa yana watu wanaitwa supplier huyu supplier hupewa tenda ya kuleta mahitaji hotelini na anacho kifanya yeye ni kukusanya kwa wazalishaji mbalimbali na mzigo ukifika anapeleka kwa Hotelini.

Kuuza Directly kunahitaji mitaji mikubwa na kuhakikisha Usambazaji hasimami.

Sasa unalima tikitika unavuna mara baada ya wiki zimakata unaanza tena kuotesha zingine, sasa hapo katikati watakaa wanakusubilia?

Pia kitumia Middle man kuna faida sana hasa kupunguza sales coast, kama mtu anakuja kununua mzigo shambani kwako na wewe unaona kuna faida unatafuta nini tena?

Kubwa ni je unapata faida?
 
Nilikua nafikiri ni mimi tu ndo naona mtoa mada anaandikaga pumba point.
Huyu mtoa mada ni mara nyingi anaandika point ambazo hazipo practical na ndipo zinageuka pumba, huu uzi alipoupost niliusoma ukiwa na comment moja tu nikasema ngoja nipite zangu kimya kimya, nafikiri ni mtu mwenye uelewa fulani na anaweza kusimamia biashara ambayo tayari iko imara na akawa mbunifu kuiongezea kampuni faida lakini asiweze kuwa mzuri katika kuanzisha ya kwake na ikasimama, no offence.

Nina rafiki yangu amesomea usimamizi wa biashara, na anafanya kazi katika taasisi fulani kubwa tu, huwa akinishauri chochote kuhusu biashara yangu/zangu, mimi humjibu kuna elimu ya biashara ya mtaani ambayo wewe huijui hivyo siwezi kukuona kama mtu bora katika kumpa mfanyabiashara ushauri.

Theories fulani fulani za biashara haziapply kivitendo katika mazingira yetu ya kibiashara hasa katika nchi yetu. Anyways sio vizuri kumdiscuss mleta mada badala ya mada, lakini kama lengo lake ni kufundisha watu, positively ajikite katika tafiti hasa zinazofavour mazingira yetu.
 
Maisha ya biashara na ujasiriamali kila unapoamka inapaswa upashe akili moto kuongeza ile 500 uliyoipata jana leo upate 1000 na kesho kutwa upate 1500 Hiyo ndio inatwa biashara na ujasiriamali.

Leo nataka kuandika kitu kidogo chakufungulia mwaka kuamsha waliolala,na jambo lingine leo nataka zaidi kuongea na wale wanaolalamika hawaoni faida katika biashara wanazofanya ijapokua wana wateja na biashara inaenda hata mtu ukienda kazini kwake kweli unaona kbsa huyu mtu anauza anapata pesa lakini yeye kiuhalisia moyoni mwake jioni anajua fika kbsa sipati kitu cha maana.

WATU wa namna hii mpo,najua upo sehemu unajifkiria kuacha hiyo bishara ujaribu biashara nyingine labda utatoboa,ila leo nataka tuongee kitu flani kisha ntaomba mkijaribu kwa vitendo,msipoona matunda yake basi nawaruhusu kufunga au kubadilisha biashara mnayofanya ila kwasasa naomba usifunge biashara au kubadilisha biashara,soma hii thread taratbu uielewe kisha ingia nayo kwenye vitendo.

Middle Man/Mtu wa katikati/Dalali
Huyu n yule mtu anaewasiliana moja kwa moja na mzalisha bidhaa anainunua kisha na yeye ndio anakuja kukuuzia wewe mfanyabiashara,najua n mara nyingi tunaenda masokoni/madukani kununua vitu mbali mbali vya biashara yetu wale wanaotuuzia vile vitu huko masokoni/madukani ndio hawa leo nataka tuwaongelee hawa ndio ma middle man wenyewe.

Yawezekana unauza sana halafu hujui hela inaenda wapi,unafanya biashara sana ila huoni ukpga hatua mbele shida sio biashara yako ila shida na mchawi anaekuvuta shati usiende mbele ni huyu middle man wala hujalogwa.

Unapotaka kuona faida ya ujasiriamali/biashara yako jitahidi kufa na kupona,afe kipa afe beki,kwa jasho na damu fanya kila unaloweza kumkwepa middle man ndipo utakapoona faida ya ujasiriamali na biashara yako. Nitatolea mifano ya biashara kadhaa ili nieleweke nin hasa naongelea leo.

KUUZA MKAA
Kuna mtu yupo mahali anafanya biashara ya kuuza mkaa kwa watu wa mtaani kwake,ukimuuliza mka ananunua wapi yeye atakwambia Pale mbeleeee kuna mama anauza mkaa kwa jumla,unapoenda kununua mkaa kwa yule mtu kumbuka yeye hachomi miti wala hatengenezi mkaa kwa maana hiyo na yeye ananunua kisha anakuja kukuuzia wewe, Gunia analonunua 50,000 yeye anakuja kukupga 150,000,sasa wewe muuza mkaa kwanini usimruke huyu mtu ukaenda tafuta mkaa huko porini kwa watengeneza mkaa wenyewe, unafkiri hautopata?

Ukifanikiwa kwende porini mwenyewe gunia utalichukua kwa 50k na utakuja kupata faida mara mbili ya ile uliyokua ukipata mwanzo,inawezekana amua tu kuacha uvivu na uinuke hapo ulipo ukatafute mwenzako anapata wapi huo mkaa.

KUUZA CHIPSI
Kuna mtu huu mwaka wa 5 anafanya biashara ya chipsi lakini maendeleo n 1+1-2 analalamika kalogwa,muulize unanunua wapi viazi anakwambia ananunua mabibo sokoni au soko kuu,gunia linauzwa sokoni 100,000 tena hapo limeshapunguzwa punguzwa ndipo mnauziwa laki,wakati ujazo wagunia hilo la laki yawe magunia matatu ndio gunia 1 kwa mkulima shambani na shambani gunia mkulima anauza 80,000, lakini kutokana na uvivu wetu wakusubiri mpaka tuletewe sokoni ndio tufate viazi tunaenda nunua mtoto wa gunia kwa 100,000,hivi unategemea faida utaipatia au iona wapi?

Uwezo wa kwenda shambani unao kama unaweza fata gunia sokoni unashndwa nn kufata gunia kwa mkulima wa viazi shambani,ila upo unasubiri Middle man akuletee,sawa kaaa hapo subiri uletewe utalikuta sokoni.

BIASHARA YA GENGE
Mtu ananunua karoti sokoni,hoho sokoni hajiulizi hizi hoho/karoti zinatoka wapi,kwann mimi nisizifate huko zinakotoka? anasubiri karoti auziwe moja 300 wakati akienda shambani mkulima anamuuzia Ndoo ya lita kumi sh.3000,hivi ndoo ya lita kumi mpaka ijae ina karoti ngapi ndani? Lakini yeye anasubri aletewe pale soko kuu akanunue 500 aje atupge mtaani karoti sh 700 atuambie karoti saivi ni BEI kumbe n uzembe wake na uvivu wake. Ukigusa Limao gengeni saivi unaweza ambiwa ni buku ila muulize huyo muuza genge katoa wapi hilo limao atakwambia soko kuu.

BIASHARA YA GESI na VIFAA VYAKE
Upo ofisini unauza gesi zikikuishia unavuta simu unapga unaletewa na kampuni hadi mlangoni,hivi umeshawahi jiliza what if nikifata mwenyewe hizi gesi ntauziwa kiasi gani? niwambie tu wauza gesi fateni gesi wenyewe huko zinapojazwa,Mtanishukuru badae kwa bei mtakayoikuta.

Unauza burner/Stand/Regulator/Pipe hivi vifaa umewahi kujua vinatengenezewa wapi? jiulize kisha vifate kutoka kwa mtengenezaji mkwepe middle man yule unaempgia simu akuletee vifaa kila vikiisha utaona bei utayoikuta.

MAMA NTILIE
Tukiachana na hawa wanaokopa vitu kwa mangi then wanalipa jioni,nawaongelea nyie mnaonunua mchele kwa cash mnauziwa kilo ya mchele 2500 hivi umeshaenda kahama huko au magugu au mbeye mchele unakotoka ukajua bei ya huo mchele unaouziwa kilo 2500,ni kwamba hiyo bei unapigwa mruke huyo middle man uone matunda ya ujasiriamali wako.

Tuache uvivu ndugu zangu tusisubiri kuletewa kisha ndio tukanunue,wanaofata mizigo china sio kwamba wao n maboss sana au wanapenda sifa hao wote wameshaona madhara ya middle man,kama unafanya biashara yoyote usipende mambo ya Free delivery sijui toa oda tunakuletea usipende hizo ofa ndio zinapunguza faida yako na mwisho unaona hupati faida kumbe unapata,Middle man ndio anaekufanya wewe ujione kama hela yako inapotea hujui inakoenda.

Kabla hujafunga au kubadlisha biashara unayofanya hebu mkwepe middle man halafu fata mzigo production center halafu tuone kama ndani ya mwezi huu mawazo ya kufunga hyo biashara kama yataendelea kuwepo.

Faida ya mauzo yako inapotezwa na huyo middle man ndie anaekupa loss wala sio kwamba una matumizi makubwa au nni TUACHE UVIVU vyakuletewa vina gharama.

Heri ya Mwaka Mpya.
Ukimkwepa middle man wengine watakula wapi mzee, na ni lazima tutegemeane, supply chain haikwepeki mzee, tena kwa kuongeza thamani ya mnyororo ndiyo inatoa fursa kukuza uchumi kwa mmoja mmoja.
 
Leo umeyumba mzee
Sasa hawa wafanya biashara wafuate gesi kiwandani kabisa mbona kama haileti maana hivi, hebu wewe fikiria kila mfanyabiashara afuate gesi kiwandani ni usumbufu kiasi gani utakuwepo kwa kiwanda husika katika kuhudumia wateja hapa ni sawa pia kwa kampuni za kuzalisha soda.

Alafu kwa watu wenye magenge unakuta mtaji wao wengine hauzidi hata 30,000, sasa afuate nyanya shambani kweli wakati yeye Mwenyewe anauza kulingana na uwepo wa wahitaji wa hizo huduma ndio unataka afuate karoti au nyanya shambani kwa kukwepa shilingi 200
Hata mimi hii bado sijaona kama ipo sawa, ukiachana na msongamano wa kila mtu kwenda kiwandani swala la kufuata wewe mwenyewe kiwandani inaongeza gharama, muda pia ukipiga hesabu usafiri unaotumia muda pia unatumia kwenda kuchukua mzigo unatengeneza hasara n8 mara mbili na atakavyokuletea wakala.
 
Huyu mtoa mada ni mara nyingi anaandika point ambazo hazipo practical na ndipo zinageuka pumba, huu uzi alipoupost niliusoma ukiwa na comment moja tu nikasema ngoja nipite zangu kimya kimya, nafikiri ni mtu mwenye uelewa fulani na anaweza kusimamia biashara ambayo tayari iko imara na akawa mbunifu kuiongezea kampuni faida lakini asiweze kuwa mzuri katika kuanzisha ya kwake na ikasimama, no offence.

Nina rafiki yangu amesomea usimamizi wa biashara, na anafanya kazi katika taasisi fulani kubwa tu, huwa akinishauri chochote kuhusu biashara yangu/zangu, mimi humjibu kuna elimu ya biashara ya mtaani ambayo wewe huijui hivyo siwezi kukuona kama mtu bora katika kumpa mfanyabiashara ushauri.

Theories fulani fulani za biashara haziapply kivitendo katika mazingira yetu ya kibiashara hasa katika nchi yetu. Anyways sio vizuri kumdiscuss mleta mada badala ya mada, lakini kama lengo lake ni kufundisha watu, positively ajikite katika tafiti hasa zinazofavour mazingira yetu.
Umeongea vizuri ni vyema ushauri uakisi hali halisi ya mazingira hilo tu, maana mambo ya theory peke hayana msaada
 
Hata kununua vitu kwa bei ya jumla Kuna okoa gharama za uzalishaji na kuongeza faida. Kuna mama mmoja alikuwa anakaanga halfcake akawa anataka aache kwa sababu haoni faida nikamshauri badala ya kununua unga kwa kilo anunue mfuko , badala ya kununua mafuta ya kupima anunue ndoo ya mafuta, tatizo kweli likawa mtaji lakini baada ya kumpiga tafu kidogo Sasa hivi anaendelea vizuri na faida inaonekana
 
Huu uzi unatufaa sisi tunaopenda kufanya shopping ya mwezi kwa mahitaji ya nyumbani na siyo wanaopenda kushinda na vidumu vya kupima mafuta ya kupikia na sukari za kupima, hata ndo maana wanalalamika maisha magumu, ukienda duka la jumla unanunua mahitaji yako kwa mwezi unajikuta umasave sana tofauti na kununua mtaani, mtaani nenda nunua kwa emagence tu, Sasa tuje kwenye biashara Kuna vitu unajitahidi umukwepe middle man Ili kuongeza faida kwenye biashara yako kadiri unaizoea biashara, hata maduka ya mangi Kuna wanaopelekewa soda kutoka kiwandani kwa gharama za kiwandani na hata bidhaa zingine na ndo maana Kila kiwanda kina sales man wewe ni kazi yako kuwatafuta Ili ununue kwa gharama za kiwandani na usafiri juu yao, Sasa hapo Kuna vitu huwezi kuvipata kutoka kiwandani hivyo ndo nunua kwa hao middle man, hili somo wataelewa wale wanaofanya biashara zenye bidhaa tofauti tofauti Kama maduka ya hardware yaani mzigo unakufikia kutoka kiwandani kwa gharama za kiwandani.
 
Maisha ya biashara na ujasiriamali kila unapoamka inapaswa upashe akili moto kuongeza ile 500 uliyoipata jana leo upate 1000 na kesho kutwa upate 1500 Hiyo ndio inatwa biashara na ujasiriamali.

Leo nataka kuandika kitu kidogo chakufungulia mwaka kuamsha waliolala,na jambo lingine leo nataka zaidi kuongea na wale wanaolalamika hawaoni faida katika biashara wanazofanya ijapokua wana wateja na biashara inaenda hata mtu ukienda kazini kwake kweli unaona kbsa huyu mtu anauza anapata pesa lakini yeye kiuhalisia moyoni mwake jioni anajua fika kbsa sipati kitu cha maana.

WATU wa namna hii mpo,najua upo sehemu unajifkiria kuacha hiyo bishara ujaribu biashara nyingine labda utatoboa,ila leo nataka tuongee kitu flani kisha ntaomba mkijaribu kwa vitendo,msipoona matunda yake basi nawaruhusu kufunga au kubadilisha biashara mnayofanya ila kwasasa naomba usifunge biashara au kubadilisha biashara,soma hii thread taratbu uielewe kisha ingia nayo kwenye vitendo.

Middle Man/Mtu wa katikati/Dalali
Huyu n yule mtu anaewasiliana moja kwa moja na mzalisha bidhaa anainunua kisha na yeye ndio anakuja kukuuzia wewe mfanyabiashara,najua n mara nyingi tunaenda masokoni/madukani kununua vitu mbali mbali vya biashara yetu wale wanaotuuzia vile vitu huko masokoni/madukani ndio hawa leo nataka tuwaongelee hawa ndio ma middle man wenyewe.

Yawezekana unauza sana halafu hujui hela inaenda wapi,unafanya biashara sana ila huoni ukpga hatua mbele shida sio biashara yako ila shida na mchawi anaekuvuta shati usiende mbele ni huyu middle man wala hujalogwa.

Unapotaka kuona faida ya ujasiriamali/biashara yako jitahidi kufa na kupona,afe kipa afe beki,kwa jasho na damu fanya kila unaloweza kumkwepa middle man ndipo utakapoona faida ya ujasiriamali na biashara yako. Nitatolea mifano ya biashara kadhaa ili nieleweke nin hasa naongelea leo.

KUUZA MKAA
Kuna mtu yupo mahali anafanya biashara ya kuuza mkaa kwa watu wa mtaani kwake,ukimuuliza mka ananunua wapi yeye atakwambia Pale mbeleeee kuna mama anauza mkaa kwa jumla,unapoenda kununua mkaa kwa yule mtu kumbuka yeye hachomi miti wala hatengenezi mkaa kwa maana hiyo na yeye ananunua kisha anakuja kukuuzia wewe, Gunia analonunua 50,000 yeye anakuja kukupga 150,000,sasa wewe muuza mkaa kwanini usimruke huyu mtu ukaenda tafuta mkaa huko porini kwa watengeneza mkaa wenyewe, unafkiri hautopata?

Ukifanikiwa kwende porini mwenyewe gunia utalichukua kwa 50k na utakuja kupata faida mara mbili ya ile uliyokua ukipata mwanzo,inawezekana amua tu kuacha uvivu na uinuke hapo ulipo ukatafute mwenzako anapata wapi huo mkaa.

KUUZA CHIPSI
Kuna mtu huu mwaka wa 5 anafanya biashara ya chipsi lakini maendeleo n 1+1-2 analalamika kalogwa,muulize unanunua wapi viazi anakwambia ananunua mabibo sokoni au soko kuu,gunia linauzwa sokoni 100,000 tena hapo limeshapunguzwa punguzwa ndipo mnauziwa laki,wakati ujazo wagunia hilo la laki yawe magunia matatu ndio gunia 1 kwa mkulima shambani na shambani gunia mkulima anauza 80,000, lakini kutokana na uvivu wetu wakusubiri mpaka tuletewe sokoni ndio tufate viazi tunaenda nunua mtoto wa gunia kwa 100,000,hivi unategemea faida utaipatia au iona wapi?

Uwezo wa kwenda shambani unao kama unaweza fata gunia sokoni unashndwa nn kufata gunia kwa mkulima wa viazi shambani,ila upo unasubiri Middle man akuletee,sawa kaaa hapo subiri uletewe utalikuta sokoni.

BIASHARA YA GENGE
Mtu ananunua karoti sokoni,hoho sokoni hajiulizi hizi hoho/karoti zinatoka wapi,kwann mimi nisizifate huko zinakotoka? anasubiri karoti auziwe moja 300 wakati akienda shambani mkulima anamuuzia Ndoo ya lita kumi sh.3000,hivi ndoo ya lita kumi mpaka ijae ina karoti ngapi ndani? Lakini yeye anasubri aletewe pale soko kuu akanunue 500 aje atupge mtaani karoti sh 700 atuambie karoti saivi ni BEI kumbe n uzembe wake na uvivu wake. Ukigusa Limao gengeni saivi unaweza ambiwa ni buku ila muulize huyo muuza genge katoa wapi hilo limao atakwambia soko kuu.

BIASHARA YA GESI na VIFAA VYAKE
Upo ofisini unauza gesi zikikuishia unavuta simu unapga unaletewa na kampuni hadi mlangoni,hivi umeshawahi jiliza what if nikifata mwenyewe hizi gesi ntauziwa kiasi gani? niwambie tu wauza gesi fateni gesi wenyewe huko zinapojazwa,Mtanishukuru badae kwa bei mtakayoikuta.

Unauza burner/Stand/Regulator/Pipe hivi vifaa umewahi kujua vinatengenezewa wapi? jiulize kisha vifate kutoka kwa mtengenezaji mkwepe middle man yule unaempgia simu akuletee vifaa kila vikiisha utaona bei utayoikuta.

MAMA NTILIE
Tukiachana na hawa wanaokopa vitu kwa mangi then wanalipa jioni,nawaongelea nyie mnaonunua mchele kwa cash mnauziwa kilo ya mchele 2500 hivi umeshaenda kahama huko au magugu au mbeye mchele unakotoka ukajua bei ya huo mchele unaouziwa kilo 2500,ni kwamba hiyo bei unapigwa mruke huyo middle man uone matunda ya ujasiriamali wako.

Tuache uvivu ndugu zangu tusisubiri kuletewa kisha ndio tukanunue,wanaofata mizigo china sio kwamba wao n maboss sana au wanapenda sifa hao wote wameshaona madhara ya middle man,kama unafanya biashara yoyote usipende mambo ya Free delivery sijui toa oda tunakuletea usipende hizo ofa ndio zinapunguza faida yako na mwisho unaona hupati faida kumbe unapata,Middle man ndio anaekufanya wewe ujione kama hela yako inapotea hujui inakoenda.

Kabla hujafunga au kubadlisha biashara unayofanya hebu mkwepe middle man halafu fata mzigo production center halafu tuone kama ndani ya mwezi huu mawazo ya kufunga hyo biashara kama yataendelea kuwepo.

Faida ya mauzo yako inapotezwa na huyo middle man ndie anaekupa loss wala sio kwamba una matumizi makubwa au nni TUACHE UVIVU vyakuletewa vina gharama.

Heri ya Mwaka Mpya.
🤣 🤣 🤣
 
Usiende China ila vile vile usiende Kariakoo , hebu nenda kajaribu Zenji kuna sehem wanaita Mtendeni ,vifaa vya Electronik bei ni kama bure.
wengine ndo tunakoshinda uko kwote kwa msudan mchina akuna sehem nisiyoijua ila sio rahic kama mnvyofikiria kumbuka kuna nauli na usafirishaji kwa mizigo mikubwa km friji,tv,desktop upiti kizembe bandalini othewise ubebe kitu kimoja au viwili vya mkononi na hata ivyo ukienda uko zanzbari vitu vingine avina tofauti bei na uku ila km mwenyeji ndo utafaidi vinginevyo utaona ushenzi tu mana tra
 
Mkuu CONTROLA,

Umeandika vyema sana, umetoa darasa na ushauri mzuri kwa walio kwenye field na wanaotafakari mambo kwa kina.
Nakuunga mkono 100%

Sitaki kuwakosoa waliokukosoa wala siwashangai wanaokubeza kwasababu wametumia haki na uhuru wao wa maoni.

Binafsi ni mnufaika mkubwa sana wa ulichokisema (kuondoa middle men)
kwenye biashara.

Siku chache zilizopita kuna mdau alileta uzi humu jukwaani akiuliza namna ya kuwa argent wa kuagiza simu China.
Alitoa bei ambazo kwasasa anuziwa simu huko aliko
Nilipoangalia kwa haraka nikagundua huyu anapigwa kwasababu ameshindwa kuwaondoa/kuwapunguza middle men kwenye biashara yake kwani bei anauziwa ni kubwa ukilinganisha na uhalisia wa soko hivyo nikamshauri apunguze kwanza middle men ili apate faida na uzoefu.
Hivyo viwili vitamsogeza sana kwenye u argent anaoutaka.
Vivyo hivyo huku mtaani tunakofanya biashara kuna watu nimewakuta kwenye b'ness, wana mtaji mkubwa kuliko mimi, lakini wanapigwa kwa kununua mizigo kwa middle men na wanafanya hivyo miaka nenda rudi wakati mimi na kamtaji kangu kadogo nikisafiri 1 week...

Kwanza, Najua soko linavyokwenda na mabadiliko yote (hunidanganyi)

Pili, Napata mzigo kwa bei nzuri kwa argent moja kwa moja hata nikishindwa kununua mzigo fulani kwasababu ya bei naongea na jamaa zangu tunachanga tunachukua mzigo
Hii inaturahisishia pia hata kwenye gharama za usafiri kwani tunashare au wakati mwingine wanalipa wao.

Tatu, ninatoka sokoni nikiwa nimetengeneza connection mpya ya muda wote ambao sitaweza kuja sokoni ili nipate update za kila siku achilia mbali kufahamiana na wafanyabiashara (maboss) ili kesho na keshokutwa nipate mzigo kwa credit sio kila wakati nitakuwa na cash.

Nne, Napata uwezo wa kupunguza bei ya bidhaa zangu na kuvutia wateja kwani biashara ni ushindani
Na kama hauna mtaji mkubwa, basi uwe na akili kubwa kibiashara atleast tengeneza connection mpya siku, wiki, mwezi au mwaka.Kuwa tofauti, sio anapoagiza Juma nawewe lazima uagize hapo hapo hii dunia ni pana.

Tano, inanipa uwezo wa kufanya uchaguzi nini kipya niongeze au nipunguze kwenye biashara yangu
Ni rahisi kufanya hivyo ukiwa mwenyewe sokoni kwakuwa unaviona kwa macho

Nadhani mtoa mada alichomaanisha hasa ni kuondoa middle men kwenye biashara
Sio lazima wote kwenda kiwandani lakini kwa nafasi yako unaweza hata ku share na mtu hata kuagiza mchele Mbeya

Naona magari ya dagaa kutoka Mwanza watu wanashare hata wanne vivyo hivyo kwenye samaki, mkaa nk.
Nadhani tuna dhana potofu kwamba wanaosafirisha bidhaa wana pesa nyingi sana sio kweli hata wenye magenge mnaweza mkachanga mkanunua mikungu ya ndizi Moshi.
Kuna mtu kila wakati huniambia napoteza fedha nyingi kwenda sokoni kila mara lakini mimi huwa na cheeeka tu
Ni kweli natumia fedha lakini nahakikisha imeleta manufaa/mapinduzi kwenye biashara yangu.

Alamsik!!
 
Back
Top Bottom