Mkuu, nashukuru. Nimesoma bandiko uliloambatanisha. Hata tukiamua kukubaliana na fatality rate ya 0.03 aliyoitoa, na hata kama tungeipunguza ikafika 0.01, lakini kuna factor ya KASI ya usambaaji wa ugonjwa hajaiweka vizuri. Just week Russia wameripoti vifo around 1000/day vinavyotokana na COVID, na tuchukulie hivyo vifo 1000/day ndo hiyo hiyo fatality rate ya 0.03, je, in terms of numbers, no ugonjwa gani unaweza kuua watu wengi hivyo ndani ya nchi moja kwa siku? Kuhusu hidden agenda, mkuu hata mimi sijui. Ila nawaza tu, kati ya njia zote walizonazo, ambazo wangeweza kutumia kutimiza nia zao ovu, ni kwa nini wachague chanjo ya Corona? Wanatengeneza madawa tunayotumia, wanatengeneza mbegu za hybrid za nyanya na vitunguu tunavyoungia mboga, wanatengeneza mbolea, na vingine vingi, bado wanatengeneza chanjo ambazo kila mtoto mchanga anachomwa, je wakiamua kutubadilishia DNA kama reference ya bandiko ulilotoa linavyoeleza, wangeshindwa?
NB: Mimi sijachanjwa na sifikirii kuchanjwa kwa sababu moja kubwa, bado ni kijana, nina nguvu na ninaamini kwenye kinga yangu ya mwili kufight against COVID. Lakini nachelea sana kuwa sehemu ya kuwatia hofu wengine juu ya madhara ya chanjo, tuhuma ambazo sina uhakika nazo kwa walau asilimia 50.