Ongezeko la deni Bodi ya Mikopo

Ongezeko la deni Bodi ya Mikopo

DoroBucci

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
253
Reaction score
190
Nafikiri hiki kitakuwa ni kitu kipwa kwa wengi ambao bado hawafika bodi hiyo kujua "LOAN STATUS" ya mikopo yao.Kuna kitu kinaitwa "PENALTY" na kingine kinaitwa "VALUE RETANTION FEE".

Kwa wale waliokwisha maliza,wanaweza kujikuta kuna deni limebakia liitwalo "VALUE RETANTION FEE".

Hakika sijajua ni kwa nini hiki kitu kimejitokeza wakati huu,kwani mkataba wa awali haukuwa na hiki kitu.Kwangu mimi ilikuwa nimalize deni mwezi wa tano mwaka huu,lakini kutokana na mabadiliko hayo nimejikuta naongezewa miaka miwili tena ya kumalizia deni hilo.

Mimi niwatake tu wale wote wanaoendelea kulipa na ambao wanatarajia kumaliza hivi karibuni wakafuatilie swala hili kwani kimsingi ni kama ongezeko la deni ambalo ni WIZI wa mchana kabisaaaaaa na uonevu mkubwa wa SERIKALI kupitia bodi ya mikopo.
 
mi nimekopa na silipi,elimu ni bure na serikali kunihudumia ni wajibu wake kama vile mzazi kumlea mtoto wake
 
Hata hiyo penalt tu, naona ni kiini macho kwa sababu mda wote sikua na ajira, nimepata ajira miaka miwili baada ya kuhitimu, nliposign mkataba tu nlisign na form yakuanza kulipa mkopo, weny penalt tayari. Imekaeje hapo wakuuu?
 
Sina uhakika na hilo swala lakn niliambiwa hata kama huna kazi inabidi utoe taarifa bodi ya mkopo ili wajue status yako, otherwise nafkri kila mda unapoenda na penalty inaongezeka gharama
 
hawa HESLB nawashangaa sana. yaan wanashindwa kuweka website yao kias kwamba mtu popote alipo anaweza kujua status ya deni lake? nimehangaika sana kwa hili lakn cjafanikiwa
 
Silipi hilo deni,wakitaka waniongezee mkopo wa kusoma Masters
 
hii ni nchi ya kicommunist?

Ya kijamaa ingawaje viongozi ni wanafiki,hawautekelezi mfumo huu kwa vitendo,wanatekeleza kwa maneno ,kuhudumia ndio msingi wa mfumo huu,so napractice ujamaa kwa vitendo na si kwa kuigiza,namuenzi Hayati Mwl.Nyerere Mkuu,au we unaonaje??
 
Back
Top Bottom