jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,530
- 9,550
Habari,
Naomba niende moja kwa moja kwa moja kwenye mada.
Zamani ilikuwa wakikutana vijana ambao wako balehe na kushiriki tendo basi asilimia kubwa ni ndani ya miezi kadhaa tu walishapeana mimba.
Lakini hali kwa sasa imekuwa tofauti mno kwani ukienda kwenye mahospitali dada zetu wanaotafuta watoto wamekuwa ni wengi mno na ukienda kwa hawa tiba mbadala like dr mwaka ndo unaweza kuchoka kwa idadi hyo ya tatizo la uzazi.
Zamani ilikuwa tatizo hili la ugumba ni kwa wanawake zaidi lakini kwa sasa hata wanaume wengi wamekuwa na tatizo hili la uzazi kiasi cha kwamba huduma za IVF zimesogezwa sana mikoa ya Dar na Arusha na wateja kila siku wanamiminika.
Swali langu kwa serikali ni kwamba athari hii ya ugumba kwa watanzania wanaiona/wanaiujua?
Na kwanini hawachukui hatua kutoa elimu na hata kuongeza nguvu kwenye hili suala? maana tusipokuwa makini tunaweza kuelekea kubaya
Mwisho endapo kama serikali inalitambua hili tatizo kwanini madawa ya kutoa na kuzuia mimba yanatolewa kiholela kwenye maduka ya madawa?
Watanzania wenzangu naomba mstuke endapo kama hutopata mtoto kipindi hiki jitahidi uwe na uzao wako kwani miaka 5 au 10 ijayo kumpata mwanaume/mwanamke mwenye 100% sawa ya afya ya uzazi itakuwa changamoto mno kama serikali haitoliingilia kati hili swala.
Mwisho
Hii ni fursa kwa wanafunzi kusomea masuala ya afya upande wa uzazi ili baadae wakifaulu wakibahatika kufungua hospitali zao hakika watapiga sana hela kwani kwa sasa wagonjwa ni wengi mno na ndani ya miaka 10 ijayo wateja watakuwa wengi zaidi.
Kwani kwa sasa wagonjwa wengi wanalifanya hili kama siri lakini wengi ni wagonjwa na wanalijua hilo so ndani ya mda huo hapatakuwa na siri tena.