SoC02 Ongezeko la bei za bidhaa ni chanzo cha wananchi kuishi kama watumwa

Stories of Change - 2022 Competition

Theorist Mosses

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
345
Reaction score
253
FB_IMG_16593999103814018.jpg

(Picha mtandoni)
Utangulizi
Ugumu wa maisha umesababisha ongezeko la umaskini hapa nchini. Wananchi wengi wamekosa mahitaji kwa sababu ya mapato yao kuwa madogo hali ambayo imewafanya wananchi kuishi kama watumwa wakitafuta angalau kidogo cha kutia mdomoni.

Wananchi wengi ndani ya sehemu mbalimbali wamekosa mahitaji yao ya msingi ili kujipatia angalau mlo mmoja kwaajili ya familia zao. Yote haya ni kwasababu ya kupanda kwa bei za bidhaa hapa nchini.

Mzunguko wa pesa hakuna na wananchi siyo kwamba hawafanyi kazi hapana ni kwa sababu ya kupanda kwa bei za bidhaa. Kuna baadhi ya wananchi wanaingiza shilingi elfu moja kwa siku kwenye kazi zao. Inamaana kwa kipato hicho wananchi hawawezi kumudu gharama za upandaji wa bei za bidhaa mbalimbali kitu ambacho kinawafanya wengi kufanya kazi kama watumwa ili angalau wapate kidogo mahitaji yao.

Ufafanuzi
Utumwa, ni hali ambayo mtu anafanya kitu ambacho hakiwezi kumletea mabadiliko au maendeleo na anafanya kwaajili ya watu wengine bila kupata mafanikio. Mtu anakuwa hapati faida za msingi anakuwa anawapa faida watu wengine wenye mamlaka ya juu sana ambao wanamtumia kumnyonya nguvu zake.

Maendeleo, ni hatua nzuri ambayo mtu anapitia baada ya kufanya kitu ambacho kitamsogeza kutoka hatua moja kwenda nyengine ili kumletea mabadiliko na kumnufaisha pamoja na mafanikio. Mtu anakuwa huru kufanya kitu ambacho ni cha msingi na anafanya kwaajili yake mwenyewe bila kutumikishwa na watu wengine.

Naomba tuzungumzie kuhusu upandaji wa bei za bidhaa na jinsi wananchi wanavyo tumikishwa na kurudishwa nyuma kimaendeleo. Alafu nitashauri kwamba nini kifanyike ili kupunguza bei za bidhaa pamoja na kupanda kwa gharama za maisha.

Upandaji wa bei za bidhaa
Tukizungumzia chanzo kimoja wapo kuhusu upandaji wa gharama za maisha hapa nchini ni lazima tutaje kipengele cha ongezeko la bei za bidhaa. Kwasababu ni kitu ambacho kinatugusa wananchi wote kwa ujumla kumbuka sisi ndiyo kiini cha maendeleo.

Sisi kama taifa tutakapo shindwa kumudu bei za bidhaa basi taifa letu lote litashindwa kufanya maamuzi sahihi na mabadiliko kwenye upande wa maendeleo. Lakini bei za bidhaa hapa nchini siyo rafiki kwa wananchi ni kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo kwa wananchi ambao ndiyo taifa la sasa.

Serikali inapo jaribu kuongeza bei za bidhaa kwa wananchi ni vyema bei na gharama zote ziendane na hali halisi ya wananchi. Kwasababu itakapo tokea wananchi wanalalamika kupanda kwa bei za bidhaa zilizo pangwa na serikali tunakuwa tuna yumbisha taifa zima kwenye suala la maendeleo.

Hatuwezi kusema tulifumbie macho suala hili kwa sababu linamadhara kwa viongozi wa kiserikali na Wananchi wote. Tunakosa maendeleo kwasababu tume jifunga wenyewe lakini ni muhimu kujifungua kwanza vifungo tulivyo jifunga ili tuweze kusonga mbele zaidi.

Hali ni mbaya sana kwenye taifa letu tumekuwa watu wa kuongea juu ya maendeleo lakini kwenye upande wa vitendo atuchukui hatua zilizo sahihi. Lakini bado tuna nafasi ya kuchukua hatua nzuri ili tujenge kwa pamoja taifa zuri na kupunguza gharama za bei kwenye bidhaa na vitu vyengine vingi ili wananchi wapate unafuu wa kulijenga taifa kwenye elimu, siasa, kilimo, uvuvi, sanaa na sayansi.

Mapendekezo na ushauri
• Serikali ishushe bei za bidhaa ili kupunguza gharama za maisha; Taifa kuwa na bei za juu kwenye bidhaa siyo ujanja utakao saidia kuchochea uchumi wa taifa letu. Upunguzaji wa bei za bidhaa hapa nchini ni hatua nzuri ya kulijenga taifa ili wananchi ambao ndiyo taifa wapewe nafasi ya kuondokana kwanza na umaskini. Baada ya hapo taifa litakuwa na watu wengi wenye maendeleo ni kitu ambacho kitasababisha mabadiliko chanya ya uchumi.

• Wafanya kazi waongezewe mishahara; Wafanya kazi pia ni wananchi ambao ni taifa. Siyo kwamba wafanyakazi wakipandishiwa mishahara watasababisha hasara kwa serikali hizo ni imani potofu. Wafanyakazi watakapo ongezewa mishara ni hatua nzuri ya wao kijikwamua kimaendeleo na kutumika kama chombo cha kujenga uchumi. Mishahara iongezwe kwa wafanyakazi ili wamudu kwenye ongezeko la bidhaa ndipo watumike kujenga taifa.

• Serikali itoe ajira kwa wananchi; Kutoa ajira siyo kuyumbisha uchumi wa taifa letu hayo ni mawazo hasi. Lakini kutoa ajira nikuongeza idadi nyingi nzuri ya wafanyakazi watakaoleta maendeleo na kuondoa idadi ya watu ambao hawana kazi wasio kuwa na mchango kwenye ujenzi wa nchi. Serikali itoe ajira ndipo taifa litakapo kuwa na wafanyakazi wengi zaidi itapelekea bei za bidhaa kushuka na taifa litaendelea kimaendeleo.

• Serikali itenge bajeti ya misaada kwa watoto yatima na walemavu; Kutenga bajeti kwa walemavu na watoto yatima siyo kupoteza pesa za serikali bure. Wale ni wananchi wenzetu pia ni vyema kuwe na bajeti kwa walemavu na watoto. kwasababu wanateseka sana kwenye upande wa kupanda kwa bei za bidhaa kuwe na bajeti yao kwaajili ya kujikwimua kwenye umaskini ndipo taifa litabalikiwa kwenye maendeleo.

• Serikali iwekeze kwenye viwanda; bidhaa nyingi ambazo tunatumia
zimekuwa zikitoka nje ya nchi kuja ndani ya taifa letu. Lakini tunatumia gharama kubwa kwenye ununuzi. Ni vyema sisi kama taifa kupitia kwa gharama ambazo tunazitumia kwenye ununuzi wa bidhaa tuzitumie kutengeneze bidhaa zetu wenyewe ambazo tutakuwa tunaingiza faida na fedha za kigeni. Kwa namna moja au nyengine viwanda vitakuwa vikichangia na kuchochea maendeleo pamoja na kupunguza wimbi la kupanda kwa gharama za maisha na ongezeko la bei za bidhaa.

Hitimisho
Ni matamanio yetu kuona taifa letu likisonga mbele kimaendeleo lakini tutengeneze kwanza mazingira ya kimaendeleo. Alafu tuweke kiwango kizuri ambacho wananchi watakimudu kwenye kila kitu ikiwemo na bei za bidhaa ili kupunguza kupanda kwa gharama za maisha. Tutakuwa tunajenga taifa imara na kamwe hatuto anguka kwenye nyanja zote.​
 
Upvote 5
Kwa wageni jinsi ya kunipigia kura gusa kimshale chini ya post "^"
 
View attachment 2311591

nimekupigia kura
 
Back
Top Bottom