Ongezeko la watu hifadhi ya Ngorongoro kuleta madhara makubwa kwa wakazi asilia na uhifadhi

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
969
Reaction score
1,055
Wakuu,

Gazeti la JAMVI LA HABARI limeendelea kuandika masuala yanayohatarisha ustawi wa watu, wanyamapori, mifugo na uhifadhi katika Mamlaka ya Uhifadhi wa Eneo la Ngorongoro.

Gazeti hilo rimeripoti kuwa watu wameongezeka kutoka watu 8000 mwaka 1959 hadi 110,000 mwaka huu linalosababisha madhara makubwa kwa wakazi asilia na uhifadhi.

Aidha Gazeti limeongeza kuwa kuongezeka huko kwa watu kunakwenda sambamba na uongezeka kwa Makazi holela yasiyo shabihiana na mazingira yameongezeka kufikia kuzuia njia za asili za Wanyama na yasiyofaa kwa maisha ya binaadamu.

Gazeti likaripoti pia kuongezeka kwa watu kumesababisha kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha umaskini kwa wakazi wenyeji wa tarafa ya Ngorongoro kufika asilimia 50.0%. ambapo uchumi unadumaa kutokana na kukosekana kwa mifugo kwa zaidi ya kaya 5,000 kati ya kaya 22,000 (22%).

Katika mwendelezo wake Gazeti likawanukuu Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na taarifa (Media Centre for Information and Resources advocacy - MECIRA) kuwataka wanaharakati kusimamia ukweli, kuacha kupotosha kuwasaidia wakazi wa Ngorongoro wapatiwe sehemu salama ya kuishi kunusuru Maisha yao ni uhai wa hifadhi.

Gazeti limebainisha kuwa siku za nyuma zaidi kaya 110 ziliwahi kuhamishwa kwa hiyari kupelekwa katika kijiji kipya cha JEMA ambapo waliwekewa miundombinu yote muhimu.

Aidha gazeti limeonyesha hatari ya Ngorongoro kuteketea au kuwa kwenye hali ni mbaya zaidi kutokana na sababu mbalimbali zinazoashiria kuharibiwa na hatimaye kupotezwa kwa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro hifadhi yenye sifa lukuki ndani na nje ya nchi.

Gazeti limeandika kuwa Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na Taarifa (Media centre for Information and Resources advocacy - MECIRA) kimesikitishwa na hali ya Maisha duni wanayoishi wakazi wa tarafa ya Ngorongroro iliyomo ndani ya hifadhi kutokana na uduni wa Maisha unaotokana na changamoto kadhaa kubwa ikiwa ni kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya watu ndani ya eneo hilo la hifadhi kunakosababisha kuongeza umasikini wa wakazi husika.

KWA UCHACHE HII HAPA SEHEMU YA HABARI ILIYOANDIKWA GAZETINI

Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iloyosainiwa na mkurugenzi mwendeshaji wa kituo hicho Habibu Mchange.

Wamesema kuwa tatizo lililopo Ngorongoro haliathiri uhifadhi pekee bali pia hata Maisha ya wananchi wa eneo hilo wanaathirika kutokana na ongezeko kubwa la watu kuliko uwezo wa eneo kuwahudumia.

Mchange amewataka wanaharakati wote wanaojitokeza kupaza sauti, kuhakikisha wanasimama kwenye ukweli ili kuwanusuru wakazi wa eneo hilo ambao kwa hakika usalama wao kiuchumi, kiafya, kielimu na kiusalama ni mdogo sana kutokana na wingi huo wa watu.

‘’Utafiti wetu tulioufanya kwa wiki mbili tatu hizi, pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali, taarifa mbalimbali na mazungumzo baina yetu na wakazi wa eneo husika, tumebaini kuwa mambo mengi yanayosemwa na wanaharakati kadhaa na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari hayana ukweli na kwa kweli yanapotosha umma na wakazi wa eneo husika hayawapendezi’’. Inasema sehemu ya taarifa hiyo.

‘’Kwakweli tumegundua mambo mengi sana, tumegundua namna watoto wadogo wa kimasai wanavyotumikishwa kazi ya ufugaji kutwa nzima bila kujali kama kuna kwenda shule, tumegundua namna maradhi ya milipuko yanavyowatesa wakazi hawa, tumegundua namna umasikini ilivyokithiri kiasi ha watu zaidi ya asilimia 50 kuwa katika hali kubwa ya umasikini licha ya kuwaona wamezungukwa na mifugo mingi’’. Ananukuliwa Mchange katika taarifa yake hiyo.

‘’Taarifa zinasema mwaka 1959 palikuwa na watu chini ya 8000 tu, emagine mwaka 2017 watu walifika elf 94, leo hii wanakadiriwa kufika watu laki moja na elfu kumi na kidogo, kwa ukuaji huu wa watu kuna kila sababu ya watu hawa kutafutiwa maeneo huru ya kuishi ili waweze kujiendeleza bila kuathiri uhifadhi na mazingira, mle hifadhini kwa sheria inayosimamia uhifadhi hawataweza kupata haki yao ya maendeleo endelevu hivyo watakuwa masikini tikatika jambo ambbalo linawekana kabisa kuepukwa kwa wao kuondoka’’. Anasema zaidi.

Mchange anasema kuwa hadi sasa taarifa za NBS zinaonyesha kuwa pamekuwepo na hali ya kudumaa kwa uchumi kunakotokana na kukosekana kwa ambapo zaidi ya kaya 5,000 kati ya kaya 22,000 (22%) zilizopo hifadhini humo hazina mifugo.

Tunajiandaa kutoa taarifa rasmi ya uchambuzi wa hali ilivyo, ilivyokuwa na itakavyokuwa hivi karibuni, lakini kwa sasa sisi kama MECIRA pamoja na kutishwa kwetu kwa kuathirika kwa hali ya uhifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro, tunadiriki kusema kuwa hali pia ya Maisha ya wenyeji na mbaya pengine kuzidi maeneo mengi hapa nchini, na ubaya huu unatokana na kuongezeka kwao kwa kasi kubwa.

Taarifa zaidi zilizozifikia gazeti hili zinaonyesha kuwa miaka kadhaa nyuma zilihamishwa kwa hiyari zaidi ya kaya 110 kutoka hifadhini kwenda Kijiji cha JEMA kilichopo wilayani humo.

Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Hifadhi ya Ngorongoro ipo hatarini kupotea na kupoteza uhai na umashughuli wake kutokana nna kukithiri kwa shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji uliopitiliza kiasi, ujenzi wa nyumba zisizofuata taratibu za kihifadhi na shughuli nyingine za kibiashara.

Mwaandishi wa habari hizi ameshuhudia bmakundi makubwa ya mifugo ikiwemo Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, kuku, na mingineyo ikichukua eneo kubwa kuliko Wanyama wa asili wanaopendwa kufuatiliwa na watalii.

Pamoja na kuzingatia ukweli kuwa Ngorongoro ni hifadhi ni hifadhi ya kipekee inayowahusisha Wanyama binaadamu na mifugo kwa pamoja lakini hali ilivyo kwa sasa inatisha kiasi cha kutishia usalama wa hifadhi na wananchi husika wa asili wanaoishi katika eneo hilo.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezitafiti ni kuwa mwaka 1959 wakati wakazi walioruhusiwa kuishi katika hifadhi hiyo kwa mchanganyiko wao na Wanyama pori, wakazi hao hawakuzidi watu elfu 9 tofauti na sasa wakazi hao wamefika zaidi ya laki moja na mifugo yao wanayoimiliki ikikadiriwa kuwa zaidi ya laki 6.

‘’Kwa mujibu wa taarifa wanasema kuna mifugo laki 2 na nusu, nadiriki kusema sio kweli, mifugo hii haipungui haipungui laki saba hadi laki nanehebu angalia tangu tumeanza kuanza makundi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo sasa hivi ni zaidi ya masaa mawili tunazunguka tunawaona tu…hii maana yake kuwa hata kama watu hawa wapo kisheria lakini inahitajika jitihada za makusudi kunusuru tatizo hili…hili ni tatizo kwa kweli’’. Alisema Paul Schenzern Raia wa ujerumani aliyekuwa katika safari za kitalii.

Schezern ameongeza kuwa kwao wanavyoifahamu Ngorongoro nin kuwa eneo bora zaidi la kiutalii na kamwe hakuwaza kama angepita barabani akipishana na ng’ombe na mifugo mingine japokuwa alikuwa anaufahamu kuwa Ngorongoro wanaishi binaadamu na Wanyama lakini si kwa kiwango alichokiona.

‘’Nimetembea hifadhi kadhaa Duniani ambazo Wanyama na binaadamu wanaishi kwa asili, kwa kweli zinavutia n ahata kuishi kwao kunaemndana na uhifadhi wa mazingira, tofauti na hapa Ngorongoro…ntapata shida san akumshawishi mtu atakayeniomba ushauri juu ya kutaka kuja hapa. Nafikiri watetezi wa haki za binaadamu, mifugo, Wanyama na mazingira wanapaswa kupaza sauti ya pamoja kuinusuru hifadhi hii muhimu na bora’’. aliongeza.

‘’Unajua watu wanaweza kulalamika kwamba wanaishi humu na haipaswi kupangwa vizuri, lakini sio sahihi watetezi makini wa binaadamu wanatakiwa watetee kwanza usalama wa mazingira, usalama wa mazingira ya Ngorongoro ndio usalama wa Arusha, usalama wa Arusha ndio usalama wa Tanzania na ndio maana Dunia nzima kunakuwa na sheria kali zinazolinda mazingira…..kujazana kwa watu na mifugo hifadhini sio haifai tu kwa mifugo bali haifai zaidi kwa binaadamu wanaoishi nhumo kwani kuishi kwao kunategemea zaidi ikolojia nya hifadhi husika’’. Alisema Habibu Mchange, Mratibu wa mtandao wa wanahabari wanarasilimali asilia na taarifa alipoombwa kutoa maoni yake.

Mchange alisema kuwa hata yeye alikuwa Ngorongoro mwishoni mwa mwaka jana na ameshuhudia ujenzi uliokithiri na unaovunja kabisa sheria na kanuni za uhifadhi na kuongeza kuwa anaandaa ziara ya wanahabari wanarasilimali asilia na taarifa kwenda kujionea hali ilivyo na kuuhabarisha umma na kuwataka wanaharakati kushirikiana kuokoa kivutio hicho muhimu.

‘’Hata mimi nilitembbea tembea mwishoni mwa mwaka, niliyoyaona Ngorongoro kwa kweli yanatisha na hayafai kusimuliwa hata kidogo, wadau nwa utalii, uhiofadhi na mazingira tusipochukua hatua na kupaza sauti, Ngorongoro itapotea kama upepo. Kwa kifupi tu nikuambie ndugu mwandishi kuwa NGORONGORO IPO HATARINI KUPOTEA’’. Aliongeza Mratibu Mchange.
alisema.

IMG-20220131-WA0091.jpg
 
Serikali ya Mama Samia ni sikivu sana.

Hawa waondolewee Haraka sana

Hongereni Sana Jamvi la Habari kwa kuonesha haya madudu
 
Inaonekana wakati sera zinatungwa hawakujiuliza juu ya ongezeko la watu na ongezeko la mahitaji. Sasa sera itamke rasmi kwamba hifadhi inaweza kuhimili kaya kadhaa, binadamu kadhaa, mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo, punda) kadhaa. La pili kuwe na makazi mbadala kwa idadi inayozidi kile kikomo.

Gazeti la Jamhuri lipongezwe badala na lipewe haki zote za vyombo vya habari kuliko mafisadi kulisumbua na fungia fungia.
 
Kwa hakika umenena. GAZETI LA Jamhuri liliwahi andika pia kama ambavyo gazeti la JAMVILAHABARI linavyoandika kwa ufasaha
 
View attachment 2102101
Kuna taasisi na watu mbali mbali wenye interest na Ngorongoro:

1. Ngorongoro Conservation Authority
2. TANAPA
3. Wizara ya Maliasili na Utalii
4. Wadau wa utalii, Arusha

Hivi kati ya hawa wote hakuna anayeona hii hatari akapiga kelele, akawaita wenzake, ili uvamizi huu uthibitiwe?
 
Tuendelee kuwakumbusha pengine wataamka
 
yaani huwa sielewi masai wataishi porini hadi lini aisee, hadi wanang'angá nia waishi na wanyamapori. waache akili za kiporipori serikali itume jeshi ikawafukuze maeneo ya mbuga haraka, wakiwalea lea ndio wanazidi kuzaliwana na wanavyooa wake wengi. kuna siku wataomba mbuga yote waibadilishe yawe makazi na kwasababu watakuwa wameshakuwa wengi basi. hivi ccm inapata kura kiasi gani kwa hao, ikiamua kuwapiga chini kura zao zina athari yeyote kwao?
 
Hivi kumbe kuna watu wa kutosha tu mpaka nyumba za bati zipo!!!????
Mkuu mpaka mabasi yanapishana kila baaada ya masaa kadhaa pia kuna maduka na bar mle, kama mtu amewahi kufika ndiye anaweza kuelezea ila kama unasikia kutoka kwa wanaotoa povu uanweza kudhani wanaonewa.

Mfano baadhi ya wanaosema wasiondolewe au kuwasemea wale jamaa waishio ngorongoro wengi wana ukwasi wa utajiri as majumba ya biashara Arusha mjini, Karatu nk, huku pale ngorongoro ikiwa ni eneo lao la kutunzia mifugo na wakiwaacha ndugu ambao kazi yao kutunza boma na mifugo.

NGORONGORO INAPOTEA, SERIKALI CHUKUENI HATUA MAPEMA.
 
Umenenaa vizuri sana
 
Kwa kweli inapoteq....na jitihada za harakavzinahitajika
 
Back
Top Bottom