Pre GE2025 Online TVs zimekuwa compromised na CCM? Anachofanya Baba Levo kuhusu ''Mama Hana Deni'' ni kampeni kwa Rais Samia na CCM kuelekea uchaguzi mkuu

Pre GE2025 Online TVs zimekuwa compromised na CCM? Anachofanya Baba Levo kuhusu ''Mama Hana Deni'' ni kampeni kwa Rais Samia na CCM kuelekea uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Hii kampeni feki kabla ya Uchaguzi iliyopewa jina la ''Mama Hana Deni'' imekaa kimkakati kuisaidia CCM ambayo ndio inaongoza Serikali kuweza kuonesha miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa kwa kodi za wananchi. Sasa hii naona Baba Levo kaamua kuichukua akishirikiana na Online TVs nchini, kuzunguka nchi nzima kukagua hiyo miradi. Mbaya zaidi wanatembelea miradi mizuri mizuri na kuacha mingi ambayo imeshindwa kufanikiwa au kutelekezwa

Kuna tuhuma na hisia miongoni mwa watu kwamba baadhi ya vituo vya televisheni vya mtandaoni (Online TVs) vinaegemea upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM) au vimeingiliwa ili kutangaza habari zinazounga mkono serikali na chama tawala.

Hii inaweza kutafsiriwa kama...
Upendeleo - Baadhi ya watu wanaona kuwa vyombo hivyo havikosoi sana serikali au CCM na badala yake vinatoa taarifa zinazounga mkono sana chama hicho.
Kulipwa au kununuliwa - Kuna wanaodhani kwamba baadhi ya Online TVs wanalipwa ili kuendesha ajenda fulani za CCM.
Uoga wa kufungiwa - Wengine wanaona kuwa huenda vyombo hivyo vinaogopa kufungiwa na mamlaka kama hawataonyesha upendeleo kwa serikali.

Hiki anachofanya Baba Levo binafsi naona ni kampeni kwa Rais Samia na CCM kwasababu hizi
  • Baba Levo ameonekana mara kadhaa kuonyesha wazi kumuunga mkono Rais Samia na CCM.
  • Slogan ya "Mama Hana Deni" imetumika sana kama sehemu ya kuonyesha mafanikio ya serikali ya awamu ya sita na kuandaa mazingira ya uchaguzi mkuu 2025.
  • Mara nyingi, kauli kama hizo kutoka kwa watu maarufu hutafsiriwa kama kampeni za chinichini za kuandaa wananchi kumpigia kura kiongozi au chama husika.
Kwa hiyo, ingawa Online TVs zinaweza kusema zinafanya hivyo kwa mapenzi yao au kama sehemu ya kazi zao, wengi tunatafsiri kuwa ni kampeni ya Rais Samia na CCM kuelekea uchaguzi mkuu.

Wito wangu kwa Online TVs, najua njaa kali sana mtaani ila hii haiwazuii kusimamia weledi wenu ipasavyo. Igeni mfano wa Jambo TVs katika uhabarishaji wenu. Kuna maisha mengine baada ya uchawa, msije tumiwa na kutupwa.

Baba Levo.png
 
Mnaoangalia ndio mjilaumu
Uzuri Utube wazuri kufunga online tv mbofumbofu!
 
Siwez kukaa na kuwasikiliza hao sjui wasafi,efm,crown, clouds na tktk zingineee
Dawa ni kuacha kuwafatiliaaa hao

Ova
 
Tatizo hawajiamini, kama wamefanya yote hayo kwanini watumie nguvu na pesa nyingi?
 
Back
Top Bottom