Ongezeko la huduma za kijamii kama biashara -haki inayotakiwa kuwekewa mipaka

Ongezeko la huduma za kijamii kama biashara -haki inayotakiwa kuwekewa mipaka

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Sasa ni rasmi kuwa nchi imeendelea na ustawi wa watu umeanza kuonekana.

Mwalimu Nyerere na Mzee wetu Karume wanaweza kuwa wanafuraha huko walipo miaka 61 ya Muungano Serikali zote zimejitahidi kuleta maendeleo.

Ikumbukwe kuwa wapo maadui watatu waliowahi kutangazwa miaka hiyo yaani ujinga ,maradhi na umasikini.
pia zipo huduma muhimu za kijamii ambazo zimekuwa kero za kudumu lakini zimebaki kama agenda za kitaifa na kisiasa ambazo bado inatupasa kuziweka sawa kwa muktadha wa haki na usawa.

Serikali ipongezwe kwa kuendelea kuwa kinara wa utoaji huduma muhimu kwa jamii lakini pia ipongezwe kwa kuendelea kuilea na kuikuza sekta binafsi ili iwe kisaidizi cha kufikia malengo na mahitaji ya huduma za kijamii.

Kwa sasa tunaona modality ya ushirikishwaji mkubwa wa private sector kama mdau muhimu.
ANGALIZO;

Tunapoendelea kuikuza sekta binafsi nchini ni muhimu kukumbuka bado kama serikali inao wajibu mkubwa na wa pekee wa kuhakikisha huduma za jamii zinaboreka na zinakuwa jumuishi na nafuu.

Sekta binafsi inaruhusiwa kujikuza au kukuzwa ipasavyo japo upo umuhimu wa kuiwekea hand break ....yaani mipaka hususani kwenye muktadha wa unafuu wa gharama za huduma.
Mfano matibabu ya figo,ugumba,urembeshaji mwili ,elimu n.k.

Ni vyema mamlaka husika kuja na bei elekezi la sivyo tutaigeuza huduma ya msingi kuwa ni anasa.

Tulifikirie na kuanza kulifanyia kazi jambo hili.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Back
Top Bottom