Ongezeko la wanywaji wa Mo Extra (energy drink) limesababishwa na nini?

Kinywaji kizuri kwanza ladha ya sukari ni ndogo ukilinganisha na azam energy.
Kina uchachu fulani na hakina tatizo ukilinganisha na azam energy ukinywa hiyo presha mpaka kichwa.

Jamaa wa mo mkemia wake ni mzuri na sijaona tatizo nikinywa ukilinganisha na energy nyingine.

Uzuri sio hatari kwa afya kama unakunywa kistaarabu
 
Kunyweni kunyweni Simba yetu isonge mbele
Mhindi wenu janja janja ataendelea kuwapiga mpaka mnyooke kama rula. Hamuendi kokote nyinyi mbumbumbu.

Na mkumbuke pia kuacha kunywa mara moja hizo takataka zake. Maana mtakufa kabla ya wakati wenu. Huwezi mtu kuwa na akili zako timamu, halafu ukanywa energy drink. Ni wendawazimu pekee ndiyo wanaokunywa hizo takataka.
 
Vijana tujitahidi tunywe maji ya kutosha,huyu mhindi unakuta yeye hanywi energy anazoziuza.
Pigia mstari. Unadhan anakunywa mavitu hayo.tunapoelekea ni kubaya siku hizi unakuta nimeshuhudia kwa macho yangu vibint viwili vina mo extra na mihogo ya kukaanga.kweli? Asubuhi asubuh nikajisemaa hiiii. Elimu ya utambuzi ndio shida.watoto vijana na watu leo sio wenye kusoma mambo
Sisi kaz yetu kujua mwijakuw leo kafanya nin bas
 
Habari zenu wakuu,

Kumekuwa na wimbi kubwa la rika lote la watu katika jamii ya Kitanzania kupendelea zaidi kinywaji cha "Mo Extra" kiukweli nilikuwa naomba tupeane shule kwanin...
Umaarufu wake umeongezwa na utumiaji wa kinywaji hicho kama mixer ya pombe kali kama double kick, smart gin, k Vant, gongo etc. Mtu anapiga hiyo mchana kweupe haumshtukii kabisa, wateja wakubwa boda2, daladala operators, mafundi, mateja.
 
Well said.
 
Mbona povu kama umekamata ugoni? Kisa umeona jina Simba umechefukwa..nani anakunywa sasa hapo unaemwambia?? Mm sijawahi na sitakuja kunywa hayo madudu..wanaokunywa wacha wanywe kwa their own risks..mimi nimeongea kwa kuwabeza tuu wanaotumia...sasa naona unanipovukia kama mm ndo nimekosa nguvu za kiume ebooo....
Kweli umekosa hata akili moja ya kutambua naongea nini hapo...
Halafu kila kitu kina risk zake unajiona mjanja kuwatukana wanywa energy wakati ww kwa siku unamaliza soda 3...
Kila kitu kinahitaji moderation..wangekua wanakunywa atleast moja kwa siku mtu anapiga hata 4....that's nonsense...
Sijui zinanogaje aisee akili imegoma hata kutaste kun vinywaji vinauzwaga mpk leo sijui ladha zake...
 
Maelezo mazuri But meharibu tu kumuita Mo "Muhindi"
Hiyo ni racism.
 
Na wewe umepaniki, na wakati nakuzingua tu. Nothing serious at all.
 
Na Kuna energy mpya imeingia mtaani kutoka kampuni ya Pepsi inaitwa supa commando huku mtaani inanyweka balaa

Hayo madude ni hatari sana ,mimi sijawahi kunywa hayo mavinywaji yao ya kuongeza nguvu.......Na wafanyabiashara washajua kama yanapendwa hivyo wanazidi kuyaongeza ,hata ali kiba alikuwa na Mofaya sijui iliishia wapi.
 
madhara yapo
 
Vijana wengi wa siku hizi mnaendekeza urojorojo mno, embu acheni kujilainisha kama mlenda. Mtu akisikia uchovu kidogo anakimbilia energy drink! Huu utamadumi mbovu kabisa. Wakati wetu mtu ukisikia uchovu unakwenda uwanjani kucheza mpira unatoka hapo unaoga, unakula ugali, unakwenda prepo au kwingineko. Vijana wa siku hizi acheni mdebwedo.
 
achana na vinywaji vya energy blah blah bla...si mo enenrgy tu, hata za kutoka nje kama redbull ni majanga matupu. ukisoma ile chemical composition tu inakuashiria hatari!
 
Naona mitaani zinanywewa kama maji tu, nafikiri hizo zinafaa kunywewa mara chache na watu ambao wanakuwa wametingwa na kazi nyingi za kuchosha mwili na akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…