Onyango kagomea safari ya Sudan akidai kutoridhishwa kupigea banch

Onyango kagomea safari ya Sudan akidai kutoridhishwa kupigea banch

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Beki wa kati wa Simba, Joash Onyango amegomea kwenda nchini Sudan kwa ajili ya kucheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na Al Hilal ya Sudan.

Kikosi cha Simba kiliwasili salama Sudan jana mchana na Onyango hakuwa katika orodha ya wachezaji 18 waliowasili nchini humo kutokana na sababu ambazo alieleza kabla ya kikosi hicho kuondoka.

Inaelezwa kuwa raia huyo wa Kenya alikuwa katika orodha ya nyota waliotakiwa kusafiri ikiwemo kupata visa na tiketi ya ndege, lakini baada ya mazoezi ya mwisho kumalizika aligomea kwenda nchini humo.

Baada ya mazoezi kuisha, Onyango inaelezwa alimfuata kocha Zoran Minojlovic pamoja na meneja, Patrick Rweyemamu aliyowaomba kufanya nao mazungumzo ya muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda kambini.

Onyango inaelezwa aliwambia Zoran na Rweyemamu kuwa hapendezewi na suala la kuwekwa benchi kama ilivyokuwa katika mechi tatu za kimashindano zilizopita pamoja na baadhi ya stahiki zake za msingi kutokupatiwa hadi leo na uongozi kama walivyokubaliana katika mkataba mpya.

Kabla ya mazungumzo hayo kuisha, Zoran inaelezwa alimuelewa Onyango ila alimwambia anatakiwa kwenda lakini mwenyewe aligoma na kudai anabaki Dar es Salaam hadi masuala hayo mawili yatakapopata ufumbuzi.

Onyango yupo Dar huku akisubiri Simba kutoa uamuzi wa kumtimizia maslahi yake, kupewa nafasi ya kucheza mara kwa mara na kama itashindikana anaweza kuomba barua ya kusitisha mkataba wake.

Tangu kusajiliwa kwa Mohamed Outtara kutoka Al Hilal, amekuwa akicheza kikosi cha kwanza na Henock Inonga katika eneo la beki wa kati, huku Onyango akiishia katika benchi.
 
Yanga wanafurahisha sana yaani jambo la simba likitokea au kusikia hata kama ni uongo mnakimbilia kuanzisha uzi ila mambo ya yanga mnakaa kimya alivyogoma aziz ki kukaa hostel za wanafunzi kule avic town mbona hukuja kuanzisha uzi hapa utopolo pro max.
 
Huyo alie anzisha uzi ni 5imba mwenzako
 
Mechi tatu tu anaanza longolongo,mbona yeye alipokuja naye alimuweka mtu bench? Ni mapema sana kwake kuanzisha hoja hii. Nasikia uto wanamchombeza.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Yanga wanafurahisha sana yaani jambo la simba likitokea au kusikia hata kama ni uongo mnakimbilia kuanzisha uzi ila mambo ya yanga mnakaa kimya alivyogoma aziz ki kukaa hostel za wanafunzi kule avic town mbona hukuja kuanzisha uzi hapa utopolo pro max.
Sasa hivi Kambole naye kalianzisha tifu anataka apewe chake asepe lakini wanapiga kimya tu.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Yanga wanafurahisha sana yaani jambo la simba likitokea au kusikia hata kama ni uongo mnakimbilia kuanzisha uzi ila mambo ya yanga mnakaa kimya alivyogoma aziz ki kukaa hostel za wanafunzi kule avic town mbona hukuja kuanzisha uzi hapa utopolo pro max.
Umewahi kufika Avic town?
 
Back
Top Bottom