SoC02 Ongezeko la single mothers na athari zake katika jamii

SoC02 Ongezeko la single mothers na athari zake katika jamii

Stories of Change - 2022 Competition

rammbiro

New Member
Joined
Dec 14, 2018
Posts
3
Reaction score
1
ONGEZEKO LA SINGLE MOTHERS NA ATHARI ZAKE
BY : RASHID ABUNAYA
Email : rashidabunaya@gmail.com

Assalaam aleykum ndugu wana jamii,

Ni matumaini yangu mu buhery wa afya kwa wale mlio na shida za kiafya basi mwenyezi mungu awafanyie wepesi mpate kupona

Ndugu wana jamii, bila shaka ninyi nyote ni mashuhuda wa ongezeko la mabinti wenye watoto, wakiwa wanapambana mitaani, bila baba (yaani single mothers)

hili suala limenifanya nitafakali kwa makini na mwishowe nimekuja na mtiririko ufuatao kuhusu mstakabali wa maisha ya vijana na mabinti hawa wanaojulikana kama single mothers.

Kwa tafiti nlizozifanya nimegundua kua mabinti wengi wenye umri wa kati ya miaka 16-25, wana watoto ambapo baba zao wametokomea kusikojulikana, au wapo lakini hawana uwezo au mpango wa kuhudumia watoto wao, wala hawapo tayari kuanza maisha na mabinti waliozaa nao, suala ambalo linawafanya mabinti hao kuishi kwa wazazi wakiwa na watoto wao wote wanalelewa na bibi na babu zao (yaani wazazi wa binti)

Kwa wakati huo ukiwaona vijana ambao ndio waliosababisha kupatikana kwa watoto hao hali zao za maisha ni duni au kawaida, na bado hawajajipanga kuhusu kupata watoto na hivyo hawaoni umuhimu wowote wa kujali, walio wengi badooo ni wachele, hawana akili za maisha, wala hawana mustakabali wowote kuhusu wanawake waliowapa mimba wala watoto waliowazaa.

Kwa kadri siku zinavyoenda naona hili suala linazidi kuongezeka, na napata picha ya usoni kua itafika kipindi mabinti wengi watakua na watoto bila kujipanga, na vijana wengi watawazalisha mabinti lukuki bila kuwajali wala kuwahudumia suala ambalo litaleta changamoto kubwa sana za kimaisha katika jamii

Lakini sintofahamu inakuja pale tunapoona katika asili mia, basi asili 40 ya mabinti wanaopata ujauzito wanapata wakiwa masomoni, (vyuoni au shuleni) suala ambalo linawapelekea kusitisha masomo yao, hivyo kuharibu mustakabali wa maisha yao,

Naaaaam, yaweza kua mzizi wa haya yote unatokea kwenye neno UJANA, ni nini hiki? Ni pepo gani hili? Ama nakumbuka ya wahenga kua ujana ni maji ya moto (basi ukiyashika kwa pupa yatakuunguza, na utabaki na makovu kama alama ya kukukumbusha kua maisha ni kitendawili na kila mtu ana jawabu lake, nalo ni sahihi kwa kila mtu ijapokua hayafanani)

Leo hii vijana na mabinti wengi wamepaparikia katika ngono tena ni zembe, wakiamini kua tendo hudumisha mapenzi baina yao kumbe kuna athari kubwa sana, ambazo wao wanashindwa kuzijua kwa kua bado akili yao haijakomaa, wanatawaliwa na wanaendeshwa na tamaa za miili yao


MTAZAMO WANGU KATIKA SUALA HILI
Katika siku za usoni, idadi ya hawa single mothers itakua kubwa kupitiliza endapo kama hatua za dharula hazitatumika katika kutatua suala hili katika jamii zetu


ATHARI ZA KUONGEZEKA IDADI YA SINGLE MOTHERS
Kuongezeka kwa ndoa za utotoni, na mimba zisizotarajiwa kwa kua hakuna hatua madhubuti za kudhibiti suala hili

Kuongezeka kwa vifo vya uzazi kutokana na kushika mimba katika umri mdogo (maternal death)

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya single mothers itapelekea uwepo wa hali duni ya maisha itakayopelekea malezi duni kwa watoto hivyo kusababisha changamoto katika ukuaji wa watoto ambao ndio taifa la kesho

Tunatarajia utegemezi katika jamii zetu utakua mkubwa sana kutokana na hali duni ya kiuchumi na ukosefu wa elimu ambayo ingesaidia kujikwamua kimaisha, hivyo wazazi wetu watalemewa kwa kutulea sisi na watoto wetu.

Kuongezeka kwa watu wasio na elimu, hasa mabinti kwani, idadi yao kubwa wanakatisha masomo kutokana na mimba zisizo tarajiwa, hii itapelekea kua na watu wasio na akili mtambuka katika kutatua changamoto za kijamii

Kusambaa kwa magonjwa hasa ya zinaa, kwani vijana wengi sio waaminifu na wanakimbia majukumu bila kuchukuliwa hatua hivyo, inawapa fursa ya kutembea na wanawake kadri ya uwezo wao, tu kwa sababu hamna kikwazo kwao

Malezi duni kwa watoto hivyo kupelekea mmomonyoko wa maadili kwa watoto, tu kwasababu wamelala katika malezi ya upande mmoja

ANGALIZO
Kama jamii na sekta husika haswa serikali , itaamua kupuuzia au kukalia kimya suala hili basi uwezekano wa kukumbana na athari tajwa hapo juu ni mkubwa na utakuja kuleta changamoto nyingi sana ambazo zitapelekea mamlaka husika kuingia gharama katika kuzitatua.


UTATUZI
Nadhani ni wakati sasa wanaharakati za maendeleo ya jamii, na masuala yote yahusuyo jamii kuingilia kati hili suala, ili sauti ipazwe na vyombo husika viweze kulitazama suala hili kwa mapana kuona ni mbinu gani zitumike katika kuokoa jamii na kusaidia maendeleo katika jamii zetu..

By . RASHID ABUNAYA MHANGAMWERA MBIRO
EMAIL : rashidabunaya@gmail.com
 
Upvote 2
Uchumi...

Sent using Jamii Forums mobile kwa hapo zamani suala la uchumi lilikua ni sababu wa kutokea kwa hayo yote,.. ila kulingana na tafiti nilizozifanya kwa kipindi cha sasa, uchumi hauchangii sana katika tatizo tajwa katika makala, ila ni ulimbukeni na papara za vijana zinazosababishwa na tamaa za miili, huchangia asilimia nyingi sana katika kuongezeka idadi ya single mothers
 
Back
Top Bottom