Ongezeko la Mahusiano ya kingono yasiyo halali katika jamii zetu

verses fountain

Senior Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
155
Reaction score
195
Habari za wakati huu wana JF. Ni matumaini yangu kuna Uzima lakini pia kwa wale walio na matatizo ya kiafya naomba Mungu awatie Nguvu.

Leo nina topic ndefu kidogo lakini Nitajitahid kuigusia kwa ufupi na kwa leo nitaongelea point moja tu inayotuhusu wote hasahasa kwa sisi vijana.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la ghafla kwa miaka ya karibuni pia nadhani pia ni kwa sababu ya uwepo wa utandawazi kwa upande wa mawasiliano kama vile simu, kompyuta na njia zinginezo wimbi kubwa la mahusiano yasiyo halali ya kingono kwa vijana (nje ya ndoa relationships). kwa miaka ya nyuma vijana wengi hawakuwa wakijihusisha katika mahusiano holela ya kingono jambo ambalo linashuhudiwa pia na ongeezeko la magonjwa yanayopitishwa kingono kama HIV\AIDS, kaswende, kisonono etc. Hapa tunazungumzia mahusiano yanayohusisha mwanamke na mwanaume ambao hawajaoana.

Kwa upande mwingine mahusiano yaliyokuwa yamezoeleka zamani ni ya mwanaume\mwanamke.

Lakini kwa wakati huu (kama wakati wa sodoma na gomora) mahusiano ya jinsia moja pia yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na yakipigiwa makofi na kupata sapoti kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali kitu ambacho kimeongeza ugumu katika suala la kupinga mahusiano ya aina hizo kwani ni kinyume na imani za watu wengi kulingana na imani zao kiujumla. Ushoga na usagaji umekuwa kitu cha kawaida katika jamii zetu. Muvi, nyimbo na aina nyingi za viburudisho zimekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mahusiano hayo yakitumia maudhui hayo kumomonyoa maadili ya vijana wengi katika jamii zetu. Lingine tena ambalo ni janga juu ya janga jingine na jambo la kutisha pia ni ongezeko la watu wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile.

Wanawake wamegeukia wanawake wenzao na wanaume pia wamegeukia wanaume wenzao kupata kile ambacho kimsingi Muumba alikusudia kiwe ama kipatikane ndani ya ndoa ya mwanaume na mwanamke tu.

Inawezekana kwa sababu moja ama nyingine hali ya mtu kuwa shoga\msagaji inachangiwa na mazingira ya mhusika tangu utotoni,malezi ambayo kimsingi yana mchango mkubwa kumfanya mtu awe kama alivyo. hatukatai kwamba changamoto zipo hasa kwa watoto wa sasa hivi (Mungu atunusuru hiki kizazi) kwani hakuna ambacho hawakijui. Kupitia simu ,Tv wanapata maudhui ambayo kwa asilimia Fulani yanachangia wao kuingia katika mahusiano haya ya kingono na kujikuta katika hatari ya kifo KIROHO kwa kuwa kwanza ni dhambi ambayo inatutenga na Mungu. Na pili KIMWILI kwa sababu kuna magonjwa ya zinaa ambayo yana madhara makubwa kwa vijana kiafya.

Lakini wazazi wote wana jukumu la kuhakikisha watoto wao wanakua katika maadili mema kwa msingi wa dini\imani ili kuwaepusha na janga hili.

Mahusiano yote haya kwa ujumla yanaongoza mtu kutenda dhambi kwa nyingine nyingi zikiwemo kusema uongo,kuua (abortion/utoaji wa mimba) na yote hayo ni chukizo kwa Mungu.

KITABU CHA ZABURI 119:9 kinatupa Swali na Jibu hapo hapo.Andiko hili Linasema

“
Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.”

Sisi kama vijana tunahitaji kuzisafisha njia zetu kwa kila namna ili tubaki safi mbele za Mungu ili aweze kututumia vyema kulitukuza Jina Lake kuu.Kuna changamoto mbalimbali abazo zinatuzunguka lakini hatupaswi kukata tamaa hasa katika kufanya jambo jema na lenye kumpendeza Mungu.

Katika kitabu cha LUKA 15:7,10 Yesu Kristo kwa kutumia mifano miwili anaonyesha na kuthibitisha kwa kinywa chake kwamba Kuna furaha miongoni mwa Malaika Wa Mungu mtenda dhambi mmoja anapotubu dhambi zake kuliko wale wengi ambao hawana sababu ya kutubu.

Ndugu yangu leo ambaye kwa namna moja umeshiriki katika dhambi ya Uzinzi au uasherati kwa mawazo na kwa matendo ni furaha iliyoje kujua kwamba Yesu ametamka kwa mdomo wwake mwenyewe kwamba atafurahi yeye ,Malaika wote mbingunii, pamoja na Mungu ikiwa\endapo utatubu dhambi zako (zote, sio uzinzi tu) na kujitahidi kwa kadri zote kuishi maisha matakatifu ukimtegemea yeye .YESU KRISTO HAANGALII dhambi ulizofanya huko nyuma kama ulikuwa mzinzi, mwasherati, shoga, msagaji etc. Anachoangalia ni utayari wako,moyo wako kuomba TOBA kwa dhambi Ulizotenda na kujitahidi kuishi maisha safi na yenye Kumpendeza Mungu.

Hatupaswi kuwahukumu wanaofanya vitendo hivi kwani hakuna mwenye Haki ya kuhukumu zaidi ya Mungu.wote tumepungukiwa na utukufu wa Mungu na hakuna ambaye anaweza kusimama na akajipiga kifua kwamba hajawahi kutenda dhambi.

Tunaloweza kufanya kama watu wenye Imani kwa Mungu kwanza ni KUOMBA kwa Mungu awafungue pia ufahamu wote wanaohusika na vitendo vyoyote visivyo halali kingono.Awape uwezo na nguvu ya kushinda dhambi zinazotawala miili yao na fikra zao.

Pili kujitahidi katika kuwaeleza ukweli na kuusisitiza miongoni mwao kwani ni kupitia maonyo mtu anaweza kuokolewa na akaacha mazoea hayo ambayo ni dhambi mbele za Mungu.

NB:Not being perfect is not excuse for US to sin as we feel like it.Though God Almighty knows we aren’t perfect he doesn’t expect us to sit down and enjoy our sinful life as if nothing eVer happened. INSTEAD,He expects us to approach Him asking for Grace and mercy to triumph over our sins and Guide us to become OVERCOMERS of sins not Slaves to SIN (JOHN 8 34).
 
Vijana hawana mitaji Wala ajira ya mashambani Wala mjini, what do you expect? Waache wang'oneke ili waondoe stress!
hata wenye ajira zenye mishahara minono bado wanachepuka kwenye ndoa zao na ambao hajaoa wala kuolewa na wana maisha mazuri tu wanajihusisha na mahusiano ya kingono na watu ambao sio wake\waume zao
 
Kazi ngumu, biashara ngumu, vijana wanachomiliki ni smart fon tuu na huko kuna kila kitu wanachokitaka
 
hata wenye ajira zenye mishahara minono bado wanachepuka kwenye ndoa zao na ambao hajaoa wala kuolewa na wana maisha mazuri tu wanajihusisha na mahusiano ya kingono na watu ambao sio wake\waume zao
Dogo, relax! Hivi unajua kuwa kufanya ngono ni tiba? Just give yourself an exposure uone jinsi mataifa mengine wanawasaidia watu wao kupata huduma ya ngono baada ya kazi ngumu!

Uliwahi kujipuliza ni kwanini madanguro ya mafuta street yalikuwa pale ilipokuwa billicanas? Ili wale wafanyakazi wa kwenye maofisi ya umma na wizara zilizozunguka pale wapate kurefresh mind na kurejea Tena kazini!
 
Kazi ngumu, biashara ngumu, vijana wanachomiliki ni smart fon tuu na huko kuna kila kitu wanachokitaka
kuwa na smart fon sio sababu maana wapo walizonazo na wanazitumia kwa matumizi positive hata kama sio kwa kuingiza hela direct basi kwa skills zingine za kimaisha.ugumu wa maisha sawa unachangia lakini sio kwa kiasi hiko kwa sababu hata wenye maisha swafi wanaingia kwenye kundi hilohilo la uzinifu,uasherati,ushoga,usagaji etc
 
Dogo, relax! Hivi unajua kuwa kufanya ngono ni tiba? Just give yourself an exposure uone jinsi mataifa mengine wanawasaidia watu wao kupata huduma ya ngono baada ya kazi ngumu!..
sawa sijakataa then kama ni tiba kwa nini vijana hatutaki kupata tiba hiyo chini ya mpango wa Mungu kwa kuingia kwenye ndoa?
Inamake sense kuenjoy sex ndani ya ndoa than nje kwa sababu nyingi pia ikiwemo risks za kujihusisha kingono na mtu usiyemjua ni kubwa na sex ni ibada.
 
Kwa kwel kama ngono tukiweza kuikwepa daaah nahis tutakanyaga mbinguni wengi sana

Shida hizi nyege zikipanda unasahau kabisa kama n dhambi. Lkn pia dhambi imetengenezewa namna ya kuonekana kama maisha ya kawaida na kama huna mpenzi katika ujana unaonekana kama hujui dunia inaendaje vile.

Ee Mungu uturehemu sisi waja wako hii tamaa ya ngono ikae mbali nasi.
 
Afu wengine tunatamani sana ndoa ila vipato changamoto. Hela ya mahali hatuna na mahali yenyewe ukiambiwa unakata na tamaa unaona bora ule hawa kwa kuja leo kesho kuondoka.
 
Mimi biblia ilinichosha niliposoma ule mstari UKIVUNJA AMRI MOJA UMEVUNJA ZOTE
Hapa lazima wengi tuwe kuni tu haiepukiki
usichoke mkuu.anayeenda motoni sio kwamba hajafanya dhambi as ingekuwa hivyo bhas sidhani kama kuna mtu angepona.bali mtu anaenda motoni kwa sababu amefanya dhambi kwa kujua na hataki kutubu na hataki msaada wa Mungu aweze kuishinda dhambi na anaendelea kutenda ile dhambi bila hata kuomba toba kwa Mungu
 

Baba mtumishi nikujuze tu kuwa ngono haikunza kufanywa jana wala leo hivyo sio kwamba kuna ongezeko

Ungekuwepo kipindi hicho ambacho mpaka magharika yanatokea sijui ungesemaje
 
Afu wengine tunatamani sana ndoa ila vipato changamoto. Hela ya mahali hatuna na mahali yenyewe ukiambiwa unakata na tamaa unaona bora ule hawa kwa kuja leo kesho kuondoka.
ok mkuu nimekupata.kwenye swala la hela pia hyo changamoto ipo lakini nina imani wapo watu wenye uwezo wa kutumia hela zao kwenye vitu visivyo na msingi kama kubeti ilhali wakilalamika ugumu wa maisha.

kwa maana hyo naamini vijana kutoa hela ya mahari wapo wenye uwezo ila hawataki kwa sababu nyingi tu lakini kimsingi wengine wanakwepa majukumu au kutokuwa na mipango ya baadae na hao walio nao katika mahusiano.

kama kweli una malengo na mtu hautashindwa kupambania mpka upate hyo hela ya mahari otherwise utakuwa huna mpango naye wa yeye kuwa kwenye future yako.
 
Baba mtumishi nikujuze tu kuwa ngono haikunza kufanywa jana wala leo hivyo sio kwamba kuna ongezeko

Ungekuwepo kipindi hicho ambacho mpaka magharika yanatokea sijui ungesemaje
sijakataa as sex ilianzia pale edeni under God command kwamba zaeni mkaongezeke na mkaijaze dunia ila point yangu ni kwamba ile circle ya vitendo hivyo kuzidi kufanyika kwa kasi tena waziwazi ndiyo inayozungumziwa hapa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…