KERO Ongezeko kubwa la ushuru wa kibali cha kusafisha mazao ya uvuvi, linatuumiza wafanyabiashara

KERO Ongezeko kubwa la ushuru wa kibali cha kusafisha mazao ya uvuvi, linatuumiza wafanyabiashara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunapaza sauti yetu kwa heshima kuhusu ongezeko kubwa la ushuru wa kibali cha kusafisha mazao ya uvuvi kutoka kilo 50 hadi kilo 75. Uamuzi huu umetuletea changamoto kubwa sana sisi wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi, hasa wafanyabiashara wadogo ambao tunahangaika kutafuta riziki.

Ongezeko hili linapunguza uwezo wetu wa kufanya biashara, linaongeza gharama kwa wavuvi na wafanyabiashara, na mwisho wake linaweza kuathiri hata bei ya samaki kwa wananchi.

Tunaomba serikali iingilie kati na kupitia upya suala hili ili kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na kulinda sekta ya uvuvi ambayo inatoa ajira na kuchangia maendeleo ya nchi.

Kwa sasa gharama hiyo imeongezeka hadi shilingi 75 kwa kilo moja, na juu ya hapo kuna ushuru wa halmashauri wa shilingi 100 kwa kilo moja. Hivyo jumla ya gharama inayotutoza kwa kilo moja inakuwa shilingi 175.

Kwa mfano, mfuko wenye uzito wa kilo 40 tunalipia takribani shilingi 7,000 kwa gharama hizi pekee. Hii ni mzigo mkubwa sana kwetu wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi, hasa wafanyabiashara wadogo ambao tunahangaika kutafuta riziki.

Tunaomba Serikali itazame upya ongezeko hili kwa sababu linaongeza gharama za biashara na linaweza kuathiri maisha yetu pamoja na upatikanaji wa samaki kwa wananchi.

Ni katika maeneo yote yanayozunguka Ziwa Victoria, hasa Mwanza na sehemu nyingine zinazofanya shughuli za uvuvi. Hiki ni kibali cha Wizara ya Uvuvi kinachotolewa kwa kutumia control number. Agizo hili la ongezeko kutoka shilingi 50 hadi 75 kwa kilo moja limeanza tarehe 15/07/2026.
 
Back
Top Bottom