Only for Great Thinkers....

Only for Great Thinkers....

Nataka kuwa mkweli kivyangu. Mimi sasa ni babu wa miaka 62

Kwanza nakiri nilishapenda na nikapendwa lakini ndoa ikashindikana kwa sababu ya majukumu, mwenazngu kapelekwa mbali kikazi na mimi nilikuwa bado nakula kitabu; tulipokutana ananionyesha ana watoto wanne hawana baba. Akaniambia bado ananipenda lakini...

Halafu nikapenda na kupendwa lakini ndoa ikashindikana kwa sababu ndugu hawakutaka binti yao aolewe na mimi na mimba yangu ikatolewa na upande wa binti. Mwenzangu akaishia kuzaa hapo nyumbani hadi leo zaidi ya miaka 20 hataki kuolewa.

Nikaamua nifuate mila angalau za upande wa mama. Nikamuona mama yangu mzazi na wajomba zangu; maana yake wanazifahamu familia zenye mabinti wenye malezi na maadili mazuri. Ukatumiwa utaratibu mzuri nikapewa uhuru wa kuchagua kati ya familia tano pamoja na sifa ya kila familia na kila binti. Nikafanya uchaguzi wangu kwa vigezo nilivyopewa na mama yangu mdogo ambaye ndiye naishi nae.

Nilikutana kwa mara ya kwanza na mwenzangu siku ya ndoa yetu. Tukakaa kimila kijijini kama inavyotakikana tukaenda kwetu.

Nakiri tulipata tabu kidogo kwa mara ya kwanza. Mungu ametujalia watoto watano. Tukasaidiana katika hali na mali, tukaaminiana matokeo yake TUNAPENDANA SANA hata baada ya miaka zaidi ya 30 ya ndoa.

Sasa huo ni uzoefu wangu kuwa mapenzi yanajengwa kwa vigezo vingi sana yanahitaji muda nakupitia kwenye mitihani hasa ya kifamilia. Ndoa inahitaji marekebishano (adjustment) ili muwe kwenye level ya kukubaliana bila kuulizana. Kwa kweli nafurahi sasa mke wangu anavyoniita mpenzi kwa sasa kwa sababu amefaulu mitihani yote ya mapenzi na mimi nampenda sana kwa thamani yake ya nyumba yetu kuheshimika.


Now, if marriage came out of a true love, does true love expires? Ndoa yangu haikutokana na "true love" ila imejengeka na imezaa "true love" kwa kipindi kirefu tukiwa pamoja na mwenzangu. Namshuru sana Mungu. It is being rejuvenated every day (INACHANUA KILA SIKU).
 
Normally marriage comes out of love... but through experience, durability of the most marriages is a matter of decision and no longer love... Now, if marriage came out of a true love, does true love expires?

I dont know if am right but mi naamini love haiishi but the SPARKLE!.thats what married people have to work on,because if you really love someone,then love lasts but what made you blossom into love ndo inaisha at times,.and true love ndo kabisa,it cant expire(still its the sparkle thats needed)..because you can marry a person that humpendi but eventually love that person because of the sparkle that arises!and the viceversa is true.
 
ther z no tru love under da sun...................no one to trust
 
Back
Top Bottom