Habari,
Jamani huu ugonjwa wa kansa mbona unaongezeka kwa bongo? Miaka miwili nyuma rafiki yangu alipoteza wazazi wake 2 kwa ugonjwa huu baadae jirani akafariki. Na sasa kuna jirani yangu amegundulika na huu ugonjwa.
Swali: Je nawezaje kujikinga/kujilinda na huu ugonjwa , je kuna vyakula vinavyosababisha kansa? au kuna vyakula vya kuzuia kansa au kuna lifestyle flani ni adopt?
Jamani msaada tafadhali
Poleni sana kwa kupoteza jamaa.ugonjwa wa cancer unatokana na rapid changes(mutation) na kugawanyika cell kusiko kwa kawaida kwenye DNA.DNA ni plan master kwenye cell inayoelekeza cell jinsi ya kukua na kugawanyika.Makosa ya maelekezo yanapofanyika ndo yanakuja kusababisha cancer.Cancer huokea kutokana na rapid growth na cell kugawanyika,cells zinazodhibiti cells growth (tumour suppressor gene) zinapobaini kunaongezeko lisilo la kawaida huzuia zisiongezeke zaidi.Lakini inapotokea kuwa mutation imetokea kwenye t. suppressor zenyewe,, inafanya kushindwa kufanya kazi yake vizuri au kushindwa kabisa kuzuia ongezeko hilo,cells hizi ndo zinakuja kusababisha tumour.
Kuna mambo yanayo mweka mtu kuwa at risk kupata cancer kama,uvutaji sigara,excessive exposure kwenye mionzi ya jua,unywaji pombe kupindukia,magonjwa ya mara kwa mara ya zinaa(STD),familia kuwa na mgonjwa wa cancer upo uwezekano wa kuja kurithiwa.
swali kuwa je kuna vyakula vinavyosababisha cancer not proven but vyakula vya kukaanga na mafuta kwa wingi vinachangia.
Vyakula vinavyopunguza uwezekano wa kupata cancer ni kutumia mboga za majani kwa wingi na matunda kwa wingi.
life style.
kupunguza au kuacha uvutaji sigara,kupunguza unywaji kama sio kuacha,kufanya mazoezi maana watu wenye obesity wako at risk ya kupata cancer,kupunguza kuwa exposed na mionzi ya jua,
NB.kumbuka hayo ni mambo yatakusaidia kupunguza cancer si kuzuia.
Matibabu ya cancer hutegemea na stage maana kama imesambaa sehemu kubwa ya mwili inakuwa ni ngumu zaidi kuliko kuwahi mapema,HIVYO NI VEMA KUWA NA MEDICAL CHECK UP YA AFYA ZETU AT LEAST MARA MOJA KWA KWA MWAKA.
hata hivyo tiba hizo ni upasuaji kuondoa cancer cells,matibabu ya mionzi,chemotherapy.