engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,149
- 1,441
Ndugu Wakulima wenzangu, habari za majukumu
Moja ya tatizo kubwa linalopunguza uzalishaji wa mazao kwa wakulima wetu ni matumizi ya Ardhi yenye alkali kubwa kupita kiasi. Hapa namaanisha utakapopima udongo wako na kukuta pH yake ni zaidi ya 7 elewa kuwa huo udongo ni wa alkali na pH huenda hadi kufikia zaidi ya 10.
Udongo wenye sifa hii huwa na matatizo ya kutoshikilia virutubisho hususani wakati wa mvua au wakati wa kumwagilia na chumvi huwa ni nyingi na hii husababisha udongo kupoteza rutuba na kupunguza uzalishaji.
Zipo njia mbali mbali za kupunguza pH na chumvi, baadhi ya njia hizo ni gharama kwa wakulima wetu.
Kwa sasa tunafanya utafiti ili kuweza kutumia njia rahisi na zenye gharama nafuu kwa wakulima wetu. Moja ya hizo njia ni matumizi ya mkaa, gypsum, vinyesi vya wanyama n.k
Kwa sasa tumeweza kufanya utafiti kwa kutumia muunganiko wa Gypsum na EM, matokeo yameonekana ni mazuri na yanatia moyo.
Unaweza kupitia link hii hapa ili uweze kupata elimu zaidi.
Effect of effective microorganism and gypsum amendments on nutrient leaching, pH, electrical conductivity, and Okra growth parameters under coastal saline soil
Karibuni wadau, kwa maslahi mapana ya kilimo chetu.