Chamber Squad muziki wamejifunzia kwa Prodyuza Expera wa Tushikamane Records pale Moro,kipindi hicho wanajiita CF Boyz..na wale hawakuwa wote watoto wa Dom sema walikutana tu shuleni Mazengo Sec,Mangwea alikuwa anaishi Forest Hill Morogoro ndipo wazazi wake wanaishi sema anapenda kuiwakilisha Dom zaidi ata Noorah Kwao ni Shinyanga...ata ivyo hawa wote ni wa juzi tu.
Moro kuna hazina kubwa ya historia ya huu muziki,sema haijawai kuwekwa kwenye maandishi watu wakaijua.
Ni vema ukajifunza mengi kuliko kujifanya unajua kila kitu!
Kuna tofauti kubwa kati ya CF Boyz (Albert Mangwea a.k.a Mangwair, Mallo Star a.k.a Nzeku Chipa, QG a.k. Moses Bushagama) na
36 Chamber Squard (Agustino Makale a.k.a Accapaino, David Kabongo a.k.a Dark Master, na Athony a.k.a Tonny Kichwa Ngumu)
CF Boyz wanafanya rekodi morogoro kwa produza Kameta mwaka 1998, album yao iliitwa Heshima kwa wote na ilikuwa na nyimbo 6.
Chamber Squard ya kina Dark Master ilishinda mashindano ya Hi Hop mkoa wa Dodoma mwaka 1995 katika Ukumbi wa NK Disco Teque, Fainali waliingia na Mob Monster na Gz Mob
Hapo Magwea, Mez B na Nzeku wakiwa darasa la 6 shule ya msingi Mlimwa!
So usiseme vitu usivyovijua, Nzeku, Mangwea na Mez B wamekua marafiki toka shule ya msingi Mlimwa wakati wakiishi Area C kabla ya kukutana Mazengo mwaka 1997 wakiwa kidato cha Kwanza na kuamua rasmi kuanzisha kundi la CF Boyz.
Mwaka 1997 Dar Master, Tony na Accapaino a.k.a Tino Makale Designer ndio walikuwa wanamaliza shule Mazengo, kwa hyo baada ya Tino na Nzeku kuacha kujishugulisha na muziki ndipo mwaka 2000 Mez B na Mangwea walipomaliza kidato cha nne wakaamua kuelekea Dar es salaam kuungana na Dar Master na Tonny na kuwa Chamber Squard!
Mwaka mmoja baadae 2001 Malik Haji Nura nae alipomaliza kidato cha 4 akajongea Dar kuugana na Chamber Squard!
Labda pia nikufahamishe maana ya 36 Chamber iliyozaa Chamber Squard, shule ya sekondari mazengo ilikuwa na mabweni 4, ila katika mabweni hayo manne Bweni la Ujamaa ndo lilikuwa kubwa, refu na vyumba vingi kuliko yote!
Miongoni mwa vyumba vya bweni hilo ni chumba namba 36, ambacho asilimia kubwa ya walikoua wakiishi hicho na kushinda walikuwa wanahusudu muziki wa HI HOP.
So ikawa wanafunzi wakikosa kuwaona wenzao darasanai wakiulizana wengine wanajibu atakua 36 Chamber!
36 Chamber Dar Master na Accapaino walikuwa wakiishi Uzunguni na Tony alikua anaishi Kikuyu!
Wakati huo Magwea na Nzeku walikuwa wakiishi Area C na Mez B walihamia Kikuyu.