Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Watu wana ingiza 150B,Tzs, nyumbani Mnafanya matangazo live!? Bank sasa Hivi mwendo wa kuchunguliana. Mtafanya watu warudie zama kuchimbia pesa. Pia tutawanuisha majirani zetu huku tukiua uchumi nyumbani.
 
Mkuu hii ni hatari, ngoja tujiandae kuzitunza ndani,

Ile ya.kisiwa.cha Guam sikuiamini kwanza nikaileta kwa wanajamvi maana watu wa Mambo hayo wapo kupitia majibu yao yamesaidia sana kujua mambo
Washauri basi we si uko karibu nao

Ova
 
Ninavyojua mimi japo sio nguli wa maswala haya ni kwamba,kiapo hutumika wakati ambapo vitambulisho unavyo sawa na ni halali kabisa lakini unakuta majina yanakuwa hayako sawa kwenye baadhi ya documents zako.

Mfano unaitwa Matayo Samwel kwenye vielelezo vingine ukasomeka Methew Samuel. Mara nyingi watu huwa tunasema tu kirahisi kuwa ni majina yale yale,hapo lazima utadaiwa kitambulisho. Na kuna kesi za aina mbali mbali hiyo ni moja tu ya mfanano.

Na kuhusu pesa inapoingia kuwa zaidi ya milioni 50,kibenki wakati unafungua akaunti kuna maswali wanakuuliza hata hilo la miamala ya kiasi gani unatarajia kwa mwezi huwa linaulizea,sasa wateja mara nyingi huwa tunatoa taarifa za uongo.

Mfano mtu unaweza kusema aah ni pesa kidogo tu kama milioni kumi mpaka ishirini. Mtu wa benki ana anfika kaka unavyoongea na wanaweka hivyo viwango kwenue system zao.

Sasa kukiwa na kiasi zaidi ya hapo kunakuwa na alert kwenye akaunti yako lazima benki wapate uthibitisho wa hivyo viwango kupanda.
 
Kwa mwendo huu itafika sehemu ukienda kuchukua Fedha hata milioni tatu tu ujaze fomu ya maombi wiki tatu kabla na uambatishe na mchanganuo wa matumizi wa fedha yote,

Kila leo unahubiri kuondoa urasimu wakati huo huo unaongeza urasmu zaidi ya ule uliokuwepo....!
 
Kenya inatuburuza hiii Hongera sana Kenya na ahsante maana sasa hivi tz tulindwa na kampuni ulinzi toka Kenya sabuni Kenya kiwi kenya
Zamani benki posta enzi zangu nilitoa pesa ikaibiwa ikabidi niende kumwona meneja! Benki ndiyo enjini ya uchumi plz waache urasimu
 
Watanzania walivyo wavivu watajenga ki room na kuzihifadhi hela zao humo majumbani mwao... Mwaka jana na mwaka huu hakuna mwekeza mpya aliye kuja kuwekeza Tanzania, hata wale matajiri wa nyumbani/Tanzania hamna hata mmoja anaepanua biashara zake tena....
 
Uzuri hapa hata "wajeda" nao wataguswa pamoja na watu wa chama chake.

Ni swala la muda tu kila mtu atamchoka na wote tutaongea lugha moja.
hau kila mtu na Lugha yake kama vile ilivyokuwa kwa Wajenzi wa mnara wa Babeli!! unaombwa ulete tofali unapeleka msumali😂😂😂.Ila Mungu atasikia kilio cha watu wake na ataleta mkombozi.
 
Benki zitakufa
Nani ahangaike kuweka pesa kwa masharti hayo utafikiri hela inaongezeka wakati kila siku ni makato tu,uende tena kwa wakili umlipe elfu 10
Watanzania wanaotumia huduma za kibenki hawazidi 30% baadala kuwahimiza angalau wafike hata 80% ndo kwanza tunawawekea masharti kibao
Hebu waende wilayani/Vijijini huko wawaulize watu kama wanawajua wanasheria/mawakili kama siyo kwenye redio tu
Zitabaki akaunti za makampuni/taasisi tu.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…