KERO Ongezeko la mabanda ya playstation /video games tishio kwa watoto wetu, mamlaka zilitizame hili kuwanusuru

KERO Ongezeko la mabanda ya playstation /video games tishio kwa watoto wetu, mamlaka zilitizame hili kuwanusuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Mabanda ya kuchezesha video games kwa watoto yamezidi. Upi mpango wa Serikali kunusuru hiki kizazi?

images.jpeg
 
Serikali inajua kumlinda mtoto ni dhidi ya ukatili wa kijinsia hawajui vitu kama hivi huweza pelekea mtoto kuharibika kitabia hasa pale akikosa hela ya kulipia hizo huduma
 
Mbona mambo ya kawaida hayo mkuu mimi nimeanza kucheza games tokea nikiwa primary na mpaka sasa nacheza wala haijaleta madhara yoyote kwangu.
 
Sio kila kitu mamlaka... Vitu kama hivi ni jukumu la mzazi kumzuia mwanae... Huwezi kumwambia mtu afunge biashara yake kisa watoto wasiolelewa vizuri... Wamiliki wa playstations na kumbi za video wao pia wasaidie japo kuwazuia watoto kushiriki hiyo michezo na sio kuwaacha tu na kutanguliza mpunga... Ila hilo ni jukumu la mzazi...
 
Nimeanza kucheza playstation mwaka 2000 nikiwa darasa la kwanza mpaka leo na sijaharibikiwa ,acheni lawama waleeni watoto wenu katika misingi imara na msisingizie sababu za kuua biashara za watu
 
Mnashindwa ku control watoto wenu, mnataka kufunga biashara za watu. What next? Maduka ya pipi na ice cream yafungwe kwasababu watoto wanaoza meno?
Hapo sasa!! Yaani jukumu la wazazi eti serikali ndio ilibebe?!! Kwani kila mzazi akiamua kumkataza mtoto wake kwenda kwenye mabanda hayo, yatakuwepo?
 
Hizi ni biashara za ovyo, siyo kwa watoto tu, hata vijana na wengine wanaenda nayo mpaka utu uzima! Quite addictive! Ni vya kupiga marufuku! Hata watu wazima wanashinda kwenye hivyo vibanda badala ya kufikiria maendeleo. Vipigwe marufuku!
 
Hakuna shida kama zitakuwa zinafunguliwa kuanzia saa kumi jioni na weekend kuanzia asubuhi.
Watoto hela ya kula shule wanapewa asubuhi mkuu, wa tution wachache sana. Hii biashara ukifungua vumilia tu usumbufu wa serikali za mtaa na ulinzi shirikishi
 
Swala la Kuzuia hilo jambo ni kumkosea/kumnyima mtoto Furaha na uhuru sababu watoto wanazuiw kufanya vitu vingi mfano movie nyingi hawastahili kuangalia , Mfano kuna Huyu mwakatobe wa hapa Bongo Anatumia lugha chafu na watoto wanakalili . Me naona wawekewe muda maalum tu.
 
Habari,

Mabanda ya kuchezesha video games kwa watoto yamezidi. Upi mpango wa Serikali kunusuru hiki kizazi?

View attachment 3047032
Naitwa Martin Lukwandali,ni Mratibu mkuu wa chama cha maktaba za video,video games na mabanda ya video Tanzania.

Asante kwa alileta hoja hiyo,
Nikili wazi kwasasa kuna ongezeko kubwa sana la mabanda ya video games inchini,kwa mkoa wa Dar es salaam kwa takwimu 2021/2022 jumla ya mabanda 2770 na 16000+ kwa mikoa zaidi ya ishirini ambayo chama cha maktaba za video kiliwafikia wadau hao na kutoa elimu na miongozo mbalimbali kuusu uendeshaji wake pamoja na ufuatiliaji wa karibu sana,licha ya kuwa na changamoto nyingi sana ikiwemo Elimu ndogo ya waendeshaji mabanda hayo,

kumekuwa na ongezeko la games za ngono na hata cartoon zenye viashiria vya ushoga na baadhi ya hao wanaoendesha shughuri hizo au michezo hiyo kuwaonyesha watoto wadogo,pia watoto kukosa kwenda shule kuhifadhiwa kwenye mabanda hayo muda wa shule, na hata mabanda mengine yako mafichoni na wengine kuweka michezo hiyo chumbani inaleta changamoto kuitambua na hata baadhi ya watoto hufanyiwa ukatili na hata kupekekea mmomonyoko kwa ujumla.

Hivyo kama chama kina endelea kufanya uratibu wa karibu kwa wadau hao ili kuwatambua na kuwapa elimu wadau hao ili iwe rahisi kuepuka vitendo viovu.
Pia kama chama tumetoa elimu kwa eneo kubwa kwenye maeneo yao kunzia serikali za mitaa,kata na kuwafikia moja kwa moja kwenye maeneo yao walipo na kuwapa elimu jinsi ya uendeshaji wa michezo hiyo na usimamizi wake.
Hivyo kama kuna banda lina kiuka taratibu basi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

PIA SERIKALI ITILIE MKAZO HAPO KWANI WAHANGA WAKUBWA WA ENEO HILO NI WATOTO,NA WATOTO NDIO TAIFA LA KESHO.
HIVYO TUUNGANE KWA PAMOJA ILI KUTILIA MKAZO ENEO HILO ILI IWE RAHISIKUDHIBITI ATHARI INGEWEZA KUTOKEA.PIA KAMA MAENEO ULIPO KUNA UKIUKWAJI MKUBWA WA VIBANDA HIVYO UNAWEZA KUPIGA SIMU NAMBA HIZO ILI TUWEZE KUSHIRIKIANA KUTOA ELIMU NA KUCHUKUA HATUA ZA KISHERIA.

0767819305,0763200313,0713245013
 
Serikali inajua kumlinda mtoto ni dhidi ya ukatili wa kijinsia hawajui vitu kama hivi huweza pelekea mtoto kuharibika kitabia hasa pale akikosa hela ya kulipia hizo huduma
Nilomshangaza mchezesha game mmoja, mwanangu kaiba buku home kaenda kucheza alivyorudi nikamtaiti akasema nikamwambia twende, tulivyofika nikadai hela jamaa kakaza eti hela sitoi popote nenda nikamjibu popote siendi na hela utatoa, nilikaza hadi buku likarudi.
 
Back
Top Bottom