Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baada ya kugundua uhakika wa kampuni unayotaka kununua item, waambie wakupe invoice yenye acc number na swift cose yao.........wakikupa unaipeleka crdb, nao crdb watatuma kwa ada yao nadhani ni $50/- lakini kama wewe una account na wao ndio wanakubali!
Jitahidi uwe umeenda kubadili tshs (hela zako) kwa US$ katika bureau, ili ununue dola kwa bei rahisi uende nazo bank kuliko ukienda na shilingi benk watakubadilishia amount kwny invoice kwa rate zao.
Mkuu umenena vizuri, ila nadhani unaongelea TT na sio purchasing ya kutumia ATM card anayoulizia MABAGHEE
japo TT ndio njia salama na uhakika zaidi sema inagharama na lazima uende benki.
Kuhusu manunuzi kwa kutumia kadi ya CRDB, kwanza kabisa lazima ujaze form ya kuomba ku activate kadi yako ili uweze kuitumia online. Fomu hii unaipata kwenye tawi lako ( kwa mujibu wa mfanyakazi wa CRDB PPF tower branch).
Ila ningekushauri upate kadi ya nabk ABC ili uwe unaweka hela pale unapotaka kufanya transaction tu, mimi natumia hiyo naogopa watu wakiamua kuniibia kadi yangu ya account nnayoitumia wataniumiza sana tofauti na kadi ya ABC ambayo huwa naweka tu kile kiasi nnachotaka kukitumia online, na hata kadi ikipotea ubadilishaji wa kupewa kadi nyingine ni wa haraka, siku hiyo hiyo unapewa kadi yako mya.
Ubarikiwe
ha ha ha ha!!nikisikia ameondoka pale nitafanya sherehe!!natamani hata achomoke...Jamani nawashukruni sana kwa maoni yenu. Niliwahi kwenda pale CRDB UDSM (ndipo nilipofungulia card yangu). Kuna dada mmoja mtoto wa kigogo wa CRDB, hana chembe ya customer care. Majibu yake ni ya mkato as if hela atakupatia yeye. Najua kuna wizi wa mtandao mfano unaweza kuhitaji kitu ebay lakini jamaa wakahack contact za ebay na mwishowe utatuma hela kwao bila kujua. Wezi hao wako Romania na Nigeria.
Dah! wanaweni mi naomba niulize!! hivi hapa kwetu hizi kadi zetu za visacard/ master card - hazina card number, date and the year of expire?? kisha nyuma ya kadi kuna 3 digits ambazo unamalizia kisha wire yoyote ile international inakubali bila kuongea au kujadiliana na benki as long kwenye account kuna karanga!! nitoeni ushamba mwenzenu. kw sababu kuna binadamu mmoja alifanya hayo ya juu hapo bila longolongo ila kadi yake ni visa kadi ya kutoka kwa wenzetu kule wanaoishi karne ya 27 already now 🙂
Jamani ninahitaji kufanya manunuzi ya vitu mbalimbali online kwa kutumia CRDB card yangu. Nifanyeje? Masharti gan yanatakiwa kufuatwa ili niwe nanunua bidhaa kutoka america, ulaya ana asia kwa kutumia kadi yangu ya benki.