Dini zinatupa mashaka sana badala ya kueneza upendo zinaeneza chuki, akifa Mkristo Muislam anafurahi and vice versa. Sasa kwanini tuendelee kuziamini? Upendo unaoenezwa na dini ni wa kinafiki, kiongozi wa dini atasimama kwenye jukwaa la wazi kutamka kama 'sisi sote tunamuabudu Mungu mmoja' wakati akiwa na waumini wake anatamka asiyeamini katika dini yetu ni mwana wa shetani si mwenzetu.
Wengi wetu tumefuata dini fulani kwa kurithi yani umekuta wazazi ni dini hiyo na wewe ukafuata mkumbo, hatuamini katika dini fulani sababu ya mazuri yake bali tumejikuta tumo tu, kisha tunafundishwa mazuri ya dini tunayoiamini na kufundishwa mabaya ya dini nyingine (chuki) na unapoambiwa mabaya ama kasoro za dini yako unakuwa mkali na kutafuta maandiko kwa namna yoyote kutafuta ushahidi hatakama maandiko hayo hayana hoja za msingi. Tumefundishwa kuamini
Binafsi naelekea kuacha huo utumwa wa kufuata vitabu vya hadithi za kale zilizoandikwa na watu wa mashariki ya kati, sema kutamka kwamba Mungu hayupo bado sijafikia huko maana kuna vitu vinaonyesha uwepo wake (creation)