realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 7,450
- 19,184
Ongezeko la wafanya biashara wa vipodozi vya kung'arisha limekuwa la kutisha. Kila siku akaunti mpya Instagram, TikTok live kila saa. Bei sh 3,000 - sh 10,000. Ahadi ni "Dada, siku 3 tu unakuwa mweupe kama umepigwa filter". Watu wengi wananunua bila kuuliza kuhusu usalama wa Ngozi.
Biashara inaenda, lakini afya yetu?
Ukweli mchungu: Ngozi ya binadamu haibadiliki kwa siku 3. Kama cream inakufanya uwe mweupe haraka hivyo, ndani yake kuna kemikali kali zilizopigwa marufuku kama Hydroquinone na Mercury.
Kazi yake ni kuchoma tabaka la ngozi ili ionekane kung'aa kwa muda. Baada ya miezi kadhaa, ndio madhara yanaanza: madoa meusi, ngozi nyembamba kama karatasi, chunusi na kadhalika.
TFDA wameshasema wazi: "Vipodozi vyote lazima viwe na namba ya usajili. Vipodozi vya kung'arisha vilivyo na hydroquinone zaidi ya 2% ni kinyume cha sheria".
Polisi wamekuwa wakikamata mizigo bandari. Lakini wauza mitandaoni bado wanaendelea. Je, sheria zetu zimedunda? Au watendaji hawana nguvu za kufuatilia mauzo ya online? Au sisi wanunuzi ndio tunawapa nguvu?
Tujadiliane:
1. Kwanini wauza vipodozi hatari wameongezeka hivi sasa?
2. Serikali kupitia TFDA inapaswa kuchukua hatua gani zaidi kudhibiti hili?
3. Wewe kama mnunuzi una wajibu gani kabla ya kupaka kitu usoni?
Lengo ni kuelimishana. Ngozi ni moja tu ndugu, tukiharibu hatuna spare.