Ongezeko la Mahusiano ya kingono yasiyo halali katika jamii zetu

Ongezeko la Mahusiano ya kingono yasiyo halali katika jamii zetu

Kwa hio wewe hilo li olo lako unalifuga mpaka siku ukioa, usipo oa je? Ngono ni nature na ndio maana hata wanyama hufanya ili wazaliane.Jogoo mmoja inamiki tetea 10.
Sheria za dini zimewekwa miaka 2000 iliopita kabla ya hapo sheria gani zilifuatw na kwa nini sheria za dini zizilichelewa kuja?
Wakati unahoji jiulize mzazi wa ko alikupata mazingira gani?
 
Mleta mada ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama wanaozunguka wanajua kweli zingine. Dunia ya Leo dhambi imekuwa kitu cha kawaida mno na ndo kinachotupeleka kwenye moto. Hii truth ulioandika hapa watakaoikubali in 100 labda 5 tena kwa mbinde. Mungu atusaidie sisi binadamu wa Leo masikio yetu yafunguke tusikie habari njema na kurudi kwenye ufalme wa Mungu maana ni hatari. Alijiimbia Rose Muhando uzinzi na uasherati imekua ni kitu cha kushangiliwa....sad truth!!! Sijui itakuwaje???
 
kuwa na smart fon sio sababu maana wapo walizonazo na wanazitumia kwa matumizi positive hata kama sio kwa kuingiza hela direct basi kwa skills zingine za kimaisha.ugumu wa maisha sawa unachangia lakini sio kwa kiasi hiko kwa sababu hata wenye maisha swafi wanaingia kwenye kundi hilohilo la uzinifu,uasherati,ushoga,usagaji etc
Napinga kwa nguvu zote vitendo vya ushoga na usagaji lakini ngono ya kawaida faza kwa kweli hakuna namna tunapeleka moto tu kwa sababu ni wazi hata hizo story za biblia nyingi ni usanii tu rejea jitu kama masanja mkandamizaji kushika biblia na kudai linaweza kuokoa watu mara ooh sijui kuna manabii yani utapeli utapeli utapeli so bora kutumia maonyo ya itikadi zetu za kijamii juu ya madhara ya ngono hiyo habari ya dhambi ni ujinga tu ambao binafsi mawazoni mwangu nimefuta kabisa nachoangalia ni utu kwangu mm kufanya mapenzi sio dhambi so long ni mapenzi ya kawaida.
 
usichoke mkuu.anayeenda motoni sio kwamba hajafanya dhambi as ingekuwa hivyo bhas sidhani kama kuna mtu angepona.bali mtu anaenda motoni kwa sababu amefanya dhambi kwa kujua na hataki kutubu na hataki msaada wa Mungu aweze kuishinda dhambi na anaendelea kutenda ile dhambi bila hata kuomba toba kwa Mungu
Hamna moto bhn hizo story za sunday school nasisitiza hakuna moto tusidanganyane
 
Kwa hio wewe hilo li olo lako unalifuga mpaka siku ukioa, usipo oa je? Ngono ni nature na ndio maana hata wanyama hufanya ili wazaliane.Jogoo mmoja inamiki tetea 10.
Sheria za dini zimewekwa miaka 2000 iliopita kabla ya hapo sheria gani zilifuatw na kwa nini sheria za dini zizilichelewa kuja?
Wakati unahoji jiulize mzazi wa ko alikupata mazingira gani?
Mkuu muelekeze kwa lugha nzuri tu ukiwafwatilia kwa kina hawa jamaa utangundua ni matapeli huyu mtoa mada mwwnyw unaweza kuta kicheche tu mm nna ushahidi kuna jamaa alikula tunda kimasikhara kwa mchungaji wa kike nae kila siku huko fb utaona maandiko yake itoshe kusema kila mtu afanye yake dunia imebadilika hii
 
Hizi ni nyakati za mwisho hazina tofauti na nyakati za nuhu! Hivyo dhambi ya uzinzi inachukuliwa kama jambo la kawaida, mwenye kuipenda nafsi yake ataiangazmiza mwenye kuichukia ataiponya!!!
 
Mleta mada ukweli utabaki kuwa ukweli hata kama wanaozunguka wanajua kweli zingine. Dunia ya Leo dhambi imekuwa kitu cha kawaida mno na ndo kinachotupeleka kwenye moto. Hii truth ulioandika hapa watakaoikubali in 100 labda 5 tena kwa mbinde. Mungu atusaidie sisi binadamu wa Leo masikio yetu yafunguke tusikie habari njema na kurudi kwenye ufalme wa Mungu maana ni hatari. Alijiimbia Rose Muhando uzinzi na uasherati imekua ni kitu cha kushangiliwa....sad truth!!! Sijui itakuwaje???
sio kitu cha kwaida lakini kwa dunia ya sasa kinaonekana kama ni kawaida tena sana.Mapambanao sio ya kimwili tu bali pia yanahusisha roho.Bila msaada wa Mungu hatwezi mapambano hayo kamwe
 
Hizi ni nyakati za mwisho hazina tofauti na nyakati za nuhu! Hivyo dhambi ya uzinzi inachukuliwa kama jambo la kawaida, mwenye kuipenda nafsi yake ataiangazmiza mwenye kuichukia ataiponya!!!
kabisa mkuu maana hesabu tutatoa kwa Mungu mtu mmojammoja na malipo pia kila mtu kulingana na matendo yake
 
Mkuu muelekeze kwa lugha nzuri tu ukiwafwatilia kwa kina hawa jamaa utangundua ni matapeli huyu mtoa mada mwwnyw unaweza kuta kicheche tu mm nna ushahidi kuna jamaa alikula tunda kimasikhara kwa mchungaji wa kike nae kila siku huko fb utaona maandiko yake itoshe kusema kila mtu afanye yake dunia imebadil
Mkuu muelekeze kwa lugha nzuri tu ukiwafwatilia kwa kina hawa jamaa utangundua ni matapeli huyu mtoa mada mwwnyw unaweza kuta kicheche tu mm nna ushahidi kuna jamaa alikula tunda kimasikhara kwa mchungaji wa kike nae kila siku huko fb utaona maandiko yake itoshe kusema kila mtu afanye yake dunia imebadilika hii
sikatai wapo wanaofanya yote hayo na ni watumishi wa Mungu na kuna ambao wanajikwaa na kutubu na Mungu anawapokea kuwasamehe na kuwaongoza tena katika njia inayostahili kama mfalme daudi.
kuwa na ushahidi wa kicheche mmoja sio kwamba wote ni vicheche ndugu na mimi Mungu ndiye anajua kama mimi sio kicheche.
na Ninamshukuru Mungu kwa jinsi ameniepushia mbali mitego yote hiyo ya kuzini na nazidi kuomba anitie nguvu kwa pale ninapopungukiwa.
na point ya mwisho sio kila mtu afanye yake bali kila mtu afanye kulingana na Imani yake kwamba ipo siku ataulizwa kutoa hesabu ya matendo yake kama hatataka kuishi maisha ya utakatifu bhas akae akijua wazi uelekeo wake sio mbinguni na sehemu iliyobaki si nyingine bali ni motoni.
 
Kwa hio wewe hilo li olo lako unalifuga mpaka siku ukioa, usipo oa je? Ngono ni nature na ndio maana hata wanyama hufanya ili wazaliane.Jogoo mmoja inamiki tetea 10.
Sheria za dini zimewekwa miaka 2000 iliopita kabla ya hapo sheria gani zilifuatw na kwa nini sheria za dini zizilichelewa kuja?
Wakati unahoji jiulize mzazi wa ko alikupata mazingira gani
sijaanza kufuga mtu mkuu.
ngono ni sawa ni nature ambayo tumewekewa kuenjoy ndani ya mipaka ya ndoa.
mfano wa Jogoo ni mfano halisi lakini hauhusiani hapa kwa sababu binadamu tumepewa utashi tofauti na wanyama wa kufanya maamuzi baada ya kuyachambua na kuangalia yale yenye faida zaidi kwetu kiroho na kimwili.
wakati hazikuwepo hakukua na kitu cha kuhukumu lakini sasa kama kipo bahs hatuna budi kufuata vilivyopo kujipima kama tuko sahihi au sio na ndio maana katika biblia sikumbuki kitabulakini andiko linazungumzia kwamba sisi hatukujua dhambi kuwa ni dhambi kabla ya sheria bali baada ya sheria kuwepo.so kama tunayo miongozo inayotuongoza kwa sasa tusigeukie nyuma kuhoji kwamba kipindi haikuwepo tuliishije.
wazazi wangu walinipata baada ya kufanya sex,ndani ya ndoa.
 
Habari za wakati huu wana JF. Ni matumaini yangu kuna Uzima lakini pia kwa wale walio na matatizo ya kiafya naomba Mungu awatie Nguvu.

Leo nina topic ndefu kidogo lakini Nitajitahid kuigusia kwa ufupi na kwa leo nitaongelea point moja tu inayotuhusu wote hasahasa kwa sisi vijana.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la ghafla kwa miaka ya karibuni pia nadhani pia ni kwa sababu ya uwepo wa utandawazi kwa upande wa mawasiliano kama vile simu, kompyuta na njia zinginezo wimbi kubwa la mahusiano yasiyo halali ya kingono kwa vijana (nje ya ndoa relationships). kwa miaka ya nyuma vijana wengi hawakuwa wakijihusisha katika mahusiano holela ya kingono jambo ambalo linashuhudiwa pia na ongeezeko la magonjwa yanayopitishwa kingono kama HIV\AIDS, kaswende, kisonono etc. Hapa tunazungumzia mahusiano yanayohusisha mwanamke na mwanaume ambao hawajaoana.

Kwa upande mwingine mahusiano yaliyokuwa yamezoeleka zamani ni ya mwanaume\mwanamke.

Lakini kwa wakati huu (kama wakati wa sodoma na gomora) mahusiano ya jinsia moja pia yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na yakipigiwa makofi na kupata sapoti kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali kitu ambacho kimeongeza ugumu katika suala la kupinga mahusiano ya aina hizo kwani ni kinyume na imani za watu wengi kulingana na imani zao kiujumla. Ushoga na usagaji umekuwa kitu cha kawaida katika jamii zetu. Muvi, nyimbo na aina nyingi za viburudisho zimekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mahusiano hayo yakitumia maudhui hayo kumomonyoa maadili ya vijana wengi katika jamii zetu. Lingine tena ambalo ni janga juu ya janga jingine na jambo la kutisha pia ni ongezeko la watu wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile.

Wanawake wamegeukia wanawake wenzao na wanaume pia wamegeukia wanaume wenzao kupata kile ambacho kimsingi Muumba alikusudia kiwe ama kipatikane ndani ya ndoa ya mwanaume na mwanamke tu.

Inawezekana kwa sababu moja ama nyingine hali ya mtu kuwa shoga\msagaji inachangiwa na mazingira ya mhusika tangu utotoni,malezi ambayo kimsingi yana mchango mkubwa kumfanya mtu awe kama alivyo. hatukatai kwamba changamoto zipo hasa kwa watoto wa sasa hivi (Mungu atunusuru hiki kizazi) kwani hakuna ambacho hawakijui. Kupitia simu ,Tv wanapata maudhui ambayo kwa asilimia Fulani yanachangia wao kuingia katika mahusiano haya ya kingono na kujikuta katika hatari ya kifo KIROHO kwa kuwa kwanza ni dhambi ambayo inatutenga na Mungu. Na pili KIMWILI kwa sababu kuna magonjwa ya zinaa ambayo yana madhara makubwa kwa vijana kiafya.

Lakini wazazi wote wana jukumu la kuhakikisha watoto wao wanakua katika maadili mema kwa msingi wa dini\imani ili kuwaepusha na janga hili.

Mahusiano yote haya kwa ujumla yanaongoza mtu kutenda dhambi kwa nyingine nyingi zikiwemo kusema uongo,kuua (abortion/utoaji wa mimba) na yote hayo ni chukizo kwa Mungu.

KITABU CHA ZABURI 119:9 kinatupa Swali na Jibu hapo hapo.Andiko hili Linasema

“
Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.”

Sisi kama vijana tunahitaji kuzisafisha njia zetu kwa kila namna ili tubaki safi mbele za Mungu ili aweze kututumia vyema kulitukuza Jina Lake kuu.Kuna changamoto mbalimbali abazo zinatuzunguka lakini hatupaswi kukata tamaa hasa katika kufanya jambo jema na lenye kumpendeza Mungu.

Katika kitabu cha LUKA 15:7,10 Yesu Kristo kwa kutumia mifano miwili anaonyesha na kuthibitisha kwa kinywa chake kwamba Kuna furaha miongoni mwa Malaika Wa Mungu mtenda dhambi mmoja anapotubu dhambi zake kuliko wale wengi ambao hawana sababu ya kutubu.

Ndugu yangu leo ambaye kwa namna moja umeshiriki katika dhambi ya Uzinzi au uasherati kwa mawazo na kwa matendo ni furaha iliyoje kujua kwamba Yesu ametamka kwa mdomo wwake mwenyewe kwamba atafurahi yeye ,Malaika wote mbingunii, pamoja na Mungu ikiwa\endapo utatubu dhambi zako (zote, sio uzinzi tu) na kujitahidi kwa kadri zote kuishi maisha matakatifu ukimtegemea yeye .YESU KRISTO HAANGALII dhambi ulizofanya huko nyuma kama ulikuwa mzinzi, mwasherati, shoga, msagaji etc. Anachoangalia ni utayari wako,moyo wako kuomba TOBA kwa dhambi Ulizotenda na kujitahidi kuishi maisha safi na yenye Kumpendeza Mungu.

Hatupaswi kuwahukumu wanaofanya vitendo hivi kwani hakuna mwenye Haki ya kuhukumu zaidi ya Mungu.wote tumepungukiwa na utukufu wa Mungu na hakuna ambaye anaweza kusimama na akajipiga kifua kwamba hajawahi kutenda dhambi.

Tunaloweza kufanya kama watu wenye Imani kwa Mungu kwanza ni KUOMBA kwa Mungu awafungue pia ufahamu wote wanaohusika na vitendo vyoyote visivyo halali kingono.Awape uwezo na nguvu ya kushinda dhambi zinazotawala miili yao na fikra zao.

Pili kujitahidi katika kuwaeleza ukweli na kuusisitiza miongoni mwao kwani ni kupitia maonyo mtu anaweza kuokolewa na akaacha mazoea hayo ambayo ni dhambi mbele za Mungu.

NB:Not being perfect is not excuse for US to sin as we feel like it.Though God Almighty knows we aren’t perfect he doesn’t expect us to sit down and enjoy our sinful life as if nothing eVer happened. INSTEAD,He expects us to approach Him asking for Grace and mercy to triumph over our sins and Guide us to become OVERCOMERS of sins not Slaves to SIN (JOHN 8 34).

Jina lako mwenyewe lina utata[emoji23][emoji23][emoji23]afu unahubiri kweli ebu kabadili jina afu urudi tukusikilize
 
Sifanyi ngono zembe kwa sababu ya kulinda nguvu zngu za asli na uwezo wangu wa kumeditate tu bas, Ila hayo mambo ya Mungu kasema Ni dhambi Ni uongo mkubwa na kutishiana tu , na ndio maana nyege zpo angekuwa ataki asingeziweka mpka mtu aoe!!
 
Kwani mkuu ngono inapunguza nguvu za asili
 
Back
Top Bottom