Ongeza faida kwenye biashara yako kwa kumkwepa middle man

Nina siku sijakusoma Mkuu na Leo imebidi nikutafute nikakutana na Bandiko lako. Asante sana kwa somo hili kwangu nitaliita zuri Maana nimeliishi
Kaka wakati naanza Biashara yangu ya Chupi nilikwenda sokoni nikauziwa Kila dozen moja 36000/=, ilinilazimu Kukomaa na bei ya 5000/pc

Lakini baada ya kuizoea na kuyajua masoko bidhaa ileile nikaanza kuipata chini ya 36000 hapo ikanirahisishia namna ya kuuza maana napata Faida.

Haikutosha now natafuta huko wanakotoa wao ni wapi na wanafanyaje Nataka nifike huko hawa middle man wapo waendelee kuwepo ila ukipata namna ya kumkimbia mkimbie haraka sana.

Hata huko China middle man wapo wengi nataka kuwakwepa pia. NASHUKURU MUNGU Kwa mtaji huu mdogo now naweza kuagiza Mzigo China unakuja namuomba Mungu mwaka huu ukiisha mwakani NAKWENDA MWENYEWE CHINA 😋
 

Mkuu maujanja kidogo unaagizaje mzigo kutoka china [emoji630] kwamtaji mdogo
 
Umesomeka sana middle men hawa usipo fanikiwa kuwakwepa kwenye biashara itachukua mda sana kutoba . Coz kuna hela nyingi sana ambayo inabidi ije kwako inapigwa pini na wao
 
Kokudo ni 1 ya watu wachache sana wanaoelewa masomo ninayo yatoa,yani kama ni mwanafunzi niaejivunia darasani hata nikifundisha kitu wengine waseme hawajaelewa ntawambia wote ambao hawajaelewa wamfate "kokudo" awaeleweshe.

sina shaka na utendaji wako,sina mashaka na wewe ktk biashara,nakuona mbali sana sana kuliko unavyoweza kufikir kuna vitu nasoma unapokua unachangia thread zangu napata majibu "yes huyu kweli ni msaka pesa ninaemtaka".

Endeleza hiyo spirit usipoe hata kidogo, acha hawa wasiojua Middle Man anawaumiza kwa kiasi gani waendeleee kulia biashara mbaya biashara mbovu,waache wao walie muda wakijitambua walipokua wanakosea itakua too late.

kuna watu utajiri wataushika wakiwa na 40's au 50's mimi nawaangalia tu wanavyo complicate mambo ktk thread ninazozitoa,waache wafanye biashara wasijiongeze.Sitochoka andika Thread zakuinua wengine na kuwasaidia wengine,ndio malengo yangu Kila mtu afaidike na uwepo wangu duniani,wanao ona naandika vitu haviwezekani nakaaga kimyaa natulia.

Kokudo Big Up,usichoke kujifunza kila iitwapo leo biashara ina mbinu tofauti tofauti ji update kila unapopata nafasi either kwa kusoma au kupga story na wafanyabiashara waliokuzidi wewe siku 1 utakua Mafia ktk dunia ya ujasiriamali na Biashara kwa ujumla wake.
 
Wachache sana watakuelewa mkuu, binafsi nimepata kitu hapo achana na wanaokosoa kwa facts za kijinga.
Sijibu hata siku 1 watu wanaopinga ninachokiandika ambacho nina uhakika nacho kwa 100%,

nawaacha wapinge/wakosoe/nk na wengi wao si wafanyabiashara maana hakuna mfanyabiashara

asiejua "hasara" ya kununua bidhaa kwa middle man,hawa wengine complicators acha niwasome tu,inatoosha.
 
Binafsi ni mnufaika mkubwa sana wa ulichokisema (kuondoa middle men)
kwenye biashara.
Zillion ktk watu walioelewa hili somo ukimtoa kokudo wewe umenielewa kwa asilimia 100

yani kuna watu mnaelewa mambo ktk namna natamani watu waelewe,ila ndio hivyo vichwa tumetofautiana

safi sana naamini wewe ni 1 ya watu hatari sana ktk biashara,Si rahisi kuelewa thread zangu kama mtu huna moyo na "biashara"

ni wale wafanyabiashara walio serious tu ndio nadhani tunaenda sawa,hawa wengine kama ulivyosema acha watimize haki yao kikatiba ya kutoa maoni.
 
Hili bandiko halikua la kila mtu.


Asanteni sana.
Asante kwa kunisaida,kuna watu ni wadandia magari wakidhani kila gari linaenda anapoenda yeye

sio kila thread ina muhusu kia mtu humu JF mbona hawa wakosoaji huwaoni kwenye jukwaa la SIASA

Huwaoni Jukwaa la sheria,huwaoni The Palace,nk kuna majukwaa huwezi wakuta kwasababu wanajijua hawa FIT

watu wanamna hiii unawakuta kule MMU ile ndio mitaaa yao,JUKWAA LA BIASHARA si kila mtu ni lake,thread zingine

ni aBove their THINKING CAPACITY, muda si mrefu ntashusha hint za kwanini Kampuni ZINAKUFA au HAZIPATI FAIDA nione

watachangia nini na vichwa vyao vyepesi,hawa ni waparamia thread wakidhani ni rahisi tu kuchangia changia kila thread.
 
ukishusha ni tag
 
Uko Sawa ndugu.....unachosema...mfano, nilienda kariakoo nikauliza Viti vidogo vya nussery nilikuwa nataka Viti 40 ,wakaniambia bei kama ifuatavyo. Mmachinga anasema anauza 6500-6000, nikaenda wanapouza jumla wanasema wanauza 5000 @ kimoja, huyu ni middle man, nikafunga Safar Hadi kiwandani, nikakuta wanauza kiti kile kile kinauzwa 4300. So piga hesabu nikimtoa middle man nitakuwa nimesave 1300, kwa kila kiti. Nawasalimu kwa jina la jamhur ya muungano.
 
Mambo ya mtu wa kati 🤣😂
 
Thanks for your acknowledge wewe wajua umenikamata kinoma noma na hua nachukua lile ninalohisi litanisogeza sehemu. Na hakika ninafaidika Sana na wewe pengine kuliko unavyojifaidi
 
Napokea hii baraka au maoni kwa imani kubwa mkuu Asante kwa sababu angalau unapokua unaandika Bandiko akilini mwako Unanikumbuka mwanafunzi wako. Nami nakuahidi nitakua mtiifu ninae kaa KITI cha mbele darasani kwako. Barikiwa sana mkuu naamini siku moja utakuja kumtembelea mwanafunzi wako
 
Ni sahihi kabisa Mkuu hata kama ni shilingi mia mbili ukiweza kuikwepa Fanya hivyo faster
Umesomeka sana middle men hawa usipo fanikiwa kuwakwepa kwenye biashara itachukua mda sana kutoba . Coz kuna hela nyingi sana ambayo inabidi ije kwako inapigwa pini na wao
 
Nikupongeze kwa kuandika mambo mengi lakini ujaiumiza akili yako sana kuwaza nje ya bosi naona kesho unaweza ukaja hapa na uzi unaosema Walaji pia waache kununua vitu wadukani waende kwa manufacture

Kisicho kwepeka ni kwamba biashara ni cheni na cheni hii inajumuisha segment kuu tatu za wafanyabiashara na kinacho watofautisha hawa watu ni mitaji yao sana sana, mtu wa kwanza kutoka kwa mzalishaji ni Wakala(agents) hawa ni wafanyabiashara wakubwa na wenye rasilimali wezeshi za kutosha niwanunuzi wakubwa wa mzalishaji na mara nyingi au wazalishaji wengi wanawauzia hapa watu tu wew mlaji uwezi kupata huduma moja kwa moja kwa mzalishaji, na hii ndio sababu ya kwanza kwann tunasema biashara ni cheni

Mtu wa pili ni muuzaji wa jumla (retailers)
Hawa ni wafanya biashara wenye mitaji mikubwa kuwafwatia hao wa hapo juu na ni wateja wa maagenti na wananunua biashara zao kwao kwa ujazo mkubwa kulingana na taratibu za agenti mfano mzuri ni biashara ya cement wewe muuzaji wa rejareja uwezi kwenda kununua kiwandani lazima ukanunue kwa muuzaji wa jumla

Mtu wa tatu ni muuzaji wa rejareja
Hapa ndio tuna mzungumzia mangi muuza genge,muuza chips na muuza duka huyu kwanza mtaji wake ni mdogo na mara nyingi yupo limited kwa vitu vingi na sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…