Ongezeko la atheists( watu wasioamini uwepo wa Mungu)

Ongezeko la atheists( watu wasioamini uwepo wa Mungu)

Habari wana-JF,

Kumekuwa na uwepo mkumbwa wa atheist duniani, sasa unahisi nini kifanyike kuokoa ndugu zetu?

Na wapi tunapofeli? Na kama tukishindwa kukemea basi tuwachukie kwa moyo wote.

Tujitahidi kusaidia atheist wanapotea vibaya mno.

Yani kile kizazi cha kukakaririshwa ndio kinaishia hivyo! Miaka 50 ijayo hakutakuwa na kanisa wala msikiti vyote vitakuwa vishakufa kifo cha kawaida wakati unasubiri mwisho wa dunia ulioambiwa! Kizazi cha sasa hakipokei haya majambo ya kwamba dunia iliumbwa wakati wanaona kuna sayari mabilioni huko kwenye universe! Mapokeo ya wakoloni ya kutawalia dunia
 
Atheists wapo hata muanzilishi wake yupo , dini hailazimishwi kikubwa wasishambulie wenye dini ...Kama watashambulia basi naona matatizo makubwa .
 
Ninachoona mimi ni kwamba wanaoamini kwamba Mungu yupo ndio wanaongezeka huku wanaoamini katika dini wakipungua kwa kasi duniani kote.

Wengi leo wanaona dini kama biashara tu hivi kwa sababu watu wa dini wanakosa kabisa majibu ya maswali mengi yahusuyo dogma zao.
 
Kwani kua atheist kuna shida gani? Kunamuathiri vipi anaeamini kuna Miungu??
 
Kwani atheist wamekufanyaje , si wanaishi maisha Yao fresh tu bila kuvunja Sheria za nchi na za kibinadamu , au ww unataka wafate unachokiamini🤔 . Kwanza neno lenyew tu linaitwa Imani , kuamini na kutokuamini , ye amechagua kutokuamini we inakuhusu nini. Imani ni kuwa na uhakika Kwa vitu ambàvyo huna uhakika navyo , ko ww pia unavoamin Mungu yupo inaweza kuwa kweli au sio kwel
 
Dini zinatupa mashaka sana badala ya kueneza upendo zinaeneza chuki, akifa Mkristo Muislam anafurahi and vice versa. Sasa kwanini tuendelee kuziamini? Upendo unaoenezwa na dini ni wa kinafiki, kiongozi wa dini atasimama kwenye jukwaa la wazi kutamka kama 'sisi sote tunamuabudu Mungu mmoja' wakati akiwa na waumini wake anatamka asiyeamini katika dini yetu ni mwana wa shetani si mwenzetu.

Wengi wetu tumefuata dini fulani kwa kurithi yani umekuta wazazi ni dini hiyo na wewe ukafuata mkumbo, hatuamini katika dini fulani sababu ya mazuri yake bali tumejikuta tumo tu, kisha tunafundishwa mazuri ya dini tunayoiamini na kufundishwa mabaya ya dini nyingine (chuki) na unapoambiwa mabaya ama kasoro za dini yako unakuwa mkali na kutafuta maandiko kwa namna yoyote kutafuta ushahidi hatakama maandiko hayo hayana hoja za msingi. Tumefundishwa kuamini

Binafsi naelekea kuacha huo utumwa wa kufuata vitabu vya hadithi za kale zilizoandikwa na watu wa mashariki ya kati, sema kutamka kwamba Mungu hayupo bado sijafikia huko maana kuna vitu vinaonyesha uwepo wake (creation)
 
God is good, always....
 
Back
Top Bottom