Mburia
JF-Expert Member
- Jul 15, 2022
- 2,369
- 3,488
Kiukweli hivi vinywaji vya kuongeza energy lengo hasa ni mtu atumie baada ya kuwa anafanya kazi ngumu mfano wabeba matofali, zege na kazi nyingine nzito nzito. Sasa unakuta mtu ni bodaboda akipiga trip 3 anarudi kijiweni anaagiza energy drink, hii ni hatari sana.Kinywaji kizuri kwanza ladha ya sukari ni ndogo ukilinganisha na azam energy.
Kina uchachu fulani na hakina tatizo ukilinganisha na azam energy ukinywa hiyo presha mpaka kichwa.
Jamaa wa mo mkemia wake ni mzuri na sijaona tatizo nikinywa ukilinganisha na energy nyingine.
Uzuri sio hatari kwa afya kama unakunywa kistaarabu