Ongezeko la bei za bima za magari kuanzia July

hii kitu italeta ulaji mkubwa sana kwa traffic hadi sasa ile motor vehicle licence wengi hawalipi hii ya bima ndo kabisaa hawatalipa na wengi watanunua feki na kubandika wajipange upya tu na bei au la tugomee tupaki magari yetu wataishi kwa bima za daladala???
 

kwenye mahesabu yako umepiga cost za comprehensive maana gari unalipwa after accident ila umechukulia mteja kalipa third party. gari ya milioni 14 ukiweka comprehensive ni laki saba (5% ya thamani ya gari) so revise your assumptions and calculations.
 

Mkuu kwanza ungejitambulisha tujue tunaongea na nnani, kwa maana unaongea kama unahusika moja kwa moja. Btw, BIMA ni biashara kama biashara zingine, nina imani kabla mtu au kampuni haijaamua kuwekeza katika biashara ya BIMA wanafanya ukokotozi na research za kutosha kuthibitisha kuwa biashara itawalipa. Na kama kiwango cha elf60 kilikuwa kinawalipa, nini kimetokea na kupelekea ongezeko la karibia asilimia mia4? Tuanzie hapo mkuu, hizo porojo zingine zitajadilika kwa ufasaha zaidi.
 
Huu ni wizi kama wizi mwingine tu,mimi nilikuwa na bima ya maisha na nika withdraw mwaka 1999,hadi leo hawajanilipa hela yangu hadi shirika la bima limekufa,watu wanakata bima sababu ni sheria lakini tofauti na comprhensive ambayo unaweza kufidiwa gari in case of an accident bima nyingine ni wizi mtupu.Ni sawa sawa na TRA sasa hivi ukienda kulipia road licence wanakukata hela ya fire extinguisher lakini hakuna fire extinguisher wanayokupa wala wanayo service,ifikia wakati wizi wa aina hii wabunge wetu waupigie kelele.Badala ya kukusanya kodi kwenye migodi tunang'ania kumnyonya maskini kila kona.
 
mkuu sababu kubwa ni hasara na kupungua uwezo wa kulipa kutokana na madai kuwa mengi na makubwa...
madai yapo ya halali na uwongo lakini pia bima kuyathibitisha inakua ngumu kwani ajali fake ni nyingi mno....na trafic police ni wala rushwa wakubwa wanasaidia sana kudhoofika kwa makampuni ya bima...huwa wanaangika ripoti za uongo za kugushi
well sabanu kubwa ni hasara walizo pata katika kipindi cha miaka 3 iliyopita....zoezi hili lilikua lifanyike zamani lakini kulikua na mashauriano baina ya wadau mbali mbali wa bima..hatimae mwaka huu ndio imepita
tukubali kulipa....ila tujue haki zetu...tujue nini kimo katika bima tunayo chukua na pia fuata masharti yaliomo ndani ya mkataba wako...sheria zipo kama unastahiki utalipwa....
 
Mkuu hapo kwa red unajua maana yake?
kwa TZ bima hai-qualify kuwa kwenye category hiyo kwa sababu ni product inayolazimishwa na sheria kwamba kila kwenye gari akate bima! hakuna option nyingine kwa mtumiaji

huria ...kwa maana ya kwamba watu binafsi wameruhusiwa kufanya hio bishara..na serikali inatunga sheria kufatwa lakini wao wapo huru....katika mipango yao...hata NIC haingiliwi na serikali katika kupanga bei zake...
 

Watakomajeeeeee?????
 
landa muhimu kwanza ufahamu nini maana ya insurance then nitakusaidia..kuwa insurance sio kodi..
[h=1]What is insurance?[/h] Insurance is the main way for businesses and individuals to reduce the financial impact of a risk occurring.



au
A practice by which a company provides a guarantee of compensation for specified loss, damage, illness, or death in return for payment of small amount of fees called premium..
hivyo bima sio kodi au lazima....bima sio lazima...ulazima wake umewekwa kwenye magari..sio kwa ajili ya mwenye gari as such..bali kuweka kinga dhidi ya abiria,wapita njia na mali zawatu kama utaua , utagonga gari au mali mtu na kuharibu....hii inakusaidia wewe kuwalipa hawa...badala ya kulipa hasara hio ya kifo na hasara ulosababisha kutoka mfukoni mwako
ama kuhusu kuwa na bima na hukulipwa hio ni tatizo la NIC kama shirika la umma lilitumiwa vibaya hivyo likafilisika....
lakini nakuhakikishia tafuta broker mzuri akushauri...na hakika bima inasaidia na utalipwa...usikate bima za mitaani ..chagua broker anejulikana na mwenye uwezo....
 
huria ...kwa maana ya kwamba watu binafsi wameruhusiwa kufanya hio bishara..na serikali inatunga sheria kufatwa lakini wao wapo huru....katika mipango yao...hata NIC haingiliwi na serikali katika kupanga bei zake...

Ngoja nikuache manake huelewi concept yangu, na hutakaa uielewe unless umesomea mambo ya insurance na free market economy.
Tutabishana bure wakati mwenzagu unaongea from business point of view huku mimi naongelea fair play in the market.
 
Acha kujustify hizi mambo wewe bima wanakuambia wao watalipa 60,000..mim wananizungusha tangu mwezi wa 4..wanapiga tu danadana ooh cjui alie gonga gari yako itabidi achangie..etc etc..huwezi kujustify..policy ya bima ni kutolipa ndo mana wanaweka masharti magumu sijui report within 24 hrs..etc etc..!!!
 
Sasa kama hizo kampuni kadhaa ulizozitaja ziko ICU sasa si waungane watoe kampuni moja kubwa..point yako ya kusema huwezi kuruhusu kampuni 15 zifunge biashara..kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi..wewe unafikiri concept ya merging of companies inakuaje..tatizo kila mtu anafikiri anaweza kuanzisha kampuni ya bima wakati hawataki kuungana..kama huna hela za kutosha ungana na wengine..kama hutaki subiri kampuni hiyo ife kibudu..Via..merging of companies..kama walivyo fanya wazungu kwenye monopoly capitalism..unafikiri kitu kama AIG..ni kidogo au ni kaji kampuni tu kamtu mmoja eenhh....over..sio mnaleta porojo za kujustify..uongeze mzigo kwa watu ili uweze kusurvive..nigga..whaaaaaa...!!!!
 

Maelezo yako yanaweza yasiwe sahihi; muanzisha mada anazungumzia bima ile ya lazima "Third party" na si "Comprehensive" sasa naomba uniambie hayo madai yanalipwa na "Third party insurance premium" na yapi zaidi ya mishahara ya watu? crabat
 

tatizo ni industry nzima imekua ilipata loss kwa muda wa zaidi ya miaka 5.claim hazilipwi kwa wakati na shareholders wamekua wakiongeza pesa ili kulipa fidia.hata ukiunganisha makampuni yote kwa rates zinazo tumika sasa haiwezi ku survive.kwani si tulikua na kampuni moja tu ? ya NIC na iliingia hasara mpka leo haijiwezi....madai ni mengi zaidi ya billion 10 wanadaiwa na wadai mbali mbali....na NIC ni kampuni ilikua na monopoly ina vitega uchumi kibao but wao pia wapo mbele kutaka mabadiliko haya.....kwa hiyo hoja yako ya merge sio rahisi...hasara ya bima za gari ni kubwa sana kuliko income inayokusanywa.
 
kuna kitu mnatakiwa mujue ni kuwa bei za bima hazitokani na demand and supply forces but inatokana na factors nyingi .na premium zote zinapangwa kwa mujibu wa sharia...na matumizi ya makampuni haya yanawekwa kwa mujuibu wa sharia....na biashara hii inategemea support kutoka makampuni ya reinsurance....bila ya support ya kampuni hizi za reinsurance kampuni zetu haziwezi kuwepo .hivyo reinsurers hawawezi kukubali rates ndogo ambazo ni hasara tupu...lazima tuwe na strong insurance industry..ili tuweze kuprotect economy yetu .....soko dhaifu la bima litadumaza uchumi wetu... hakuna anayeweza kuchukua bima kwani huko bei zake hapa kama tupo picnic
 
Maelezo yako yanaweza yasiwe sahihi; muanzisha mada anazungumzia bima ile ya lazima "Third party" na si "Comprehensive" sasa naomba uniambie hayo madai yanalipwa na "Third party insurance premium" na yapi zaidi ya mishahara ya watu? crabat
na mfano wangu nazungumzia third party insurance ndio maana nikasena shs 60,000 kama premium na loss ya 10,000,000 jee hio 60,000 ilipwe na magari mangapi ndio ilipe claim moja tu!!!!
 
tatito ni pale unapopata ajali wanatumia muda mrefu sana kulipa mfano kuna kampuni moja ya bima ipo pale morogoro na samora ppf tower ghorofa ya sita ,duu yaani wanachukua mpaka miezi sita kulipa bajaji tu iliyopata ajali wanakera sana
 
Mkuzi kucheelewa kwako kulipwa basi unatikana na hasara kutokana na premium kuwa ndogo
Leo tukiweka bei mwafaka hakutokua na ucheleweshaji
Hiyo kampuni unayisema nni moja ya makampuni muflis kutokana na soko kuharibika kwa undercutting
Na hizi bima zimepanda zaidi kwenye trucks na tankers na wao ndo watu wanao leta madai mengi sana feki
Hawa wanajidai hawapati faida but wao ndio matajiri wakubwa na kila mtu anajua wanafaidika na biashara yao
Sasa iweje wapinge kuliwezesha soko lipanuke na kijiimarisha
Kwa nini .nao wasipandushe bei zao za transit cargo?

Ukiwambie watazua biashara itakwenda kenya lakini sasa mbona kenya premium zipo juu sana?
Ukweli gari za private hazikupanda sana
Dala dala pia zimepannda kidogo sana na mabasi ya mikoani rate hii ilikuwa inatumiwa na baadhi ya makampuni

Huwezi kujustfy kupata faida secta yako na kutojali secta ya wengine
Au kuona bima ni kama kodi au sio muhimu
katika kipindi cha miaka 50 bima za magari zimepanda mara 3 tu na zote ni kabla ya 1997
Baada ya liberazation 1998 bei ya third party kwa truck ilikua ni 20,000 kwa tani
Sasa utaona kuanzia 1998 mpaka sasa hakuna ongezeko la bima ila bei imekua ikipungua kutokana na kila kampuni inayoingia kupunguza bei ili kupata wateja
Hatimae soko limepata hasara kubwa
Sasa kinachofanyika ni kurehesha bei zilizokuwapo zamani
Na piaimekubaliwa kuwepo na nidhamu ya makampuni kuweza kuhudumia wateja uzuri
Lengo sio faida mbele kama ni faida kila mmoja angekataa kkutoa bima za magari
Tuwape nafasi ili tuwe na secta yenye nguvu ya bima
 
Kwa taarifa zilizonifikia ni kwamba rate mpya zimesitishwa kwa muda usiojulikana. Zaidi baadaye!
 

Suala la risk liko mikononi mwa mwenye mali, mtu wa bima halimuhusu. Third party ni compulsory hivyo tusilazimishe watu comprehensive.

Kama kukata bima ni salama, kwa nini magari ya serikali hayakati hiyo comprehensive?

Ngoja nitoe elimu kidogo. Unapokuwa na magari mengi yenye thamani kubwa, ni heri ukafanya kitu kinaitwa, 'captive insurance' yaani bima ya ndani (kwa tafsiri yangu) kuliko kulipia bima nje.

Mfano, chukulia una magari 30 yenye thamani ya TZS 40 milioni kila moja; hivyo TZS 1.2 billion kwa yote. Kwa bima ya asilimia 4 kwa mwaka ni sawa na TZS 48 milioni (zaidi ya kununua gari mojawapo jipya kila mwaka). Swali, je kila mwaka lazima gari lipate ajali kiasi cha kuteketea kabisa, yaani write-off? Inawezekana hata miaka mitano ikapita lisitokee lolote, bima wao wataendelea kuvuta tu!

Ndio maana makampuni makubwa yenye magari mengi na yenye ma CFO wa ukweli hawalipi comprehensive! Sio kwamba ni wajinga na wanapenda kupoteza bali wamepiga hesabu vizuri.

Wito: Watu wasilazimishwe comprehensive, waachwe wapime wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…