Only in Tanzania

Only in Tanzania

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2011
Posts
9,836
Reaction score
7,231
Nimesoma gazeti la Habari Leo na kukuta habari ya wanafunzi 44 waliofeli la 7 wako sekondari huko Mkoani Katavi. Hawa wanafunzi walifeli la 7 kwa sababu hawana akili za darasani, leo hii waje kwenda sekondari na chuo kikuu si tutapata viongozi dizaini ya waziri Muhongo hapa? Jamani kwa nini hivi Tanzania? Siyo kila mtu lazima awe kiongozi, pengine hawa watoto waliofeli ndiyo wakulima bora.

Chanzo: HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania/index.php/habari-za-kitaifa/6055-waliofeli-la-saba-wakutwa-sekondari
 
Du mkuu naogopa kuchangia kwani waziri Muhongo si professor
 
Kuchangia unaweza kuchangia kama una hoja, ila naona umejichanganya kwani mi sikusema kama waziri Muhongo ni profesa. Niliuliza tu kama hali ni hii ya kupeleka wanafunzi waliofeli la 7 sekondari (provided they are NOT smart, that's why they failed) then waje waende chuo kikuu, si tutapata viongozi wasiokuwa na akili na maadili ya kuongoza nchi? Au ulisahau miwani mkuu, rudia tena mistari yangu halafu nisahihishe.
 
ku fail darasa la saba sio kutokuwa na akili . na ikitokea wakaenda chuo kikuu na wakamaliza basi hao wana akili ndio maana wasoma hadi chuo kikuu na kumaliza . harafu kwani mkulima stadi hatakiwi kusoma ??????? nadhani wewe uliyeleta hii hoja ndio unamatatizo either ya elimu ndogo au upeo duni wa kufikiri.
 
sasa hao wanafunzi wasipofaulishwa kuingia sekondari inaweza ukakuta shule za sekondari zina wanafunzi wawili tu darasani sa kuliko kufundisha wanafunzi wawili si bora shule zifungwe au hao vilaza wapitishwe wajaze madawati
 
Kuchangia unaweza kuchangia kama una hoja, ila naona umejichanganya kwani mi sikusema kama waziri Muhongo ni profesa. Niliuliza tu kama hali ni hii ya kupeleka wanafunzi waliofeli la 7 sekondari (provided they are NOT smart, that's why they failed) then waje waende chuo kikuu, si tutapata viongozi wasiokuwa na akili na maadili ya kuongoza nchi? Au ulisahau miwani mkuu, rudia tena mistari yangu halafu nisahihishe.

Uliposema kuwa "leo hii waje kwenda sekondari na chuo kikuu si tutapata viongozi dizaini ya waziri Muhongo hapa?" hapo ndo sikuelewa vizuri maana najua huyu mtajwa ni miongoni mwa mawaziri ndani ya baraza la mawazili ambao ni maprofessor
 
Safi sana. Lakini si unajuwa huo uprofesa anaujuwa yeye kwani huyu jamaa ni mtaalam wa kughushi vitu hivyo hata uprofesa wake ni batili pia. Binafsi siamini chochote asemacho huyu jamaa. We profesa gani hajuwi historia ya nchi yake? Yaani ni afadhali angejichanganya kwa vingine lakini nchi ambayo yeye ni mtawala wa wizara? Aaaah, huku si kuchemka ila ni umagumashi wa kujitwisha vyeo asivyoviweza.
 
Ndugu nadhani uko kasi sana ndo maana umechemka, jaribu tena kupata muundo wa baraza la mawaziri mimi nadhani unataka kumaanisha waziri philip mulugo wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi na si profesa muhongo wa nishati na madini,labda ututhibitishie ni wapi na lini huyu prof. muhongo alikosea historia ya nchi.
 
Mkuu, hebu punguza nguvu kwanza maana nahisi ume engage 4WD kwenye lami. Hapa unamzungumzia Prof. Muhongo wa nishati na madini au Mulugo naibu wa Elimu?
 
Mleta mada umechemka, kufeli darasa la saba ndio huna akili? Moderator kindly delete this one!
 
Safi sana. Lakini si unajuwa huo uprofesa anaujuwa yeye kwani huyu jamaa ni mtaalam wa kughushi vitu hivyo hata uprofesa wake ni batili pia. Binafsi siamini chochote asemacho huyu jamaa. We profesa gani hajuwi historia ya nchi yake? Yaani ni afadhali angejichanganya kwa vingine lakini nchi ambayo yeye ni mtawala wa wizara? Aaaah, huku si kuchemka ila ni umagumashi wa kujitwisha vyeo asivyoviweza.

Unajivua nguo sasa kwa kung'ang'ana kuonyesha kuwa ulichoandika ndicho ulichomaanisha ilhali hujui kuwa umechemka, asiyejua historia ya nchi yake ni Philip MULUGO naibu waziri wa elimu na sio MUHONGO ambae ni wa nishati na madini, pia sio sahihi kudhani kuwa kila aliyeshindwa kwenda sekondari basi hana AKILI ZA DARASANI, huwa kuna mazingira mengine yanayoweza changia hali hii, istoshe siyo sahihi kudhania kuwa kilimo ni kazi ya waliokosa elimu, hiyo ni dhana potofu mno
 
Mkuu umechemka nadhani ulimaanisha Hon mulugo mwenye bachelor degree ya uchumi na historia(kanjanja)
 
nimesoma gazeti la habari leo na kukuta habari ya wanafunzi 44 waliofeli la 7 wako sekondari huko mkoani katavi. Hawa wanafunzi walifeli la 7 kwa sababu hawana akili za darasani, leo hii waje kwenda sekondari na chuo kikuu si tutapata viongozi dizaini ya waziri muhongo hapa? Jamani kwa nini hivi tanzania? Siyo kila mtu lazima awe kiongozi, pengine hawa watoto waliofeli ndiyo wakulima bora.

Chanzo: habarileo | gwiji la habari tanzania/index.php/habari-za-kitaifa/6055-waliofeli-la-saba-wakutwa-sekondari

investigative journalism au siasa blaa blaaa??????????
 
hivi kumbe kufeli darasa la saba huna akili? au huwezi kuwa kiongozi?????? hapo nimebaki njia panda
 
Unajivua nguo sasa kwa kung'ang'ana kuonyesha kuwa ulichoandika ndicho ulichomaanisha ilhali hujui kuwa umechemka, asiyejua historia ya nchi yake ni Philip MULUGO naibu waziri wa elimu na sio MUHONGO ambae ni wa nishati na madini, pia sio sahihi kudhani kuwa kila aliyeshindwa kwenda sekondari basi hana AKILI ZA DARASANI, huwa kuna mazingira mengine yanayoweza changia hali hii, istoshe siyo sahihi kudhania kuwa kilimo ni kazi ya waliokosa elimu, hiyo ni dhana potofu mno

Ni kweli na ninashukuru kwa kunisahihisha kwani niliandika kwa pupa. Badala ya kuandik Mulugo nikatia Muhongo....samahani wasomaji wenzangu na ahsante sana kwa kunisahihisha.
 
Mkuu, hebu punguza nguvu kwanza maana nahisi ume engage 4WD kwenye lami. Hapa unamzungumzia Prof. Muhongo wa nishati na madini au Mulugo naibu wa Elimu?

Nilikuwa na hasira na wala hata siku moja sikutaka kumaanisha Prof. Muhongo, samahanini.
 
Ndugu nadhani uko kasi sana ndo maana umechemka, jaribu tena kupata muundo wa baraza la mawaziri mimi nadhani unataka kumaanisha waziri philip mulugo wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi na si profesa muhongo wa nishati na madini,labda ututhibitishie ni wapi na lini huyu prof. muhongo alikosea historia ya nchi.

Ni kweli nilichemka lakini sikutaka kumaanisha Profesa....nilishikwa na hasira za ujinga wa utawala wa nchi yetu kwani listi ya mawaziri ilikuwa nyingi mu kichwa. Sintorudia tena kwani nitasoma kabla ya kupost.
 
kufeli la 7 si kukosa akili..wangapi walifaulu la 7 na form four waka score 0 ya 35 na wangapi walifeli la 7 na form 4 waka score div 1 ya points 7....kufaulu la saba n bahati tu.....
 
Waliofeli std 7 wanaweza kurekebisha kasoro zao na wakafaululu kwa distinction kwenye level za juu.Ni vijisababu tu vinavyo changia kufeli.Hivyo si vema kuwabeza wanaofeli na maisha yao ya baadaye.Kuna options nyingi kwa waliofeli ikiwa ni pamoja na kurudia darasa na kurudia mithihani.
Inaonyesha una hasira na Hon.Mulugo.Njoo na hoja strait forward na si kuzungukia waliofeli mitihani.
 
Back
Top Bottom