Wataalam wenyewe ukiingia tu wataanza kukwambia usome mavitabu, unaweza ingia ukapata ukichaa, u can lose all kabisaa
Vitabu, websites za forex, kufuatilia fundamentals na zinavyoingilia bei za fedha .
Mfano, bei ya mafuta inaingiliana sana na bei ya dola kwa sababu mafuta yananunuliwa kwa dola, lakini nchi za kiarabu zinazouza mafuta nyingi baada ya kupata dola hufanya biashara ya kununua vitu kutoka Europe kwa kutumia Euro, bei ya mafuta ikishuka hilo linaweza kumaanisha nini kwa uwiano wa Euro/Dollar?
Kufuatilia ma gavana wa benki kuu za nchi muhimu wanahosema kuhusu mwenendo wa hela, interest rates etc.
Kitu kama "Economic Calendar" ya Wall Street Journal ni muhimu sana kusoma ili kujua vitu vilivyokuwa scheduled kwa wiki.
Nasoma Wall Street Journal la jana hapa, kuna story moja inaelezea USD itaendelea kupata pressure, pia nasoma Economic Calendar Jumatano kuna Minutes za Federal Reserve ya US, hizi zinaweza ku move markets, Alhamisi kuna ripoti ya Wizara ya Biashara ya Marekani kwa mwezi wa May, hii nayo inaweza ku move markets itakapotoka. Ijumaa kuna ripoti ya Wizara ya Kazi ya Marekani, watu wataangalia mishahara ilivyoongezeka na ripoti ya unemployment kwa mwezi wa June.
Hizi habari zote mtu akitaka kufanya forex inabidi azijue.
WSJ la July 03 attached, kuna article "Dollar is Getting Squeezed From All Angles" inaongelea dollar na kuna economic calendar ya week. Those are must reads.